Julius Mtatiro amenifanya niandike...

Julius Mtatiro amenifanya niandike...

NKWENYE

Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
59
Reaction score
184
Poleni sana wanajukwaa mliotega masikio kuhusu mambo mbali mbali. Pole zangu kubwa ziende kwa waliopotelewa na wapendwa wao hasa wale waliopotea wakihusishwa na mambo ya kisiasa....

Poleni sana wanahabari kwa matukio yanayochipua taratibu dhidi yenu ,kwa kuwa mimi siyo mwanahabari sina cha kuwafundisha kwa kuwa sijui mnafundishwa mbinu gani mkiwa kwenye masomo yenu, ila poleni sana ndugu zangu...

Poleni sana waumini wa siasa tena siasa ya tanzania. Nami naomba nijipe pole kwa sababu pia ni muumini....

Baada ya pole hizo nirudi kwenye mada yangu ya msingi...

Kwanza niwakumbushe wanabodi wenzangu kuwa toka matokeo ya urais,wabunge na madiwani utangazwe mwaka 2015 hatujawahi kumaliza mwaka bila kuingia kwenye uchaguzi aidha wa wabunge au madiwani... Maana yake toka mwaka huo tuko kwenye uchaguzi mpaka leo.. Uchaguzi haujaisha..Na tutaendelea hivi mpaka 2020 na ikumbukwe rais alitoa agizo la watu kutofanya siasa zisizo za msingi ili nchi "Iconcentrate " na ujenzi wa nchi.. Lakini mpaka leo hatujamaliza uchaguzi.. Sababu mnazijua

Wanasiasa wamekuwa wakihama sana hasa kutoka upinzani kwenda kumuunga mkono mheshimiwa rais, lakini wote waliokuwa wanahama hawakuwahi kunitesa sana kwa sababu wengi wao nilikuwa nawaelewa vizuri..

Leo kuna kijana mmoja ambae sitaki nimuite mwanasiasa kwa sababu ambazo nilikuwa nampa... Huyu ni julius mtatiro...

Huyu ni moja ya vijana wachache niliokuwa ninahisi hawana maisha ya "Utikiti maji " anaejitambua sana,, ambae amejijenga katika mtazamo wa self reliance hivyo kutoishi maisha ya kinafiki. Lakini leo nimemsikiliza na kupata hofu kidogo... Wakati napata hofu nikajiuliza maswali machache

1: Nini maana ya upinzani wa kisiasa?

2: Upinzani ulianza kipindi kipi?

3: Je, kipindi upinzani unaanza ulikuwa unahitajika sana kuliko kipindi hiki?

4: Ikitokea CCM ikafuta "Political leaders" wote wa upinzani hasa wabunge nini kitatokea?

5: Je, upinzani unazuia rais na watendaji wake kujenga nchi??

6: Kuna nchi ngapi ulimwenguni hazina vyama vya upinzani?....

Wanabodi nisema tu wazi mimi siyo mpinzani ila ni muumini wa mawazo pevu... Kuna muda nchi yetu inahitaji mawazo chokonozi ili isonge mbele, na mara nyingi mawazo hayo huwa hayatoki kwa mabosi.. Hutoka kwa walala hoi. Hawa ndiyo wajenga nchi.. Wanajua matamu na machungu zaidi...

Baada ya kuwasikiliza wote wanaohama na leo mtatiro nimegundua machache

1: Mitaala yetu ya elimu ni mibovu sana (watanielewa wachache).

2: Mabadiliko ya nchi kama tanzania hayatafanywa na wanasiasa bali wananchi tu.

3: Hata CCM ibaki yenyewe upinzani haufi.... (nitaeleza)

4: CCM hakuna inachokifanya cha kuwaweka madarakani milele ndiyo maana wanaogopa kuruhusu mashindano ya kisiasa...

Mwisho niwakumbushe point yangu namba tatu above... Upinzani siyo mbowe, siyo lissu, siyo zitto, siyo wapinzani... Upinzani ni tafsiri ya mioyo ya watu.... Anaweza kutoka mbowe, lissu ila mioyo ya watu ikaendelea kujenga upinzani mkali zaidi..... Natamani upinzani wa majukwaa uishe ili tuanze moja.. Tutakuwa na mapinduzi na siyo upinzani. Msifadhaike sana mnaoamini mawazo mbadala.

Wasaaaaaaaaalam...

Mwananchi wa kawaida
 
Note
Screenshot_2018-08-11-16-40-44.jpg
 
Maana ya Democracy ni ikiwemo mtu mmoja kuchagua chama cha siasa akitakacho. Au kwako Democrasia ni Mzee Lowasa na Mzee Sumaye pamoja na Nyalandu kubama CCM kwenda CDM tu? Kuweni na kumbukumbu. Nyarandu alihama mlishangilia sana nyie hao hao. Hamkuona cha gharama wala nini. Democrasia iko hivyo so vumilieni tu
 
Mkuu NKWENYE mmi nimekuelewa vyema kabisa naomba niongezee jambo moja muhimu sana hapa, Taifa bado lipo katika kipindi cha mpito kuelekea mabadiliko ya kweli na hii ndio time frame yetu, wengine wanapigana kwa miaka 100 na wengine miaka michache zaidi lakini yenye maumivu makubwa mpaka kuja kuleta Taifa lenye kuheshimu mawazo ya watu wake, uhuru wa watu wake, na utu. Kama taifa bado tunafinyangwa na kuingizwa kwenye acid kali, moto wenye joto kali sana na hatimae kupata golden state ambayo tunaihitaji sana. Bado tunaendelea na process na tutaona mengi mpaka pale wananchi wenyewe (bila ya kutumia wana siasa) watakapo amka.
 
kiza kinene ni dalili ya mapambazuko, hakika MUNGU yuko pamoja na sisi.
 
Sasa hivi maumivu ndio yameanza,chadema leo imepoteza Halmashauri ya monduli,bado wazito wengine wanakuja
 
Ukitusaliti tunakublock tu tusione hata nyayo zako
 
Last summary yak,umeanza vzur bt ukamalzia na mawaz ya bavicha.unaelekea kupata tabu,sana ww!
 
Back
Top Bottom