Julia Nyerere: Vitu ambayo vimenisaidia kuishi Tanzania baada ya kuishi Marekani kwa miaka 21


Kwa mujibu wa Julia Nyerere, mjukuu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye amekuwa akiishi na kusoma nchini Marekani kwa miaka zaidi ya 20, yafuatayo ni mambo 13 yanayomsaidia kuweza kuishi Tanzania ambako amekuta mambo ni tofauti na alivyozoea huko ughaibuni.

Julia Nyerere:

1. Nimejifunza kubargain. Mtu akikwambia bei Marekani anakwambia bei halisi, TZ watu ambao wanatoa services wamezoea kwamba mtu atataka upunguze so anaanza juu automatically, the trick ni kudivide by 3 alafu unaanza kubargain ili mkutane katikati.

2. Nimepunguza kutoka na kufatana na watu ambao wanatoka kila siku. Sio kila mtu anatumia hela zake anapotoka (machawa) na kuna wengine wanatoka na hawanunui chochote. Ukijaribu kushindana na watu ndio utajuta.

3. Sio kila mtu anaetaka kuhang na wewe ni rafiki yako au yupo genuine, nimejifunza kutofautisha na imenisaidia kua na genuine circle.

4. Invest invest invest, fursa zipo kwenye kila sector. Ushindwe wewe tu!

5. Jiwekee mazingira mazuri nyumbani kwako ili usitamani kutoka mara kwa mara. Kama unapenda kuangalia movies, jiunge na netflix.

6. Jifunze kuomba msaada na ushauri kwa wazoefu, huwezi kujua kila kitu.

7. Usiamini kila kitu unachoambiwa. Hapa ndio wanadiaspora wengi wanapokata tamaa, wanaassume kila mtu atakua mkweli so wanatapeliwa kiurahisi. Hii inaapply kwenye biashara na mahusiano.

8. Subira ni muhimu sana, itachukua muda kuadjust, usifikiri kwamba utazoea kiurahisi.

9. Ukitaka kutumia hela, usiwaze kwa currency ya ulipotoka. Waza kwa shillings, itakusaidia kutumia hela kwa uangalifu zaidi.

10. Usifanye kitu chochote kwa shortcut, mambo yako yote ya nyooke, hata kama mtu akijaribu kukushawishi kwamba ni sawa usikubali. Haijalishi utaspend kiasi gani zaidi kufanya vitu the proper way, cheap is expensive!

11. Enjoy and usijinyime, pale unapoweza jitreat na enjoy kua nyumbani. Kuna sehemu nyingi za kuona na kutembelea nyumbani, pafaidi mpaka wanadiaspora wengine watamani kurudi nyumbani.

12. Mtu asikutishe kwamba hutaweza kusurvive. Bora nyumbani mara ishirini kuliko ugenini. Wapo watu kibao ambao sio watanzania wamehamia huku na wanaishi vizuri tu na wanafaidi mpaka mimi nawaonea wivu kwamba nimechelewa kurudi.

13. Sali sana na sali kila siku, Mungu atakuongoza na hawezi kukubali ufeli.
Huyu ni wew mwenyew Miss Julia au ume paste hapa..nataka twende sawa ..nna maswal kadhaa kwako...sio ya kifamilia.wala kimapenz.ni maswala ya hayo hayo uliyoongelea
 
Upele humwota asiye na kucha,
Kwa exposure na jina la babu yake angekuwa anaandika mambo muhimu ili kupata nafasi kubwa serikalini.
Anaacha kuwaza kuanzisha foundation eti anawaza kujiunga netflix.

Yote kwa yote ni mbaya, hata bure sichovyi
 
Upele humwota asiye na kucha,
Kwa exposure na jina la babu yake angekuwa anaandika mambo muhimu ili kupata nafasi kubwa serikalini.
Anaacha kuwaza kuanzisha foundation eti anawaza kujiunga netflix.

Yote kwa yote ni mbaya, hata bure sichovyi
Watu hawaangalij ubaya kaka.watu wanaangalia nyota.kwamba umepiga mjukuu wa.....wee vip baharia.unakwama wap..hiv unahis ukinyoa hyo pisi..connection utakosa kwel
 
inamaana mzee nyerere hakubahatika kuwa na angalau,mjukuu ama mtt, genius na mwenye karama Kama yake!? Haka mbona kanaonekana kaswahili Swahili sana.
Kwani nyerere hakuwa mswahili sana?Mi nafikiri kati ya watoto wote wa Nyerere basi Huyu somehow anae element za mwalimu sema tu ndo basi malezi yashamuharibu kwa kiasi fulani hasa ukizingatia shadow ya JKN ado inamfunika ili akichiwa na kupewa nafasi anaweza sana kumtafuta babu yake
 
Huyu ni mjukuu kwa mtoto yupi wa Nyerere?

Maana wajukuu wa Kambarage wengi wao wana vimo virefu si kama huyu
 
Back
Top Bottom