Julius Mtatiro amenifanya niandike...

Julius Mtatiro amenifanya niandike...

Nililia, nikalia nikalia nikalia sana. Haikutosha. Naililia nchi yangu.

Mungu wangu ni wewe ndiye umeamua mambo haya kuwa hivi Tanzania?
 
Hawa wangine wanaoenda CCM nahisi wanaenda kimkakati zaidi.!
Time will tell
 
Magufuli na serikali yake kama wanataka kuua upinzani wanaweza kufanya jambo bila kuliingizia taifa gharama za uchaguzi.

Wapeleke hoja bungeni ili kufanya maboresho kwenye katiba na sheria ya vyama vya siasa.

Kwamba wanaweza kuweka kipengele kinachoruhusu viongozi kujivua uanachama wa chama kimoja na kujiunga na chama wanachotaka bila kuathiri nafasi zao.

Wakifanya hivyo watakuwa wamesaidia siyo tu kupoteza muda wa watu kushiriki uzalishaji na kuliongezea taifa mapato, lakini pia watakuwa wameokoa fedha ambazo zingetumika kuratibu chaguzi hizi za ajabu ajabu
 
Siasa za kibongo ni pasua kichwa!

Kikubwa kuangalia maendeleo yako na familia yako tu!

Wewe umenena, watu wanafikiri Upinzani ndo utawaletea maendeleo yao. Tumeona nchi zina upinzani wa hali ya juu, na demokrasia iliyokomaa, lakini watu ni masikini kupindukia. Ukitaka kujua hilo, nenda huko wanakokuita bondeni, kwa tata Mandela, Soweto. Fanyeni kazi, upinzani hauna tija kwa maendeleo binafsi
 
Kadri nionavyo,CCM kwa upande mwingine wanatakiwa wawaangalie kwa makini hawa wanaohamia kwa sasa. Sidhan kama sababu wanazotaja kwa watu makini zina mashiko. Ila sababu ambayo ina mashiko ni ile UHURU WA KIKATIBA kuhama chama A kwenda B ambapo Lowasa,Nyalandu et al,huku Mwita, Mtuli et al walihama kwenda upande tofauti
 
Boss NKWENYE Umeandika vizuri sana, Kuna ka usemi nakapenda sana, Bila Upinzani wa kweli na madhubuti, hakuna Maendeleo. So jibu rahisi tu hapo, hao si Wapinzani wa Kweli na Madhubuti. Hata kama umefanya makubwa katika Nchi hii. Unatakiwa usimamie kitu mpaka tone la mwisho, hapo ndio utahesabika Shujaa. Sasa hivi kila MwanaSiasa anapigania tonge lake.



Poleni sana wanajukwaa mliotega masikio kuhusu mambo mbali mbali. Pole zangu kubwa ziende kwa waliopotelewa na wapendwa wao hasa wale waliopotea wakihusishwa na mambo ya kisiasa....

Poleni sana wanahabari kwa matukio yanayochipua taratibu dhidi yenu ,kwa kuwa mimi siyo mwanahabari sina cha kuwafundisha kwa kuwa sijui mnafundishwa mbinu gani mkiwa kwenye masomo yenu, ila poleni sana ndugu zangu...

Poleni sana waumini wa siasa tena siasa ya tanzania. Nami naomba nijipe pole kwa sababu pia ni muumini....

Baada ya pole hizo nirudi kwenye mada yangu ya msingi...

Kwanza niwakumbushe wanabodi wenzangu kuwa toka matokeo ya urais,wabunge na madiwani utangazwe mwaka 2015 hatujawahi kumaliza mwaka bila kuingia kwenye uchaguzi aidha wa wabunge au madiwani... Maana yake toka mwaka huo tuko kwenye uchaguzi mpaka leo.. Uchaguzi haujaisha..Na tutaendelea hivi mpaka 2020 na ikumbukwe rais alitoa agizo la watu kutofanya siasa zisizo za msingi ili nchi "Iconcentrate " na ujenzi wa nchi.. Lakini mpaka leo hatujamaliza uchaguzi.. Sababu mnazijua

Wanasiasa wamekuwa wakihama sana hasa kutoka upinzani kwenda kumuunga mkono mheshimiwa rais, lakini wote waliokuwa wanahama hawakuwahi kunitesa sana kwa sababu wengi wao nilikuwa nawaelewa vizuri..

Leo kuna kijana mmoja ambae sitaki nimuite mwanasiasa kwa sababu ambazo nilikuwa nampa... Huyu ni julius mtatiro...

Huyu ni moja ya vijana wachache niliokuwa ninahisi hawana maisha ya "Utikiti maji " anaejitambua sana,, ambae amejijenga katika mtazamo wa self reliance hivyo kutoishi maisha ya kinafiki. Lakini leo nimemsikiliza na kupata hofu kidogo... Wakati napata hofu nikajiuliza maswali machache

1: Nini maana ya upinzani wa kisiasa?

2: Upinzani ulianza kipindi kipi?

3: Je, kipindi upinzani unaanza ulikuwa unahitajika sana kuliko kipindi hiki?

