Julius Mtatiro apandisha jazba kuhusu Tamko la Chadema kutoungana na CUF Bungeni

Mtatiro anajaribu kuokoa jahazi linalozama kwa kasi kubwa, kumbe nani mwingine mwenye haiba japo kidogo pale CUF? Prof Safari kajiengua, Hamad rashid nazidi kushuka hadhi kwa uroho wa madaraka bungeni, Lipumbe si mtu wa propaganda; sas nani azue propaganda na kubwabwaja? Mtatiro you are in a sunken ship
 
chadema wameikaba lini, ok masikio yangu hayasikii, naomba nibandikie hapa nilione.
mi nishatoa msimao wangu huko juu kaka,sihitaji kurudia. we hata usipoamini sawa tu, mi nimeshajitambua na sikushangai sana coz i was once like you remember?

Kuhusu DOWANS, tamko la KK ya CDM lilikuwa hivyo
 
Attachments

  • TAMKO.doc
    27 KB · Views: 54
Carmel naona umeivalia njuga post hii ya Mtatiro,lakini reading btn lines inaelekea una kitu na Mtatiro siyo bure. Mimi sioni logic ya kupinga the obvious!!! Hata naona sasa mawazo yako yanaiabisha picha hiyo uliyoitumia kama ID yako maana mwenyewe ana busara sana. Nini cha ajabu CDM kukataa kushirikiana na CUF ? Sababu nyingi zimetolewa sasa nini ni kigumu kuelewa?
 
Heshima kwako Mohamed Shossi,

Mkuu unapoteza muda wako bure hawatachelewa kukuita majina ya ajabu ajabu bora unyamaze wasijekutoa macho ukabaki na chongo.Sioni tatizo la CUF kutoshirikiana na CHADEMA bungeni.Ikiwa CUF wanatengwa kwasababu ya kushikishwa kwenye SUK Zanzibar NCCR Mageuzi au UDP nao wameshikishwa huko Zanzibar ?.Naamini CHADEMA wameanza kulewa sifa na ulevi wa madaraka sioni sababu za msingi zaidi ya kutaka kuonekana wana haki kuongoza upinzani wenyewe bungeni.Nilishangaa sana kipindi cha uchaguzi wa spika CHADEMA waliwaandikia barua CUF wawaunge mkono wakati huo huo hawataki kuwashirikisha kuunda kambi ya upinzani.Tusikubali kushabikia kila jambo bila kulichunguza na kuridhisha akili zetu.

Nina amini kambi moja ya upinzani bungeni ni jambo jema CUF kushirikiana na CCM si dhambi.
Tukijadili mwaka 2000 na hata mwaka 2005, CUF waliwaalika wabunge wa vyama vingine kuunda upinzani rasmi si kwa sababu ya kupenda, ila kwa sababu kikanuni wasingeweza kuunda kambi hiyo kivyao.
Kwa maneno mengine, kanuni ndizo ziliwafikisha CUF kuwa na uchaguzi wa kushirikiana na vyama vingine kuunda upinzani rasmi bungeni si mapenzi kwa vyama vingine na kutaka kuwatumikia wananchi kama ambavyo Hamad Rashid anataka umma usadiki leo.

Lakini suala la sasa la ushirikiano wa CUF na Chadema ni tata zaidi kuliko hata kwa hoja ya idadi ya wabunge na kanuni tu, CUF ni shehemu ya serikali ya CCM walau kule visiwani Zanzibar, lakini kwa mujibu wa muundo wa Muungano wa Tanzania , serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina muunganiko na serikali ya Muungano. HIVYO KWA MANENO MENGINE CUF IS WAPINZANI

Rais wa Zanzibar ambaye ndiye anashirikiana na CUF kule Zanzibar akiwa anatoka CCM ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri la rais Jakaya Kikwete, yaani serikali ya CCM.Hawa wanakubaliana kwa pamoja katika Baraza la Mawaziri la Muungano na Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa sasa wa Zanzibar hawezi kuacha kuwa sehemu ya makubaliano hayo, kama ambavyo Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, hawezi kukwepa kuwa sehemu ya makubaliano ya pamoja katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Source: Hamad Rashid anatamani kuwa popo | Gazeti la MwanaHalisi
 
