Judge Mstaafu Augustino Ramadhan apewa Daraja la Uchungaji Anglican

Judge Mstaafu Augustino Ramadhan apewa Daraja la Uchungaji Anglican

Hongera zake padre mpya, hata hawa wakatoriki wataoa tu miaka si mingi.

Kuna jamaa aliniambia kuwa Uingereza huwezi kuwa waziri mkuu kama wewe siyo mfuasi wa dhehebu hili, je ni kweli?

Uko Sahihi.Church of England ni Anglican na hata Tonny Blair alikuwa Converted to Catholic baada ya Kustaafu u PM.
 
Hajaropoka ni ukweli.
Daraja la Upadre liko kanisa Katoliki tu, Wanaofutia , ni Wachungaji au Wainjilisti, Kwa hio huyo jaji mstaafu sio padri bali ni Mchungaji, Mwandishi wa habari kashindwA kutofautisha Watumishi wa Katoliki na Anglican.
Oooh! Uliza ueleweshwe.
 
Atubu kwanza manake yeye kama binadamu na hasa mkiristo hadi kufikia ujaji kuna hukum alizozitoa hasa kutoa uhai wa watu kwa kunyongwa kwa wahalifu waliopatikana na hatia za uhalifu wa kunyongwa kwa ushahidi wa kibinadam ambao wakati mwingi huwa wa kuongezwa chumvi kukomoana hivyo binadam kuhukumiwa kutolewa uhai kwa uamzi wa binadam mwingine kinyume na mafundisho ya biblia
 
Nilikutana naye supermarket moja masaki akiwa amevaa kola ya uchungaji nikadhani nimemfananisha. Mpaka leo nikawa najiuliza bila majibu kumbe mzee ameamua kuchapa injili sasa. Hongera sana Mzee ila usisahau kutubu maana ujaji siyo rahisi kumaliza bila kuonea mtu hasa katika siasa za Tanzania.
 
Kama zanzibar awe makini akajifunze kukwepa na risasi
 
JAJI MKUU MSTAAFU, AUGUSTINO RAMADHANI (ALIWAHI KUWA BRIGEDIA JENERALI WA JWTZ ) ATAWAZWA KUWA MCHUNGAJI WA KANISA LA ANGLIKANA HUKO ZNZ

Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawazwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na kusema ameshangazwa na mashambulizi ya tindikali dhidi ya viongozi wa dini Visiwani humo.

Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.

Alisema Wakristo na Waislamu Zanzibar kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi kama ndugu bila ya kubaguana kwa sababu za itikadi ya dini licha ya Waislamu kuwa asilimia 95.

Hata hivyo, alikumbusha kuwa wakristo wana mchango katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ambapo idadi kubwa ya waumini wake walianzisha Chama cha African Association mwaka 1935, ambapo rais wake wa kwanza alikuwa hayati, Mzee Augustino Ramadhan na baadaye akafuata hayati Mzee Abeid Amani Karume.

"Vitendo vya watu kumwagiwa tindikali vinanishangaza, sababu halisi siifahamu, najiuliza haya yametokea wapi, siyo jambo jema wala siyo sifa ya Zanzibar tokea enzi na enzi," alisema.

Alisema wakati umefika na kuwataka viongozi kuwa mstari wa mbele kukemea matukio ya hujuma za tindikali na uhalifu mwingine ikiwemo mashambulizi ya kutumia silaha za moto na watu kupotezewa maisha.

Jaji Augustino amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na Tanzania, Brigedia Jenerali wa JWTZ pia amewahi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki, ambapo amesema kazi ya sheria hazitofautiani na kazi za kiroho kwa vile zote zinahitaji utende haki na kutimiza wajibu upasavyo.

Kwa upande wake Askofu Philip Baji wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John cha Dodoma, alisema huu ni wakati mwafaka kwa Serikali kuwalinda viongozi wa dini bila ya kujali tofauti ya madhehebu yao kutokana na kukithiri kwa vitendo vya hujuma.

Source; Paparazi

Mimi nadhani ni mchungaji na si Padre maana cheo cha padre utumika kwa Kanisa Katoliki na si rahisi kukipata, unakisotea miaka na miaka.
Anglican Church tunao Walimu, mashemasi, Padre kisha Askofu na si mchungaji.. Mchungaji ni wa makanisa ya Lutheran na Pentekoste n.k Kwa ufupi Catholic na Anglican Church ni dugu moja. Angalia uendeshaji wa ibada zao zimefanana sana.
 
Familia yao naona ina upako wakiutumishi maana kaka yake aitwae john ramadhani amepata kuwa askofu mkuu wa anglikana tanzania miaka ya tisini alinipa kipaimara.
 
Usipotoshe watu wewe nae huelewi

Jaji baada ya kusikiliza kesi na kuridhika kuwa mtuhumiwa katenda kosa kulingana na ushahidi uliotolewa mbele yake na kutafasiri sheria zinasemaje anatoa hukum kuwa mtuhumiwa amepatikana na hatia au la na kama ndio apewe adhabu gani kifungo cha maisha au kunyongwa hadi kufa

hivyo rais au magereza wanatekeleza maamuzi ya jaji kwa hiyo jaji ndo muuaji
 
Mtu ameishatoa hukumu za kunyongwa watu leo hii anakuwa Padre.

