Waraka kuhusu ujenzi wa “jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja” wahimiza ushirikiano na kunufaika kwa pamoja

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG41BU010994.jpg


Serikali ya China imetoa waraka kuhusu ujenzi wa “jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja” miaka 10 baada ya Rais Xi Jinping wa China kutoa pendekezo hilo ambalo limefuatiliwa na wachambuzi wengi wa mambo ya kiuchumi na kidiplomasia. Kutolewa kwa waraka huu, kunachukuliwa kuwa ni urasimishaji wa busara zilizoonekana kwenye pendekezo hilo katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.



Kwa wale wanaofuatilia mambo ya kidiplomasia ya China, maneno “kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja” si mageni. Hili ni wazo lililotolewa na Rais Xi Jinping wa China mwaka 2013, waraka huu unaotolewa miaka 10 baada ya pendekezo hilo kutolewa, kunatokana na uzoefu uliopatikana baada ya utekelezaji, uchambuzi na hata matokeo ya pendekezo hilo kuonekana kuwa ni jambo lenye manufaa kwa binadamu wote.



Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, dunia na binadamu wamekumbana na changamoto nyingi ambazo zote zimethibitisha kuwa, inapotokea changamoto binadamu wote tunakuwa hatarini, na tunaposhirikiana basi tunaweza kutatua changamoto hizo kwa urahisi.



Katika miaka kumi iliyopita changamoto mbalimbali zimetokea duniani, ikiwemo janga la COVID-19, madhara ya mabadiliko ya tabia nchi, ukame na hata mafuriko. Baadhi ya nchi zilijiona kuwa ni tajiri, zenye teknolojia, na usimamizi makini wa magonjwa ya mlipuko, lakini matokeo yake yakaonesha kuwa licha ya kuwa na nguvu hiyo haiwezi kukabiliana na janga la COVID-19 peke yake.



Nchi za magharibi kwa mfano, zilijaribu kuhodhi chanjo ya COVID-19 lakini baada ya kuona kuwa kama janga hilo likiendelea kuwepo katika sehemu nyingine duniani, nazo pia hazitakuwa salama. China kwa upande mwingi tangu wakati wa utafiti wa chanjo yake, ilitangaza wazi kuwa chanjo hiyo kwa ajili ya dunia nzima. Kwenye changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi, wakati China ikijitahidi kuzisaidia nchi zinazoendelea kuendeleza matumizi ya nishati mpya, nchi za magharibi ziliendelea na ubinafsi na kutotoa fedha na teknolojia, zaidi ya kuendelea kulaumu nchi nyingine.



Changamoto nyingine ambayo imezikumba moja kwa moja nchi za magharibi, ni madhara ya mabadiliko ya tabia nchi. Majanga ya moto wa misituni yameripotiwa katika nchi mbalimbali za magharibi, na kuonesha kuwa bila dunia kushirikiana kwenye changamoto hii, binadamu wote hatutakuwa salama.



China katika sera yake ya mambo ya nje imepiga hatua nyingi zaidi, na kuhusisha mambo mengi ambayo ni hatma ya pamoja ya binadamu, na kama mambo hayo yakiachwa basi binadamu watakiwa kwenye matatizo. Ndio maana waraka huo umesema juhudi za kujenga dunia iliyo wazi, jumuishi, safi na nzuri, ambayo watu wake wanafurahia amani ya kudumu, usalama kwa wote, ustawi wa pamoja, ndio itakayoweza kubadilisha hamu ya watu ya kuwa na maisha bora kuwa jambo halisi.



Tunatakiwa kukumbuka kuwa China siku zote imekuwa ikihimiza ushirikiano na nchi nyingine duniani, ni kusema kuwa maendeleo yake yanatakiwa kunufaisha nchi nyingine. Hii imethibitishwa katika mipango mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na nchi nyingine duniani, nchi za Afrika kwa mfano zimeweza kunufaika kupitia pendekezo la Ukanda mmoja, Njia moja (BRI) au Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na kuzipatia nchi za Afrika fursa za maendeleo.
 
Back
Top Bottom