Julius Mtatiro amenifanya niandike...

Julius Mtatiro amenifanya niandike...

Mtatiro anatafuta cheo tu full stop.
Inasemekana toka amalize degree yake Mlimani pale alipoingia mtaani hajapata kazi ya uhakika ya kujipatia kipato.
Kaona CUF anashinda na njaa tu alafu Ruzuku yote keshakomba Lipumba.
Hahahhaaa. Njaa mbaya kweli aisee.
 
KAMA WEWE UNAVYPATA TAABU SANA BAADA YA BIASHARA YA KUBEBA MABOX KUPIGWA PIN KWA TRUMP
 
F**k wanasiasa wote ni wanafki
Njaa zinawasumbuaa na hamjui kukabiliana na pilika za maisha
Nyie ni wanafki forever

Ova
 
Moja ya sababu ya Julius Mtatiro mmoja wa vijana waliokuwa wakihoji kutaka maendeleo ya haraka ya Tanzania kuhama upinzani leo ni sababu inayofikirisha sana.

Ni sababu inayosadifu mwelekeo wa siasa za Tanzania katika zama hizi mpya.

Julius ameeleza sababu ya kuondoka alikokuwa ili "akapate zaidi fursa ya kufanya siasa za maendeleo."

Hakika niemwelewa, Siasa katika asili yake si mchezo mchafu kama baadhi wanavyotaka kusema...Nadharia sahihi ya siasa ni maendeleo.

Hakuna mwanasiasa awe yeyote wa kweli anayeweza kusema anafanya siasa kwa ajili ya mzaha. Siasa msingi wake ni kutafuta fursa ya kufanya au kuleta maendeleo.

Ndio maana siku Dr. Slaa alipoona CCM wamembania alitafuta fursa Chadema ya "kuleta maendeleo."

Siku Lowassa alipoona CCM hana nafasi akaenda Chadema kutafuta "fursa ya kuleta maendeleo."

Ipo mifano mingi lakini nimalizie pia kuwa hata Zitto Kabwe alipoona Chadema hakuna fursa alihamia au kuanzisha ACT ili kupata fursa ya "kuleta maendeleo."

Julius Mtatiro namfahamu bayana kuwa anaamini katika Tanzania yenye neema tele.

Tanzania yenye ukuaji mzuri wa uchumi, Tanzania yenye uongozi unaofanya uamuzi kwa maslahi ya nchi na watu wake.

Namfahamu Julius kuwa kijana anayeamini katika kupinga rushwa, ufisadi na anayeamini katika siasa za kuwaletea wananchi maendeleo.

Rais Magufuli anayafanya yote haya ya maendeleo: amekuza uchumi, ameongeza mapato ya Serikali, amepiga vita rushwa na ufisadi ipasavyo, anatekeleza miradi mbalimbali ya kuwaondoa Watanzania katika unyonge na anasimamia mageuzi ya kimaendeleo.

Sikupata fursa ya kumuuliza Julius anaamini siasa ni nini lakini kwa leo ametupa jibu kuwa yeye ni muumini wa siasa za maendeleo na siasa ambazo ndio msingi wa utawala wa Rais John Pombe Magufuli.

Kwa muktadha huu sitashangaa wanasiasa wote wanaoamini katika maendeleo wakiungana na JPM na kuwaacha wale wanaoamini katika siasa ni mchezo mchafu wabaki huko huko kwenye michezo michafu.

*Anaandika PoliticalJurist, formerly UDOM, MA student London*
hivi siasa za maendeleo ni zipi hasa ,hivi upinzani unaposema watu wanauawa siyo hoja? Kupiga waandishi wa habari ni siasa za maendeleo? Kuzuia bunge live ni siasa safi? Kutopandisha watumishi mishahara ni siasa safi? Kujenga reli wakati wanachi hawana uchumi imara ni sifa? Kumpiga tundu LISSU lisasi wakati waliopitisha mikataba ya hovyo wapo ni sawa? kununua ndege tena yenye hasara kila mwaka ambayo bunge halijapitisha ni siasa safi...?
Siasa safi unayo maanisha ni jokate kuwa mkuu wa wilaya..... Siasa safi unayotaka ni patrobas katambi kuthaminiwa kuliko nape nnauye anaetaka wakulima wa korosho wathaminiwe..... Poor, poor,,, poor
 
Hii nchi sio ya kuamini unaeza ukalala moshi asubuhi ukajikuta upo Kongo
 
Huyu ndiye alietuaminisha kua ccm inanunua wapinzani vipi nae kanunuliwa?
 
