Juma Raibu awavua nguo waliomvua Umeya Moshi

Fred Mwakitundu

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
227
383
Aprili 11 mwaka huu baraza la madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Moshi lilifanya maamuzi magumu ya kung'oa kwenye kiti chake cha umeya,Juma Raibu ambaye ni diwani wa kata ya Bomambuzi .

Miongoni mwa tuhuma zilizomng'oa Raibu kwenye nafasi yake ni pamoja na madai ya rushwa katika utoaji wa vibali vya ukarabati na ujenzi kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya mipango miji ya manispaa ya moshi.

Kampeni ya kung'oa JUma Raibu iliendeshwa na madiwani 18 ambao kwa sasa wameunda kikundi ndani ya Baraza la madiwani kijulianacho kwa jina la M18 maana yake ni madiwani 18.

KInara wa kikundi hicho ni diwani wa kata ya Shirimatunda,Francis Shio pamoja na madiwani wengine wenye ushawishi akiwamo Deo Mallya,Abuu Shayo,JUma Mahamuod,Zuberi Kidumu na wengineo.

Hata hivyo wakati JUma Raibu aking'olewa kutokana na tuhuma hizo,bundi ametua kwa madiwani waliomchongea JUma Raibu baada ya kubainika kuwa nao ni vinara wakubwa wa rushwa katika ukarabati wa nyumba katikati ya mji wa moshi.

Juma Raibu ameanika majina sita ya madiwani anaowatuhumu kuchukua rushwa kwa watu mbali mbali kuruhusu ukarabati huku Shio akitajwa kuanza ukarabati kwenye nyumba moja ya kulala wageni ambayo ipo katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Nyumba hiyo ya kulala wageni iitwayo Kenyatta Lodge,ipo katikati ya mji wa moshi na anatajwa kuinunua kwa zaidi ya sh Milioni 200 huku mwenyewe akidai amefuata taratibu zote za kupata kibali toka ofisi ya mipango miji.

Tutaweka majina ya madiwani weanaotuhumiwa kwa rushwa hapa pindio tutakapowapata na kupata kauli zao.

Kaa mkao wa kula
 
JUma Raibu yuko uraiani au yuko magereza?​

Attachments

  • DBF7FAE4-F39E-4C47-B554-625B73100AF4.jpeg
    DBF7FAE4-F39E-4C47-B554-625B73100AF4.jpeg
    64.7 KB · Views: 27
Sasa haya si maneno tuu ambayo hayana ushahidi

Juma Raibu alikosea kitu kimoja Tuu kutoleta umoja zidi ya maadui zake wa kisiasa

Alipaswa kuwafanya marafiki hao 18 angalau nusu yake
 
We ndo huyo meya mfisadi ulieng'olewa? Ilikuwa wapi kutoa tuhuma za hawa madiwani hapo kabla!!? Huu ni utetezi tu wala hauna mashiko yeyote na kwa lugha nyingine tuseme ni kama unataka kulipa kisasi tu kwa hao waliovumbua madudu yako na kuyaweka hadharani .. Kwanza ulioaswa uwe mahabusu na sio uraiani.
 
Aprili 11 mwaka huu baraza la madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Moshi lilifanya maamuzi magumu ya kung'oa kwenye kiti chake cha umeya,Juma Raibu ambaye ni diwani wa kata ya Bomambuzi .

Miongoni mwa tuhuma zilizomng'oa Raibu kwenye nafasi yake ni pamoja na madai ya rushwa katika utoaji wa vibali vya ukarabati na ujenzi kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya mipango miji ya manispaa ya moshi.

Kampeni ya kung'oa JUma Raibu iliendeshwa na madiwani 18 ambao kwa sasa wameunda kikundi ndani ya Baraza la madiwani kijulianacho kwa jina la M18 maana yake ni madiwani 18.

KInara wa kikundi hicho ni diwani wa kata ya Shirimatunda,Francis Shio pamoja na madiwani wengine wenye ushawishi akiwamo Deo Mallya,Abuu Shayo,JUma Mahamuod,Zuberi Kidumu na wengineo.

Hata hivyo wakati JUma Raibu aking'olewa kutokana na tuhuma hizo,bundi ametua kwa madiwani waliomchongea JUma Raibu baada ya kubainika kuwa nao ni vinara wakubwa wa rushwa katika ukarabati wa nyumba katikati ya mji wa moshi.

Juma Raibu ameanika majina sita ya madiwani anaowatuhumu kuchukua rushwa kwa watu mbali mbali kuruhusu ukarabati huku Shio akitajwa kuanza ukarabati kwenye nyumba moja ya kulala wageni ambayo ipo katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Nyumba hiyo ya kulala wageni iitwayo Kenyatta Lodge,ipo katikati ya mji wa moshi na anatajwa kuinunua kwa zaidi ya sh Milioni 200 huku mwenyewe akidai amefuata taratibu zote za kupata kibali toka ofisi ya mipango miji.

Tutaweka majina ya madiwani weanaotuhumiwa kwa rushwa hapa pindio tutakapowapata na kupata kauli zao.

Kaa mkao wa kula
DAh akiwa mawenzi sekondari alikuwa na mambo ya ki*****
 
Back
Top Bottom