Nimeshangazwa na Matokeo ya Kidato cha Nne 2021

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,661
Wasalamu Wakuu

Leo Baraza la Mitihani Tanzania Bara, Limetangaza matokeo ya Kidato cha Nne Na Kuonesha Ufaulu ukiongezela kwa Asilimia Chini ya 2%. Well And Good.

Lakini Baada ya Kufuatilia Matokeo Ya Shule Nyingi Nimeona Division 1 zikiwa Nyingi sana na Division 4 zikipungua Sanaa. Hii ikanipa Maswali na Kujiuliza Kuhusu Ubora wa Mitihani Wanayotungiwa Vijana wetu na Ubora wa Elimu. Nakubaliana na wanaosema kuwa Ubora wa Elimu haupimwi kwa Ufaulu lakini mwaka 2021 nimeona ndio Mwaka ambao Division 1 zimekuwa Nyingi sanaa kuliko miaka Yote na Wasichana Wamefaulu sanaa kuliko Miaka Yote.

Hii imenipa Maswali na Kuhisi Kuwa Huenda Siasa Imeingia Kwenye Elimu yetu, Yaani Katika Kuunga Juhudi za Rais Mwanamke na Ufaulu umeenda Sana kwa Wanawake kuonesha Juhudi ambazo Serikalo inafanya kuwainua wanawake. Hii nimewaza kwa sauti.

Naweza kuwa sina Points nzuri za Ku Address hili lakini Kiukweli kuja Harufu ambayo sio Nzuri kwenye Elimu yetu.

Najiuliza hizi Division 1 je ni sawa na zile za miaka ya 2012 kuja Chini? Zile za miaka ya 2000-2011? Ni sawa na hizi? Je, waalimu mtusaidie Mitihani ni sawa? Au mitaala kwa Ujumla Imebadilika?

Hii inanifanya kuwaza Mbali, Huenda hawa Vijana Wetu wakaja kukumbana na Kitu Kizito katika Matokeo yao ya kidato cha sita ambacho wengi Wanatarajia Kufaulu vizuri kwenda Chuo na Kupata Mkopo wa Serikali, kwasababu Hapo serikali Itahitajika kutenga Budget Kubwa Huenda Hawa Vijana wetu walio Pitishwa Kiholela Wakashindwa Kwa Wingi kwenda Chuo kwa Kigezo cha Serikali kuogopa Kutoa Mikopo ya Elimu Ya Elimu Ya Juu kwa Wanafunzi Hawa, na Kuongeza Late ya Unemployment mtaani na Kitakacho tokea ni Hawa Kuamua Kwenda Diploma kuendelea kupoteza muda wa Kuajiriwa na Kuongeza ugumu wa Maisha.

Tuwajibu kama wadau wa Elimu Nchini Kuangalia Hili kwa Undani sanaaa? Nakumbuka Kipindi Chetu Mama Ndalichako Alifahamika na Wanafunzi wote kwasababu Ya Mitihani Yake, Lakini Mrithi wake wa sahizi sijui hata kama anafahamika kama Mama Ndalichako, katika Kusimamia Ubora Wa Mitihani.

Mfano Mkubwa Ni Mdogo wangu Ambaye Amefaulu kwa Division 1 ya 7 huku nikijua Fika Kichwa chake ni Kigumu, na Hajawahi Kuwa Kwenye 20 bora Darasani Kwao. Inanipa Wasiwasi Kwa Form 6

Wadau Tuangalie sana hili
 
Hii inamaana Kuna Mwaka Ufaulu utakuwa kwa Asilimia 100% kama Kila mwaka ufaulu unaongezeka kwa zaidi ya Asilimia 1.5% ni sasa tupo asilimia 88% ina maana baada ya miaka 5-8 ufaulu utakuwa asilimia 100%
Nchi ngumu Sana hii, ndo maana tuna wimbi kubwa la wasomi useless nchi hii.

Yote hii Ni sababu ya mfumo corrupt wa elimu
 
Sababu kubwa ya wingi wa hizi division 1 ni kutokuwa na zile penalt za hesabu!

Ufaulu wa hesabu kwa mwaka huu ni wa kiwango cha chini sana kuliko miaka yote na kama penalt zingekuwepo basi division 1 huenda mwaka huu zingekuwa chache kupita miaka mingine!

Wapo wanafunzi wengi sana wana division 1 lakini wana F za hesabu.
 
Matokeo ya mwaka huu yako kisiasa zaidi, sio ya kuyachukulia serious Sana.

Kuna mchezo mchafu Sana umefanyika uko wanakosahihisha na kupanga matokeo

Kwa Hili mkuu nakubaliana na Wewe, Huenda Kuna Jitihada zimefanyika ikizingatiwa Mkopo Wa Corona Tulipata kabla ya Mitihani ya Kidato cha Nne. Imewachukua mwezi 1 kusahihisha Mitihani, Kukusanya Matokeo, na Kutangaza matokeo.

Ukifuatilia Utagundua kuwa Makokeo ya Sasa Yamewahi kuliko miaka Yote. Yamechukua Mwezi 1 tuuu kuwa Tayari.
 
Sababu kubwa ya wingi wa hizi division 1 ni kutokuwa na zile penalt za hesabu!
Ufaulu wa hesabu kwa mwaka huu ni wa kiwango cha chini sana kuliko miaka yote na kama penalt zingekuwepo basi division 1 huenda mwaka huu zingekuwa chache kupita miaka mingine!
Wapo wanafunzi wengi sana wana division 1 lakini wana F za hesabu…!!

Hivi lile suala la Penalt lilitolewa?
 
Nani ana kumbukumbu ya matokeo ya mwaka 2012....ilikuwa ni kizazaa...wanafunzi walifeli kupita kiasi...nchi nzima...cha kushangaza yaliporudiwa aliyekuwa na div2 anajikuta ana div.4,,,, na mweny div4...anajikuta ana Div.2 au 3,,, sasa sielewi ni mchezo gani ulifanyika hapo katikati....Mi pia ni muhanga wa miaka hiyo 2012
 
Ninachowapendea Necta huwa wanaenda na upepo unavyoenda, kuna nyakati Tanzania One alitoka Chattle, kwahyo lazzma uangalie upepo unaelekea wapi? Nani anapenda kibarua chake kiote nyasi?
Hahahaha
 
Nani ana kumbukumbu ya matokeo ya mwaka 2012....ilikuwa ni kizazaa...wanafunzi walifeli kupita kiasi...nchi nzima...cha kushangaza yaliporudiwa aliyekuwa na div2 anajikuta ana div.4,,,, na mweny div4...anajikuta ana Div.2 au 3,,, sasa sielewi ni mchezo gani ulifanyika hapo katikati....Mi pia ni muhanga wa miaka hiyo 2012
Daaah nakumbuka huu mwaka mabloo walifanyiwa mambo ya ajabu sana.
 
Hivi hamuelewi kuwa kwa sasa kidato cha nne ndiyo shule ya msingi?nina uhakika mtoto akifika kidato cha nne atakuwa anajua mambo ya msingi....siasa ipo
 
Back
Top Bottom