Mkuu hukumu kama hizi na nyingi nyingine za kikatili kabisa zimetolewa sana na ANDIKO LAKE.

Kwa hiyo yeye alichokuwa anafanya ni kukamilisha unabii tu.
 
jaij.jpg

Jaji Mkuu Mstaafu, Jaji Augustino Ramadhani akitoa mkate kwa waumini wa Kanisa la Anglikana baada ya kupewa Daraja la Ukasisi katika Kanisa la Anglikana lililopo Mkunazini mjini Zanziabar jana. Picha na Sahim Shao

KWA UFUPI

  • Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.

Aliapishwa jana kuwa mchungaji wa Kanisa la Anglikana, Zanzibar.

Zanzibar. Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani ametawazwa kuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar na kusema ameshangazwa na mashambulizi ya tindikali dhidi ya viongozi wa dini Visiwani humo.

Akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kutawazwa ndani ya Kanisa la Anglikana la Minara Miwili Mjini Unguja, Jaji Ramadhan amesema vitendo vya hujuma vinavyofanywa dhidi ya viongozi wa dini na Serikali ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar.

Alisema Wakristo na Waislamu Zanzibar kwa miaka mingi wamekuwa wakiishi kama ndugu bila ya kubaguana kwa sababu za itikadi ya dini licha ya Waislamu kuwa asilimia 95.

Hata hivyo, alikumbusha kuwa wakristo wana mchango katika harakati za ukombozi wa Zanzibar, ambapo idadi kubwa ya waumini wake walianzisha Chama cha African Association mwaka 1935, ambapo rais wake wa kwanza alikuwa hayati, Mzee Augustino Ramadhan na baadaye akafuata hayati Mzee Abeid Amani Karume.

"Vitendo vya watu kumwagiwa tindikali vinanishangaza, sababu halisi siifahamu, najiuliza haya yametokea wapi, siyo jambo jema wala siyo sifa ya Zanzibar tokea enzi na enzi," alisema.

Alisema wakati umefika na kuwataka viongozi kuwa mstari wa mbele kukemea matukio ya hujuma za tindikali na uhalifu mwingine ikiwemo mashambulizi ya kutumia silaha za moto na watu kupotezewa maisha.

Jaji Augustino amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar na Tanzania, Brigedia Jenerali wa JWTZ pia amewahi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mahakama ya Afrika Mashariki, ambapo amesema kazi ya sheria hazitofautiani na kazi za kiroho kwa vile zote zinahitaji utende haki

na kutimiza wajibu upasavyo. Kwa upande wake Askofu Philip Baji wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu John cha Dodoma, alisema huu ni wakati mwafaka kwa Serikali kuwalinda viongozi wa dini bila ya kujali tofauti ya madhehebu yao kutokana na kukithiri kwa vitendo vya hujuma. Jaji Ramadhani awa mchungaji Anglikana - Kitaifa - mwananchi.co.tz

wanaoua viongozi wa dini no serikali yenyewe rehea tukio la bomu la kanisa huko Arusha..
 
Anglikana hawana mchungaji, bali padre,

Kasisi maana yake ni Padre.
 
Mtu ameishatoa hukumu za kunyongwa watu leo hii anakuwa Padre.

Kama mbakaji, mporaji, mkware asiye na mwiko, muuwaji bado kuna misukule wanaamini ni mtume, jaji ambaye alikuwa anatekeleza sheria ambayo imewekwa na mwajiri wake kwa nini ashindwe kupewa daraja la upadre ? Labda kama kuna anayeweza kumtuhumu kwa kupindisha sheria na kutoa hukumu isiyo ya haki kutokana na kupofushwa na Rushwa hakika atakuwa na hoja.
 
Wewe ni mtu usie hitaji heshima wala hukufunzaa na wazee wako namna ya kujadili na watu!
Wakati mi nawachambulia huo uchafu wenu wa hayo maandiko yalio chakachuliwa. Ndugu zangu weengi sana WaKIISLAMU Wamenitumia ujumbe wakinisihi nisiuonyeshe Uchafu wenu HADHARANI!
Na mimi najitahidi kadri ninavyoweza kujadili kistaarabu.

Lkn unakuta mitoto sijui mingine ya haramu?
Haiwezi kabisa kujadili kiistaraabu.!
Sasa na mimi nikianza kukuiga wewe sitaki nyodo za kulia lia.!
I am warning you!
Halafu huyo padri kama LAIKUWA MFUASI WA mungu WA AGANO JIPYA. Kwa nini ASIWASAMEHE TU HAO WAUWAJI!
AU na yeye aliisahau lile ANDIKO LINALOSEMA "USIHUKUMU USIJE KUHUMIWA""!!
Huyu anaonekana ALILIPINGA AGANO JIPYA MUDA MREFU SANA.

Alikuwa ni MUASI MKUBWA!

Na hakufaa KABISA KUWA PADRI!
 
Hivi mahakama ya kadhi chini ya sharia ya kukata watu mikono na kuamuru watu wapigwe mawe hadi kufa inaendeshwa na nani?
 
Back
Top Bottom