Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Kura 18 zimemkataa.

Alikuwa na kashfa ya kushiriki birthday ya shoga mmoja hapo Moshi.

Ni kashfa iliyotrend sana kwenye vyombo mbalimbali vya habari kama magazeti.

Nafikiri ndio hiyo imemng'oa labda kama kuna sababu nyingine tutajua

Kapigiwa kura Leo, 18 zimemkataa na 10 zimemkubali.

Juma Raibu.jpg

BARAZA la Madiwani Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, limepiga kura za siri za kumuondoa Meya Juma Raibu madarakani kutokana na tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili.

Awali akisoma taarifa ya timu ya uchunguzi ya Mkoa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Rashid Gembe, amesema Meya huyo, Juma Raibu, alikuwa akikabiliwa na tuhuma mbalimbali zilizowasilishwa na madiwani wapatao 20.

Baadhi ya tuhuma hizo ni kutumia nafasi yake vibaya, kutowaheshimu viongozi wanaohudhuria vikao na mikutano ya Halmashauri, kushiriki vitendo vya rushwa katika ujenzi holela (CBD), mienendo mibaya na ukosefu wa adabu kwa madiwani wenzake, ukosefu wa maadili na kushiriki sherehe za watu wa jinsia.

Akitangaza matokeo hayo leo, mara baada ya kura kupigwa, Mkuregenzi huyo amesema jumla ya wajumbe halali waliopiga kura ni 28 sawa na asilimia 100, ambapo kura za ndio ( za kumuondoa Meya ) zilikuwa 18 sawa na asilimia 64.3, huku kura za hapana zilikuwa 10 sawa na asilimia 35.7.

Kutokana na hali hiyo alisema kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Baraza la Madiwani Mwaka 2015 kifungu cha 5.2, kanuni hiyo imetumika kumuondoa madarakani Meya huyo.

Wakizungumza kwa niaba ya Madiwani wenzao, Diwani wa Kata ya Miembeni, Mohamed Mushi na Diwani wa Kata ya Mji Mpya, Abuu Shayo, wamesema wameridhishwa na uamuzi wa baraza kutokana na mwenendo mbaya aliokuwa nao Juma Raibu.

Kwa mujibu wa kununi hizo, Naibu Meya, Stewart Nathaniel ataendelea kushikilia nafasi ya Meya hadi atakapopatikana Meya mpya.

=========================

Pia soma
 

Attachments

  • video5954133533474687675.mp4
    3 MB
20220411_140933.jpg

Bazara la Madiwani Manispaa ya Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro, leo limemng’oa Meya wa manispaa hiyo, Juma Raibu, kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuhudhuria sherehe ya mashoga. Kati ya kura 28 zilizopigwa, zilizomkataa 18 sawa 64.3% na 10 zikiwa upande wake sawa 35.7%
 
Back
Top Bottom