Kupinga ni asili ya mwadamu

Upinzani ulikuwepo
Upinzani uPO
Upinzani utakuwepo mpaka mwisho wa ulimwengu

uko sahii mkuu
nadhani wakati mrema watu wanasukuma gari lake ili asitumie mafuta mtatiro alikuwa bado ananyonya.
kigoma malima akihutubia kipindi hicho nadhani mwita alikuwa analima tarime.
kasangatumbo akiunguruma viwanja mbalimbali nadhani bwana mtulia alikuwa anavalishwa nepi
so hii inakuonyesha kuwa mmoja akiondoka anawaachia nafasi wengine pia wajitokeze,
madrid alikuwepo raul akaondoka.akaja figo,delima zidane,ronaldo nasasa nae kaondoka very sooon kuna mwingine ata take chances
 
Mwanasiasa sio wa kumwamin hata akikwambia usiku mwema toka njee uhakikishe kama kuna giza
 
Mtatiro au mtaro au vyovyote uwavyo sitokuamini kwa chochote kile kitokacho kinywani mwako iwe umeteuliwa au raia wa kawaida!
Hakika umenipa funzo kubwa sana maishani mwangu! Nakuapia sio mm tu nahis hata watu wako wa karibu kabisa wanakuangalia kwa jicho la hofu na mashaka! Hate huko ulikohamia bado kuna watu wanakuogopa zaidi ya ukoma!
Utavaa na kutamba majukwaani kama wao ila still hawatokuamini kamwe!
Mwanaume wa kweli humpokea kwa mashaka mke alomsaliti mmewe kwa tamaa za mali
 
Kuna kitu kikubwa sana kinapangwa kwa siasa za nchi, tuwe tayari kwa lolote. Na wala siyo zuri kabisa, moyo unaniuma sana kwa mustakabali wa nchi yangu.
Sina maslahi yoyote binafsi na upinzani wa nchi hii zaidi ya kuusupport kwa maslahi ya nchi.
Yanakatisha tamaa Ila tupeane moyo siku ipo demokrasia huru itapatikana ndani ya nchi yetu.
Hakuna kisichokuwa na mwisho, Mungu anajua kwanini anaamua kutupisha huku ambapo sisi kama binadamu tunaona ni kugumu lakini yeye anajua kwanini iwe hivi.
Wala tusife mioyo hata kama inauma, ni kama mwanga hauonekani lakini mi imani yangu ni kwamba mwanga utaonekana.
Siasa za kiafrika bado ni ngumu sana kwa wapinzani, vijana wengi walioko upinzani wanaona mapambano wakiwa upinzani unawachelewesha kula national cake wakati vijana wenzao walioko chama tawala wanakula na kusaza wakati wanaamini wanauwezo mdogo kuliko wao.
Tubaki na upinzani mioyoni kwetu tukiwa katika jitihada za kutafuta njia ya kupita, itakapoonekana basi tuwe tulioimarika zaidi, kuliko walio kata tamaa.
Mungu awe nanyi wote mnaoupigania upinzani kwa maslahi ya Tanzania yetu, tusife moyo.
 
maadam liwasa yupo chama kile...
mpaka bint mdee anatoka!
same case kwa vyama vingine!
Tz hakuna upinzani wa vyama@
 
Poleni sana wanajukwaa mliotega masikio kuhusu mambo mbali mbali. Pole zangu kubwa ziende kwa waliopotelewa na wapendwa wao hasa wale waliopotea wakihusishwa na mambo ya kisiasa....

Poleni sana wanahabari kwa matukio yanayochipua taratibu dhidi yenu ,kwa kuwa mimi siyo mwanahabari sina cha kuwafundisha kwa kuwa sijui mnafundishwa mbinu gani mkiwa kwenye masomo yenu, ila poleni sana ndugu zangu...

Poleni sana waumini wa siasa tena siasa ya tanzania. Nami naomba nijipe pole kwa sababu pia ni muumini....

Baada ya pole hizo nirudi kwenye mada yangu ya msingi...

Kwanza niwakumbushe wanabodi wenzangu kuwa toka matokeo ya urais,wabunge na madiwani utangazwe mwaka 2015 hatujawahi kumaliza mwaka bila kuingia kwenye uchaguzi aidha wa wabunge au madiwani... Maana yake toka mwaka huo tuko kwenye uchaguzi mpaka leo.. Uchaguzi haujaisha..Na tutaendelea hivi mpaka 2020 na ikumbukwe rais alitoa agizo la watu kutofanya siasa zisizo za msingi ili nchi "Iconcentrate " na ujenzi wa nchi.. Lakini mpaka leo hatujamaliza uchaguzi.. Sababu mnazijua

Wanasiasa wamekuwa wakihama sana hasa kutoka upinzani kwenda kumuunga mkono mheshimiwa rais, lakini wote waliokuwa wanahama hawakuwahi kunitesa sana kwa sababu wengi wao nilikuwa nawaelewa vizuri..

Leo kuna kijana mmoja ambae sitaki nimuite mwanasiasa kwa sababu ambazo nilikuwa nampa... Huyu ni julius mtatiro...

Huyu ni moja ya vijana wachache niliokuwa ninahisi hawana maisha ya "Utikiti maji " anaejitambua sana,, ambae amejijenga katika mtazamo wa self reliance hivyo kutoishi maisha ya kinafiki. Lakini leo nimemsikiliza na kupata hofu kidogo... Wakati napata hofu nikajiuliza maswali machache

1: Nini maana ya upinzani wa kisiasa?

2: Upinzani ulianza kipindi kipi?

