Julai 2017: Nyongeza za mishahara na kupandishwa vyeo - Kilio cha Watumishi wa Umma

Wabongo kweli tumelongwa sio utani kwani ukiona mshahara hautoshi acha kazi tafuta sehemu nyingine sio kutujazia saver zetu tu hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
607455133ce6a8007efd0c443dd4b7b1.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
badala mjiajiri mnategemea mishahara ya mawazo ya serikali na sasa hivi wanavyobana posho marupurupu na safari mtatembelea rim kudadeki

Mimi sina mpango wa kuacha kazi serikalini mpaka milele,wanaotembelea rim ni wale wanaojifanya wazalendo ila mwehu kama mimi huku ndio sehemu sahihi kwangu ukitumia akili mshahara wa serikali mtamu sana mpwa niamini mimi hawa wenzangu hata kuiba muda wanaogopa lazima walalamike,muajiri alipoanza kunichukulia poa na mimi nikamchukulia poa sijutii kuajiriwa.
 
Ndugu wapendwa mishahara imeanza kutolewa kwa awamu awamu kikubwa zaidi hakuna ongezeko lolote hata annual increment kitu ambacho kwa watumishi wengi hasa walimu limewasononesha sana ukizingatia aliyejuu ni mwenzao anayeyajua machungu ya kada hiii kiukweli hata mimi haijaniingia akilini wakati tunasema tunaboresha elimu sijui ni elimu ipi? maana huwezi kuzungumzia elimu bila kumgusa mwalimu na kitu ambacho nadhani hakiko sawa walimu wakuu wanalipwa 200000 kwa mwezi kama pesa ya madaraka sijui wanafundisha peke yao? na kuna waratibu elimu kata (afsa elimu kata) wanalipwa 250000 kwa kila mwezi hivi hili liko sawa?
 
Back
Top Bottom