Juliana Shonza: Kigezo pekee cha kutoa mikopo kiwe ni ufaulu

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Shonza amedai wale wanaostahili kupata mikopo hawapati na wale wasiostahili mara nyingi huwa ndio wanaopata, amedai pia bodi haijajitambua kuwa ule mkopo wanaotoa ni mkopo au hisani ndio maana vigezo vyao huwa havieleweki na wanaopewa mkopo hawajajitambua kuwa wanakopeshwa au wanapewa hisani.

Ameongeza kuwa utaratibu wa kuweka majina kwenye gazeti haisaidii bali wanatakiwa kuja na mkakati ambao utambana yule aliyepewa mkopo na serikali ili warudishe kwa wakati na aweke kigezo pekee cha ufaulu ndio kiwe cha kutoa mikopo sio kama ilivyo sasa hivi mwanafunzi aliyepata division 1 hapati mkopo na aliyepata division 3 anapata.

mikopo ni kwa ajili ya watoto wa masikini na wasiojiweza kiuchumi...mtoto kama wa lowasa utampa mkopo wa nini hata kama ana division 1 wakati baba yake ni tajiri kupindukia?

matajiri ndiyo likely kukopeshwa hata kwenye mabenki maana kuna uhakika wakurudisha anyway tuliache hilo.

Mikopo ya elimu naona iwe haki ya kila aliyefaulu vizuri na hiyo inaweza kuwa motisha wa kuwafanya wanafunzi wasome sana. Pili ni kigezo kisichokuwa na ukiritimba wa kumtambua nani mototo wa tajiri au masikini. Elimu / uelewa kichwani mwako ndiyo iwe sifa. One of few good contribution from Hon. Shonza.
 
vigezo viwe ni watoto wa masikin tu au wasiokuwa na uwezo kwasababu inawezekana mtoto wa tajir apeww mkopo kwasababu tu ya division one na wale wasiojiweza wakose mkopo kwasababu ya division three aliyoipata kwa shida shule za kata
 
kweli, japokuwa kuna changamoto za kugundua masikini kweli ni yupi
 
Kwa hiyo masikini apewe tu mkopo hata kama mbulula? Watumie vigezo gani vya kupima huyu baba tajiri anaweza na huyu sio kama baba zao sio public figure. Huu utaratibu unaharibiwa na wanasiasa wenyewe ili kupata wanachotaka hata kama kiwe na madhara mbeleni. Zamani watu walishajizoelea only public universities ndio walipata mikopo na private unajisomesha mwenyewe.
 
Kwa mara ya kwanza huyu binti ametoa mchango kwa fikra iliyotulia. Naunga mkono hoja yake kwa mara ya kwanza
 
Tatizo la kuwa na wabunge wasioweza kufikiri sawa sawa, mbunge huwezi kuja na akili ndogo namna hiyo. Akili kubwa ni kutengengeza investment vehicle, mikopo inayorejeshwa iuzwe at discount watu wawekeze wawe wanapata periodic return based on risk return profile, fedha iliyopatikana wakopeshwe wanafunzi wengi zaid.
Kwa kufanya hiv Utakuwa umetanua wigo wa mikopo, kodi kwa serikali na kukuza soko la fedha, ndo utaratibu unatumika America na ulaya. Haya ni mawazo yangu ambayo yatabaki kuwa property ya JF, ukikopi unatakiwa ulipie.
 
Pumba tupu mtu kasoma feza na mi st kayumba apewe mkopo yeye mi ninyimwe kisa ufaulu wakati wanaiba mitihani
Pointless kabisa
 
Mkopo anapewa mtu aliekidhi vigezo vya bodi ya mkopo,kama haujakidhi vigezo mkopo haupati atakama una Div 1 .
 
Kama ni ivo shule zile za private sizihusike na mikopo mana wao ni spoon feeder mpaka kwenye papers kigezo cha ufaulu kiwe kwa shule za kata na kundi lingine la kuangaliwa ni yatima
 
matajiri ndiyo likely kukopeshwa hata kwenye mabenki maana kuna uhakika wakurudisha anyway tuliache hilo.

Mikopo ya elimu naona iwe haki ya kila aliyefaulu vizuri na hiyo inaweza kuwa motisha wa kuwafanya wanafunzi wasome sana. Pili ni kigezo kisichokuwa na ukiritimba wa kumtambua nani mototo wa tajiri au masikini. Elimu / uelewa kichwani mwako ndiyo iwe sifa. One of few good contribution from Hon. Shonza.
Nakubaliana Na Wewe lakini Hivi Ni Kweli Mtu Anayemiliki Billioni 70 ukamkopeshe millioni 2,400,00/= za tuition fee?
Mkuu Maana ya "KUKOPA" ni Kuwa Umekosa "UWEZO WA KUMILIKI"! sasa Ni Ajabu Kubwa Kuwa Mtoto Wa Rostam Aziz eti anafaiwa millioni 10 alizokopesha na Serikali!!
Wacha sisi tusiojiweza Tudaiwe Mkuu...
 
Pumba tupu mtu kasoma feza na mi st kayumba apewe mkopo yeye mi ninyimwe kisa ufaulu wakati wanaiba mitihani
Pointless kabisa
Na Yule Aliyesoma KAIZIREGE mtihani unasolviwa Darasani Kama Past Paper kabla ya hata Ratiba Ya Mtihani Kutoka eti apewe Mkopo Kisa Ana Div 1, Aachwe Yule Wa Kilwa kisa Hana div 1, ridiculous.....
 
Nakubaliana Na Wewe lakini Hivi Ni Kweli Mtu Anayemiliki Billioni 70 ukamkopeshe millioni 2,400,00/= za tuition fee?
Mkuu Maana ya "KUKOPA" ni Kuwa Umekosa "UWEZO WA KUMILIKI"! sasa Ni Ajabu Kubwa Kuwa Mtoto Wa Rostam Aziz eti anafaiwa millioni 10 alizokopesha na Serikali!!
Wacha sisi tusiojiweza Tudaiwe Mkuu...
Ni Mtoto wa Rostam below the age of 18, zaidi ya hapo ni business ya bodi ya mikopo na yeye
 
Xaxa kama umexoma primary ukalpa mil4 kwa mwaka sec mil 5 a level mil 6 kwa mwaka mmoja alaf upewe mkopo mil 2 na lak 5 itamsaidia nn hyo but kuna ambao hapo walpo bado wanadaiwa ada ya o level
 
Back
Top Bottom