Julius Mtatiro: Vyama vya Upinzani ni Mali za Watu binafsi, Vijana ondokeni Upinzani mjiunge CCM

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa chama cha wananchi CUF taifa, Julius Mtatiro ambaye miezi kadhaa iliyopita amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewataka vijana kuvikimbia vyama vya upinzani hapa nchini kwani ni mali za watu fulani.

Mtatiro ameyasema hayo leo jioni wakati alipokuwa akimnadi mgombea wa jimbo la Ukonga kwa tiketi ya CCM ndugu Mwita Waitara katika kampeni zilizofanyika eneo la Pugu Kajiungeni jimboni humo na kuwataka vijana kuachana na vyama vya upinzani na kujiunga CCM ambapo ndicho chama kinachopigania maendeleo ya Watanzania kwa ujumla.

"Msishangae kabisa vijana wengi wenye akili zao timamu wakaendelea kuondoka vyama vya upinzani wakahamia Chama Cha Mapinduzi ni maamuzi tu, vyama vya upinzani vinawachukulia vijana for granted, mimi nimekaa upinzani kwa miaka 10 nimefanya juhudi kubwa sana kurekebisha makosa makubwa ambayo yamekuwa yakifanywa na vyama vya upinzani lakini mwisho wa siku vyama vile vimeshikiliwa na watu" – Amesema Julius Mtatiro.

Mtatiro amewasihi wananchi wa jimbo la Ukonga kumchagua Mwita Waitara kuwa mbunge wao kwa maendeleo ya jimboni hapo huku akielezea historia ya uongozi aliyonayo mgombea huyo tangu alipokuwa rais wa wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam na harakati za kupigania haki ya kupewa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchi nzima.

“"Mkimpata Waitara kuwa mbunge wa Ukonga na mara hii akitokea kwenye chama kinachoongoza dola akiungana na viongozi wa mkoa, wakuu wa wilaya, mawaziri na akiungana na chuma John Pombe Magufuli mambo ya Ukonga yatakwenda mbio sana" - Mtatiro.

Aidha amewataka wananchi kuacha ushabiki wa vyama na kumchagua mgombea huyo wa CCM na kuwahakikishia wana Ukonga kuwa wamempata mbuge imara na sio legelege.

Pia amefunguka suala la viongozi wa upinzani kununuliwa ili kujiunga CCM ni propaganda kwani kuhama chama si usaliti.

"Kuna watu wanazungumza mtaani kuwa Waitara kanunuliwa, tena wengine wanaenda mbali eti eneo hili kuna ndugu zetu Wakurya nataka niwaeleze kuhama chama si kusaliti" – Ameongeza Julius Mtatiro.

Chanzo; Dar Mpya
 
Back
Top Bottom