4: Ikitokea CCM ikafuta "Political leaders" wote wa upinzani hasa wabunge nini kitatokea?

5: Je, upinzani unazuia rais na watendaji wake kujenga nchi??

6: Kuna nchi ngapi ulimwenguni hazina vyama vya upinzani?....

Wanabodi nisema tu wazi mimi siyo mpinzani ila ni muumini wa mawazo pevu... Kuna muda nchi yetu inahitaji mawazo chokonozi ili isonge mbele, na mara nyingi mawazo hayo huwa hayatoki kwa mabosi.. Hutoka kwa walala hoi. Hawa ndiyo wajenga nchi.. Wanajua matamu na machungu zaidi...

Baada ya kuwasikiliza wote wanaohama na leo mtatiro nimegundua machache

1: Mitaala yetu ya elimu ni mibovu sana (watanielewa wachache).

2: Mabadiliko ya nchi kama tanzania hayatafanywa na wanasiasa bali wananchi tu.

3: Hata CCM ibaki yenyewe upinzani haufi.... (nitaeleza)

4: CCM hakuna inachokifanya cha kuwaweka madarakani milele ndiyo maana wanaogopa kuruhusu mashindano ya kisiasa...

Mwisho niwakumbushe point yangu namba tatu above... Upinzani siyo mbowe, siyo lissu, siyo zitto, siyo wapinzani... Upinzani ni tafsiri ya mioyo ya watu.... Anaweza kutoka mbowe, lissu ila mioyo ya watu ikaendelea kujenga upinzani mkali zaidi..... Natamani upinzani wa majukwaa uishe ili tuanze moja.. Tutakuwa na mapinduzi na siyo upinzani. Msifadhaike sana mnaoamini mawazo mbadala.

Wasaaaaaaaaalam...

Mwananchi wa kawaida
 
Moja ya sababu ya Julius Mtatiro mmoja wa vijana waliokuwa wakihoji kutaka maendeleo ya haraka ya Tanzania kuhama upinzani leo ni sababu inayofikirisha sana.

Ni sababu inayosadifu mwelekeo wa siasa za Tanzania katika zama hizi mpya.

Julius ameeleza sababu ya kuondoka alikokuwa ili "akapate zaidi fursa ya kufanya siasa za maendeleo."

Hakika niemwelewa, Siasa katika asili yake si mchezo mchafu kama baadhi wanavyotaka kusema...Nadharia sahihi ya siasa ni maendeleo.

Hakuna mwanasiasa awe yeyote wa kweli anayeweza kusema anafanya siasa kwa ajili ya mzaha. Siasa msingi wake ni kutafuta fursa ya kufanya au kuleta maendeleo.

Ndio maana siku Dr. Slaa alipoona CCM wamembania alitafuta fursa Chadema ya "kuleta maendeleo."

Siku Lowassa alipoona CCM hana nafasi akaenda Chadema kutafuta "fursa ya kuleta maendeleo."

Ipo mifano mingi lakini nimalizie pia kuwa hata Zitto Kabwe alipoona Chadema hakuna fursa alihamia au kuanzisha ACT ili kupata fursa ya "kuleta maendeleo."

Julius Mtatiro namfahamu bayana kuwa anaamini katika Tanzania yenye neema tele.

Tanzania yenye ukuaji mzuri wa uchumi, Tanzania yenye uongozi unaofanya uamuzi kwa maslahi ya nchi na watu wake.

Namfahamu Julius kuwa kijana anayeamini katika kupinga rushwa, ufisadi na anayeamini katika siasa za kuwaletea wananchi maendeleo.

Rais Magufuli anayafanya yote haya ya maendeleo: amekuza uchumi, ameongeza mapato ya Serikali, amepiga vita rushwa na ufisadi ipasavyo, anatekeleza miradi mbalimbali ya kuwaondoa Watanzania katika unyonge na anasimamia mageuzi ya kimaendeleo.

Sikupata fursa ya kumuuliza Julius anaamini siasa ni nini lakini kwa leo ametupa jibu kuwa yeye ni muumini wa siasa za maendeleo na siasa ambazo ndio msingi wa utawala wa Rais John Pombe Magufuli.

Kwa muktadha huu sitashangaa wanasiasa wote wanaoamini katika maendeleo wakiungana na JPM na kuwaacha wale wanaoamini katika siasa ni mchezo mchafu wabaki huko huko kwenye michezo michafu.

*Anaandika PoliticalJurist, formerly UDOM, MA student London*
 
Anatafuta cheo cha kisiasa hakuna lolote!ina maana wasio wanachama wa ccm hawamuungi mkono rais katika kuleta maendeleo?nchi kama marekani jee leo mtu anaweza akawa republican kesho akawa democratic?halafu na nyie mlie kipigania chama miaka nenda rudi hamna uwezo wa kuteuliwa???mpaka aliyetoka upinzani anapata mbeleko ya chuma???mjitafakari wana ccm asili
 
Lengo la kuua upinzani ni kitu na kwann mnatumia polisi kama mnaamini kweli kwenye siasa za maendeleo l. Stupidity
 
Back
Top Bottom