Mimi sijai attach chadema, ni nyie wanachadema ndo mna attack vyama vingine kila siku. na mi sijajiona bora zaidi yako au mwingine, so acha kulalama kaka, jibu hoja. ni nani wanaotukanaga watu wa vyama vingine hapa kila kukicha? na nilishakwambvia mi si cuf, wala, ccm, wala chadema, sina kadi ya chama chochote, natetea maslahi ya nchi kaka, take it or leave it. hakuna anayekulazimisha kukubaliana na hoja zangu. bye peolpe, naona nyongo zinapanda

Kwanza nikuhakikishie kwamba huna uhakika kama mimi ni mwanachadema. Kama ungebahatika kusoma thread ya wabunge wa viti maalum chadema iliyotolewa na kitila mkumbo ndo ungejua kama mimi ni mwanachadema ama la. Lakini pia hainipi shida kukunasibisha na cuf, kama sio mwanachama basi wewe ni mshabiki, na hili halihitaji macho ya ziada kuliona.
Unapowanyooshea kidole wenzako kwamba ndio wanatukana huku wewe ukijiona msafi ni kichekesho, soma maandiko yako vizuri utaona jinsi ulivyotukana tena thread hii hii huitaji kwenda mbali, na ndio maana nikasema ni vizuri kukubaliana kutokubaliana kuliko kutoa matusi ya kireja reja na kujikweza. Manake wakati mwigine ninapata shida mtu kujiona bora kuliko wenzake wakati wamekutana kwenye key board na hakuna anayemsaidia mwenzake kusurvive na hatuko hapa kutaja ninini tulicho nacho na vyeo ama utajiri ni kila mmoja kivyake, cha msingi ni kwamba wote tunakutana hapa jf kila mmoja kwa njia yake.

Narudia kusema huwezi kutetea maslahi ya nchi kwa kupiga kelele tu, kama huoni umuhimu wa kushiriki kutetea maslahi ya nchi yako japo hata kwa kupiga kura na upo ndani ya nchi hii, ni aibu kusema kwamba nawewe unatetea maslahi ya nchi hii, na kwa hali hii nashangaa ni kwa namna gani unaweza kuandamana kama huwezi kupiga kura.
 
Heshima kwako Mohamed Shossi,

Mkuu unapoteza muda wako bure hawatachelewa kukuita majina ya ajabu ajabu bora unyamaze wasijekutoa macho ukabaki na chongo.Sioni tatizo la CUF kutoshirikiana na CHADEMA bungeni.Ikiwa CUF wanatengwa kwasababu ya kushikishwa kwenye SUK Zanzibar NCCR Mageuzi au UDP nao wameshikishwa huko Zanzibar ?.Naamini CHADEMA wameanza kulewa sifa na ulevi wa madaraka sioni sababu za msingi zaidi ya kutaka kuonekana wana haki kuongoza upinzani wenyewe bungeni.Nilishangaa sana kipindi cha uchaguzi wa spika CHADEMA waliwaandikia barua CUF wawaunge mkono wakati huo huo hawataki kuwashirikisha kuunda kambi ya upinzani.Tusikubali kushabikia kila jambo bila kulichunguza na kuridhisha akili zetu.

Nina amini kambi moja ya upinzani bungeni ni jambo jema CUF kushirikiana na CCM si dhambi.

Kiongozi salama mkuu,

Usiishie kuishangaa chadema kuomba kuungwa mkono na cuf kwenye uchaguzi wa spika, pia jitahidi kushangaa ni vipi cuf walimpigia kura mgombea wa ccm halafu tena wanaandika barua kwa KUB kuomba kushirikishwa kwenye kambi ya upinzani.
Ule uchaguzi wa spika na naibu wake ulikuwa ni mtego tosha kuwajua cuf wako upande gani.
Kama ni ulevi wa madaraka basi wanao cuf wanaoshiriki kuunda SUK Zanzibar at the same time wanataka wakaribishwe kambi ya upinzani.
 
