wala huhitaji kunieleza yote hayo. nayajua sana tu. nilichokiandika ungekisoma btw the line wala usingehangaika na haya. Ukweli ni kwamba wanachofanya serikali ya ccm sio sahihi hata kidogo, na hilo liko wazi kwa kila mmoja mwenye akili kama MIMI. ila mimi kwa upande mwengine nina furaha sana kwa anachokifanya magufuli. Kikwete aliwapa uhuru sana karibia wa kila kitu. mkaishia kumtukana na hata wengine kutaka kumdhalilisha kabisa. sasa acha kwanza muone upande wa pili wa shilingi ili siku nyingine mjifunze.
Mama Makinda pia mlimtukana sana wakati kiukweli kabisa alikuwa fair sana mpaka na kumuita majina ya ajabuajabu kama bibi kiriboto. sasa mmekutana na mkono wa chuma wa joka la makengeza.
nasema na iwe hivyo ili siku zijazo iwe fundisho kwenu na kwa vizazi vyenu vijavyo.