Judge Mstaafu Augustino Ramadhan apewa Daraja la Uchungaji Anglican

Judge Mstaafu Augustino Ramadhan apewa Daraja la Uchungaji Anglican

Waanglikana wana Mapadre kama Katoliki, ispokuwa wa kwao wanaoa...

Hongera zake padre mpya, hata hawa wakatoriki wataoa tu miaka si mingi.

Kuna jamaa aliniambia kuwa Uingereza huwezi kuwa waziri mkuu kama wewe siyo mfuasi wa dhehebu hili, je ni kweli?
 
Ni kweli ameropoka

Hajaropoka ni ukweli.
Daraja la Upadre liko kanisa Katoliki tu, Wanaofutia , ni Wachungaji au Wainjilisti, Kwa hio huyo jaji mstaafu sio padri bali ni Mchungaji, Mwandishi wa habari kashindwA kutofautisha Watumishi wa Katoliki na Anglican.

Waanglikana wana Mapadre kama Katoliki, ispokuwa wa kwao wanaoa...
 
Ametii sauti ya Bwana na aliadhimisha siku ya kuzaliwA KWAKE. Alikata keki na kuambiwa awe mwaminifu hadi ....Bwana awe pamoja naye
 
Hongera sana Jaji Mkuu(mstaafu) AUGUSTINO RAMADHANI

Mungu ni Mwema
Kila iitwapo Leo.
:A S-heart-2:😛oa:violin::A S-rose::A S-rose:
 
Yaani amehukumu watu vifungo vya maisha na kunyongwa na sasa ni mchunga kondoo!
Sijui maandiko matatifu yanasemaje kuhusu hili!
 
Jaji Ramadhani awa mchungaji
Anglikana
>Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustino
Ramadhani alionekana akitoa mkate kwa waumini wa Kanisa la Anglikana
baada ya kupewa Daraja la Ukasisi
katika Kanisa la Anglikana lililopo
Mkunazini mjini Zanziabar jana.
source Mwananch.


JAJI MKUU MSTAAFU, AUGUSTINO RAMADHANI (ALIWAHI KUWA BRIGEDIA JENERALI WA JWTZ ) ATAWAZWA KUWA MCHUNGAJI WA KANISA LA ANGLIKANA HUKO ZNZ


date.png
8:19 PM




Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawazwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na kusema ameshangazwa na mashambulizi ya tindikali dhidi ya viongozi wa dini Visiwani humo.

Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.

Alisema Wakristo na Waislamu Zanzibar kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi kama ndugu bila ya kubaguana kwa sababu za itikadi ya dini licha ya Waislamu kuwa asilimia 95.

Hata hivyo, alikumbusha kuwa wakristo wana mchango katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ambapo idadi kubwa ya waumini wake walianzisha Chama cha African Association mwaka 1935, ambapo rais wake wa kwanza alikuwa hayati, Mzee Augustino Ramadhan na baadaye akafuata hayati Mzee Abeid Amani Karume.

"Vitendo vya watu kumwagiwa tindikali vinanishangaza, sababu halisi siifahamu, najiuliza haya yametokea wapi, siyo jambo jema wala siyo sifa ya Zanzibar tokea enzi na enzi," alisema.

Alisema wakati umefika na kuwataka viongozi kuwa mstari wa mbele kukemea matukio ya hujuma za tindikali na uhalifu mwingine ikiwemo mashambulizi ya kutumia silaha za moto na watu kupotezewa maisha.

Jaji Augustino amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na Tanzania, Brigedia Jenerali wa JWTZ pia amewahi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki, ambapo amesema kazi ya sheria hazitofautiani na kazi za kiroho kwa vile zote zinahitaji utende haki na kutimiza wajibu upasavyo.

Kwa upande wake Askofu Philip Baji wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John cha Dodoma, alisema huu ni wakati mwafaka kwa Serikali kuwalinda viongozi wa dini bila ya kujali tofauti ya madhehebu yao kutokana na kukithiri kwa vitendo vya hujuma.


source; Paparazi

 
Hajaropoka ni ukweli.
Daraja la Upadre liko kanisa Katoliki tu, Wanaofutia , ni Wachungaji au Wainjilisti, Kwa hio huyo jaji mstaafu sio padri bali ni Mchungaji, Mwandishi wa habari kashindwA kutofautisha Watumishi wa Katoliki na Anglican.