Carmel naona umeivalia njuga post hii ya Mtatiro,lakini reading btn lines inaelekea una kitu na Mtatiro siyo bure. Mimi sioni logic ya kupinga the obvious!!! Hata naona sasa mawazo yako yanaiabisha picha hiyo uliyoitumia kama ID yako maana mwenyewe ana busara sana. Nini cha ajabu CDM kukataa kushirikiana na CUF ? Sababu nyingi zimetolewa sasa nini ni kigumu kuelewa?

i have come to learn that it is too expensive to be a great thinker. Hao waliochagua hiyo slogan nimewavulia kofia
 
Kiongozi salama mkuu,

Usiishie kuishangaa chadema kuomba kuungwa mkono na cuf kwenye uchaguzi wa spika, pia jitahidi kushangaa ni vipi cuf walimpigia kura mgombea wa ccm halafu tena wanaandika barua kwa KUB kuomba kushirikishwa kwenye kambi ya upinzani.
Ule uchaguzi wa spika na naibu wake ulikuwa ni mtego tosha kuwajua cuf wako upande gani.
Kama ni ulevi wa madaraka basi wanao cuf wanaoshiriki kuunda SUK Zanzibar at the same time wanataka wakaribishwe kambi ya upinzani.
Tena eti mgombea badala ya kueleza kwa nini achaguliwe yeye anajitoa..........!!! hii ni ajabu..............alafu unadhani kujitoa kwa mgombea yule kulikuwa ni kwa maamuzi yake binafsi.........!!! (kwa kiswahili kisicho rasmi) ALIJITOA KWA VILE ALIONA ANAJIPINZANIA MWENYEWE
 
Kiongozi salama mkuu,

Usiishie kuishangaa chadema kuomba kuungwa mkono na cuf kwenye uchaguzi wa spika, pia jitahidi kushangaa ni vipi cuf walimpigia kura mgombea wa ccm halafu tena wanaandika barua kwa KUB kuomba kushirikishwa kwenye kambi ya upinzani.
Ule uchaguzi wa spika na naibu wake ulikuwa ni mtego tosha kuwajua cuf wako upande gani.
Kama ni ulevi wa madaraka basi wanao cuf wanaoshiriki kuunda SUK Zanzibar at the same time wanataka wakaribishwe kambi ya upinzani.

Nikiri tu kwamba leo nimeshikwa na butwaa namna watu wamejitokeza hapa kuponda washabiki wa chadema kwama siyo great thinkers kwa kuwa tu wanaorodhesha ushahidi kwamba cuf siyo chama cha upinzani. Watu hao wakashindwa kabisa kunishawishi kwamba wao ni great thinkers. Kwamba great thinking imekuwa relative, yaani inategemea anaye ku judge yuko upande gani wa mawazo yako. kama yeye ni cuf na wewe umesifu cuf basi wewe ni great thinker. vivo hivyo na vyama vingine.

narudia kukiri, leo nimejifunza sana
 
Katika wanasiasa wa kutumainiwa kwa ajili ya nchi hii Mtatiro naye yupo?!!HAPANA
Mtatiro ana sifa kuu zifuatazo, ambazo sisi tuliofanya nae siasa pale Chuo Kikuu tulimfahamu, na tukamtoa kwenye KUNDI LA WANASIASA-VIONGOZI WA BAADAE WA KTUMAINIWA NCHI HII:

1. Ni mtu wa kuongea tu kabla ya kufikiri..Hufikiria baada ya kutenda..
2. Hatumii logic, hupanic sana...
3. Ana vunga ana msimamo lakini muda wowote anakupotezeni..mfano: Tulipofanya mgomo kuishinikiza serikali kutoa kipengele cha madaraja katika kugawa mikopo, tukafukuzwa miezi miwili..katika kufanya juhudi za kuwarejesha wanafunzi wote salama, sisi vionogzi tulibaki Dar es salaam tukikutana na kujadiliana..haikuchukua muda akatukimbia na kukimbilia Kenya kwa ndugu zake..kisa uoga kwa Serikali.
4. Ni kiongozi mwenyye tamaa na ulafi wa madaraka kila alipo..wengi watakumbuka alivyomlipa fadhila Rais aliyemteua Deo Daudi, kwa kuendesha hila aangushwe madarakani.
-Vivyo hivyo aliwahi kuhatarisha serikali ya Mwita Magesa kuangushwa madarakani, wakati huo akiwa ni waziri wake..Mwita ilibidi amtimue madarakani..ingawaje huwa anatamba kuwa alipeleka barua ya kujiuzulu mapema..si kweli.
5. Ana 'madudu' yake ambayo hutaka kuyatimiza kwa gharama yoyote ile..aliwahi kuishinikiza kamati fulani ya uchaguzi pale DARUSO iwapitishe 'madada' flani kuwa wagombea...kamati ile hata hivyo iliwabwaga kwa kukosa vigezo...ile ilileta uhasama kwake na kwa wanakamati wale.