3: Je, kipindi upinzani unaanza ulikuwa unahitajika sana kuliko kipindi hiki?

4: Ikitokea CCM ikafuta "Political leaders" wote wa upinzani hasa wabunge nini kitatokea?

5: Je, upinzani unazuia rais na watendaji wake kujenga nchi??

6: Kuna nchi ngapi ulimwenguni hazina vyama vya upinzani?....

Wanabodi nisema tu wazi mimi siyo mpinzani ila ni muumini wa mawazo pevu... Kuna muda nchi yetu inahitaji mawazo chokonozi ili isonge mbele, na mara nyingi mawazo hayo huwa hayatoki kwa mabosi.. Hutoka kwa walala hoi. Hawa ndiyo wajenga nchi.. Wanajua matamu na machungu zaidi...

Baada ya kuwasikiliza wote wanaohama na leo mtatiro nimegundua machache

1: Mitaala yetu ya elimu ni mibovu sana (watanielewa wachache).

2: Mabadiliko ya nchi kama tanzania hayatafanywa na wanasiasa bali wananchi tu.

3: Hata CCM ibaki yenyewe upinzani haufi.... (nitaeleza)

4: CCM hakuna inachokifanya cha kuwaweka madarakani milele ndiyo maana wanaogopa kuruhusu mashindano ya kisiasa...

Mwisho niwakumbushe point yangu namba tatu above... Upinzani siyo mbowe, siyo lissu, siyo zitto, siyo wapinzani... Upinzani ni tafsiri ya mioyo ya watu.... Anaweza kutoka mbowe, lissu ila mioyo ya watu ikaendelea kujenga upinzani mkali zaidi..... Natamani upinzani wa majukwaa uishe ili tuanze moja.. Tutakuwa na mapinduzi na siyo upinzani. Msifadhaike sana mnaoamini mawazo mbadala.

Wasaaaaaaaaalam...

Mwananchi wa kawaida

Wewe ni Mpinzani uchwara. Kama kweli we mtz. Unaweza kusema kwa dhati tatizo La Tz ni Mambo ya kuwepo Upinzani Au Hapana. Is that the first and biggest problem or challenge that we face as Tanzanians. Mi mtz Ingawa naishi nje. Mwaka 2014-2015 kila ofisi ni siasa tu Hakuna kazi. Baada ya uchaguzi tena mnataka siasa. Lini Watu watafanya kazi. Uvivu ndo inawafanya mkae na kuwaza Haya Mambo. Kwani Mbunge kama Lissu akihimiza Vijana waache bangi walime nyanya atakuwa sio Mpinzani. Upinzani wenu ni Wa kijinga kipumbavu na hauna tija. Mnasahau kuwa swala Akifeli kiongozi tunafeli na sisi. Umeona wapi wapinzani wananuna kama miundo mbinu Au Ndege Au Reli nk vikiboreshwa. Tena mtakazana kuanzisha Mauzi ili tu Mambo haya yasionekane muhimu. That’s why I see you people as stupid and I am still wondering if you are really Tanzanians. Be proud of your country Kama vile katika familia Ndani ya nyumba mama na baba wanavyoficha vituko vya Familia. Hakuna Mzungu pamoja na majanga yao Mengi tu atakayekusimulia wewe mabaya ya Nchi yake mpka iwe ubest kweli lakini usijisahau ni wazalendo Kwanza. We kaa kimya. Sivyo utareportiwa then maisha yako yatakuwa magumuuuuuu.
 
Huu uzi Nimeulewa sana

Na mm nikazie tuu,, Upinzani sio hivyo vyama vya siasa,

Upinzani uko mioyoni mwa watu,,huko ccm kwenyewe sidhani km wanafurahia haya yanayoendelea
 
Mtoa mada huna la maana lolote ktk mada yako......wewe sema tu huipendi CCM na hayo mapinduzi unayoyataka kamwe si Tanzania labda huko kwenu Congo.............
 
Magufuli na serikali yake kama wanataka kuua upinzani wanaweza kufanya jambo bila kuliingizia taifa gharama za uchaguzi.

Wapeleke hoja bungeni ili kufanya maboresho kwenye katiba na sheria ya vyama vya siasa.

Kwamba wanaweza kuweka kipengele kinachoruhusu viongozi kujivua uanachama wa chama kimoja na kujiunga na chama wanachotaka bila kuathiri nafasi zao.

Wakifanya hivyo watakuwa wamesaidia siyo tu kupoteza muda wa watu kushiriki uzalishaji na kuliongezea taifa mapato, lakini pia watakuwa wameokoa fedha ambazo zingetumika kuratibu chaguzi hizi za ajabu ajabu
Hawawezi kufanya hivyo, kule tunakopeleka bakuli ili kufidia budget wanaheshimu demokrasia ambayo wanaamini inaletwa na vyama vingi. Tutabanwa humu humu, kufa hatutakufa lakini chamoto tutakiona.
 
Hao naona wanatafuta namna ya kujijenga kisiasa, mawazo kinzani ya namna ya kuendesha mambo lazima yawepo tu hata kama kila mtu atahamia ccm.
 
Back
Top Bottom