NIni maana ya kugawa mikopo ya wanafunzi kwa haki?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,301
12,600
Serikali imeamua kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa kutumia chombo kinachoitwa Bodi ya mkopo (Higher education students' loans board, (HESLB)) kwa malengo gani? Je, ni kuongeza idadi ya wanafunzi wanaomudu kupata elimu ya chuo kikuu? Je, ni kuongeza idadi ya watumishi nchini wenye elimu ya chuo kikuu? Je, ni kusomesha watoto vyuo vikuu?

Ili kujibu maswali yote haya kikamilifu serikali lazima iamue kama mikopo hii itolewe kwa haki, sawa au kwa usawa. Ili kutoa mikopo kwa haki, sawa na kwa usawa lazima variables zifuatazo zikokotolewa kwanza:
1. Haki ya kila mtoto kupata elimu hadi mwisho wa ukomo wake (bila kujali ni mtoto wa nani?)
2. Aina ya Chuo anachokwenda kusoma mtoto (serikali, shirika la kidini au private kabisa)
3. Ada ya chuo alichochaguliwa kusoma.
4. Aina ya familia anayotoka mtoto (married, single parents, cohabiting parents, divorced, orphans)
5. Uchumi wa familia, mlezi wa mtoto vs ukubwa wa familia ya wazazi/walezi?
6. Mahitaji maalum ya mwanafunzi (walking/hearing aids, special assistance/costs)
7. Aina ya kozi

Hivyo kama mikopo inatakiwa kutolewa kwa haki ili kila mtoto aweze kumudu gharama za kusoma vyuo vikuu basi ili haki ionekane ikitendeka kwa watoto lazima mikopo hiyo izingatie nani hawezi kusoma kwasababu ya kukosa ada. Je kama tukipitia orodha ya wanafunzi wote waliopewa mikopo hii ambayo haitoshi kwa wote hakuna watoto ambao wamepewa mikopo hii lakini walikuwa na njia nyingine ya kuendelea na masoma ya chuo bila ulazima wa kupata mikopo hii na kuwanyima wale wasiokuwa na njia nyingine? Hapa waziri angepaswa tu kupita vyuo vikuu vyote na aombe apewe mafile ya wanafunzi wote itapata taarifa za wototo wenye mikopo na wasiokuwa na mikopo, atagundua mikopo iligawanywaje, na pengine asingehitaji kuunda tume wala task force kuujua ukweli huo maana taarifa zote za watoto ziko kwenye mafaili yao vyuoni.

kama mikopo hii ilipaswa kugawanywa sawa basi tulingetarajia kuwa kila mtoto wa chuo kikuu angepatiwa kiasi sawa cha mkopo kama vile watoto wote kuke jeshini kuruta tulivyokuwa tukipewa posho (kichele) sawa bila kujali ni mtoto wa nani, yaani wangegana kisugura hata manyoya yake.

Kama lengo lingekuwa kutoa mikopo kwa usawa basi wangezingatia uhitaji, ukubwa wa ada kwenye chuo chake, hali ya familia na hali ya mwanafunzi mwenyewe. Hata mfuko ule wa serikali kwa jina maarufu la Samia scholarships ungetumbukizwa kwenye kundi hili ili kulivuta kwenda juu kule waliko wenzao wenye nafuu. samia scholarships ingesikika vizuri kama ingetolewa kwa wanafunzi kwenye kundi hili ambao wana ufaulu mkubwa kama vile division one single-digit au kigezo kingine kuliko ufadhili huu ulivyotolewa kwa sasa. Kundi hili la watoto wenye uhitaji ni lile kundi ambalo mtoto mmoja huyo alifaulu anaweza kusababisha ndoa kuvunjika, nyumba, mifugo yote na mashamba/viwanja kuuzwa, akina baba kuiba na akina mama kujiuza ili kupata ada ya mtoto mmoja tu, na watoto wengine kukosa chakula, matibabu na kila kitu kwaajili ya elimu ya ndugu yao.

Namuomba Prof. mkenda apite vyuoni yeye mwenye na timu aombe mafaili ya wanafunzi wenye mikopo na wasio na mikopo alinganishe na wale ambao wameshindwa kuripoti vyuoni kwa kusosa ada. Hii haihitaji kwenye kwenye mifumo ya bodi ya mikopo, watakudanganya bure tu waziri




la kuongeza idadi ya wanafunzi wanaokwenda kusoma
 
Hakika...
Waziri anaunda kamati ya kufanya nni sasa wakati waliopewa mikopo na taarifa zao ziko vyuoni? aende pale pale MUHAS, UDSM na vyuo 2 vya Private akaombe files za watoto wote wenye mikopo na wasio kuwa na mikopo afanye comparative study kati ya watoto waliopewa na waliokosa alinganishe na orodha ya watoto ambao hawakuripoti kabisa ingawa walichaguliwa na afyanye analysis kisha atoe ripoti kwa umma juu ya alichokiona, kisha achukue hatua badala ya kwenda kushitaki bungeni taarifa ambayo ni mbichi kabisa. Elimu yetu imeshuka sana.
 
Back
Top Bottom