Huyo ndio 'mwanasiasa' MTATIRO KWA UCHACHE...
Hayo ya CHADEMA NA CUF ayajibu kwa hoja.......sio kuongea tu ilimradi anaongea

Mkuu hayo nimekwisha yaona kwa huyo kijana Julius Mtatiro, nadhani anatakiwa abadilike ..la sivyo ataishia kuwa kama Yusuph Makamba
 
Kuhusu DOWANS, tamko la KK ya CDM lilikuwa hivyo

Ahsante sana kiongozi kwa hii atachment.
Nadhani dada yangu carmel amejichimbia mahali muda huu anajisomea tamko la cdm, akimaliza atakuja kutwambia kama dowans ametajwa kwenye hilo tamko ama la.
 
Nikiri tu kwamba leo nimeshikwa na butwaa namna watu wamejitokeza hapa kuponda washabiki wa chadema kwama siyo great thinkers kwa kuwa tu wanaorodhesha ushahidi kwamba cuf siyo chama cha upinzani. Watu hao wakashindwa kabisa kunishawishi kwamba wao ni great thinkers. Kwamba great thinking imekuwa relative, yaani inategemea anaye ku judge yuko upande gani wa mawazo yako. kama yeye ni cuf na wewe umesifu cuf basi wewe ni great thinker. vivo hivyo na vyama vingine.

narudia kukiri, leo nimejifunza sana

Utashangaa sasahivi kuna watu hawataki kuuona ukweli na kuukubali.
Ukionekana una mawazo tofauti na yake basi ishakuwa taabu, yani ni kama vile wao ndo wenye haki ya kusema kwakuwa hawana vyama wako"neutral". wengine tukisema, tunaambiwa nyie wanachadema wakati hata ofisi za cdm wilayani kwangu sijui zilipo.
 
Ahsante sana kiongozi kwa hii atachment.
Nadhani dada yangu carmel amejichimbia mahali muda huu anajisomea tamko la cdm, akimaliza atakuja kutwambia kama dowans ametajwa kwenye hilo tamko ama la.

Hajarudi bwana, hata mimi nilikuwa namsubiri
 
Mtatiro yuo are in a wrong side, sit down and think if realy CUF is the right place for you. I think you have a good intension at the same time you have conflict of interest. Why dont you look for the real oposition party of join CCM.
 
Kwa mtazamo wangu, wapinzani kuungana au kuto kuungana kunaweza kusiwe na mantiki sana kwa wakati huu, ingwa kwa mimi ninavyo muona Mtatiro, angekuwepo Bungeni angaliweza kuleta changamoto ya namna yake pale kwani, hata kama alisha wahi kuchemka alipo kuwa chuoni lkn hii ni level nyingine kabisa, kitu ambacho nataka kumkosoa, asingepaswa katu kusimama kugombea ubunge Ubungo, kuna majimbo ambayo yeye kama yeye angeweza kupata kwa umuhimu na chama alichokuwemo, kwasasa ajipange tu, na ikibidi awe na hypothesis ambazo hazita muangashusha ni vema akasimame na wagombea dhahifu kuliko kuangalia upinzani majimboni kama tunapiganisha mabondia, yeye ni kichwa kwa nafasi yake, kwasasa hata kama wataungana hata kuwa na kubwa lolote. kwasasa atulie ale matunda ya ukatibu pale basi inatosha, makumbuka Ahmad Rashid alishindwa kabisa kufincha kilicho kuwa kina msikuma kung'ang'aniza muungano wa upinzani mpaka akasema oooohhhh unajua zile pesa milioni 100 ni nyingi kwahiyo tuungane tuzipange sawsawa, sasa Ntatiro asije akijipaka rangi mbaya, akomae na kupambana hali akiwa nje ya bunge, ya muungano ya nini? ukiachia sababu za kwanini wasiungane au waungane.
 
Back
Top Bottom