Mhhh.....!!!! Kama hujui uliza. Kuuliza si ujinga. By the way hongera sana Padre A. Ramadhan
 
Nampongeza. Na sina uhakika kama ana undugu wa damu na Askofu Mkuu mstaafu wa Anglikan Tanzania, Askofu John Ramadhan, ambaye nae kwasasa anaishi huko Zanzibar. Namtakia baraka za bwana ktk kazi yake hiyo ya kiimani.

Ni Mtu na kaka yake!
 
Kwani waanglican wana wapadre au wachungaji? Mimi nilidahani na naendelea kudhani kuwa padre ni kwa wakatoliki tu. Hebu mnifafanunulie hapa!!
 
Hajaropoka ni ukweli.
Daraja la Upadre liko kanisa Katoliki tu, Wanaofutia , ni Wachungaji au Wainjilisti, Kwa hio huyo jaji mstaafu sio padri bali ni Mchungaji, Mwandishi wa habari kashindwA kutofautisha Watumishi wa Katoliki na Anglican.

Unalijua kanisa la Anglikana au umekariri tu? Upadre hauko Catholic Church peke yake.
 
Hongera sana Padre Augustino Ramadhani,chunga vema kondoo wa mungu
 
Hongera sana Jaji mstaafu mtumikie Mungu kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote.

Mungu ni Mwema
Kila iitwapo Leo
.
 
Judge Mkuu mstaafu wa Tanzania Augustino Ramadhan jana amesimikwa na kupewa daraja takatifu la Upadre ktk Kanisa Kuu la Anglican Mkunazini-Zanzibar,na hivyo sasa atahudumu ktk shughuli za kiroho ktk Kanisa la Anglican. Akiongea baada ya hatua hiyo hiyo,Pd.Augustino Ramadhan amemshukuru Mungu ktk maisha yake,kwa kumpa nafasi ya kuwahudumia watu kiroho na kimwili,kwa kuwatumikia kama kiongozi ktk muhimili wa mahakama na kama kiongozi wa kanisa. Pia Pd.Ramadhani amewakumbusha waamini na jumuiya ya Zanzibar kudumisha umoja,amani na upendo miongoni mwao,bila kujali tofauti zao za kiimani na kisiasa,amesisitiza kuwa matuki yanayojitokeza ya kumwagiana tindikali Zanzibar si tu yanaichafua sifa ya visiwa hivyo,bali pia yanaua undugu wa mda mrefu kati ya waumini wa kikristo na kiislamu visiwani humo,kwani wamekuwa na umoja na ushirikiano wa karne na karne. Kabla ya kuwa Padre wa kanisa la Anglican,Pd.Ramadhani aliitumikia jamii kama Jaji Mkuu,Jaji wa Mahakama ya Rufaa na wa Mahakama ya Afrika Mashariki,pia ni Brigedia Jenerali mstaafu wa JWTZ. NB:Wanaojua taratibu za Kanisa la Anglican hii imekaaje??
Ukiona hali kama hii ni kwamba Mh. Augustino Ramadhani ni mtu mwema, mwenye kustahili kupata upadre namuombea kwa MUNGU azidi kutumikia jamii
 
mimi binafsi namchukulia Austustino Ramadhani kama kiongozi mahiri, mtenda haki na alivaa viatu vya ujaji mkuu vizuri. Alifanya wajibu wake mpaka nje ya mipaka ya kazi aliwasaidia wengi sana na alisimamia haki muda wote regardless kuhujumia wakati mwingine. Alifanikiwa kusaidia wanyonge wengi na wakapata haki. Kuna hata waliohukumiwa kunywangwa lakini alipojapitia hukumu zile aliona mapungufu na hila na aliamuru faili kuchunguzwa upya na kutoa hukumu ya haki. Jaji Ramadhani ni hatasahaulika kwa kazi yake nzuri na hii ni moja ya thawabu anazopewa kujitakatifuza zaidi. Mawazo Yangu!
 
Dah akina Khataan na F/foxy hawajapita hapa bado!

Hongera zake amefaidi duniani huenda akafaidi na heaven, wengine wana zali dah
 
Back
Top Bottom