Judge Mstaafu Augustino Ramadhan apewa Daraja la Uchungaji Anglican

Judge Mstaafu Augustino Ramadhan apewa Daraja la Uchungaji Anglican

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,944
jaij.jpg


Judge Mkuu mstaafu wa Tanzania Augustino Ramadhan jana amesimikwa na kupewa daraja takatifu la Upadre ktk Kanisa Kuu la Anglican Mkunazini-Zanzibar,na hivyo sasa atahudumu ktk shughuli za kiroho ktk Kanisa la Anglican.

Akiongea baada ya hatua hiyo hiyo,Pd.Augustino Ramadhan amemshukuru Mungu ktk maisha yake,kwa kumpa nafasi ya kuwahudumia watu kiroho na kimwili,kwa kuwatumikia kama kiongozi ktk muhimili wa mahakama na kama kiongozi wa kanisa.

Pia Pd.Ramadhani amewakumbusha waamini na jumuiya ya Zanzibar kudumisha umoja,amani na upendo miongoni mwao,bila kujali tofauti zao za kiimani na kisiasa,amesisitiza kuwa matuki yanayojitokeza ya kumwagiana tindikali Zanzibar si tu yanaichafua sifa ya visiwa hivyo,bali pia yanaua undugu wa muda mrefu kati ya waumini wa kikristo na kiislamu visiwani humo,kwani wamekuwa na umoja na ushirikiano wa karne na karne.

Kabla ya kuwa Padre wa kanisa la Anglican,Pd.Ramadhani aliitumikia jamii kama Jaji Mkuu,Jaji wa Mahakama ya Rufaa na wa Mahakama ya Afrika Mashariki,pia ni Brigedia Jenerali mstaafu wa JWTZ.

NB: Wanaojua taratibu za Kanisa la Anglican hii imekaaje?
 
I head before nikajua sio kumbe imekuwa, bac hongera zake ni mtumishi wa mungu mzuri sanaaaa
 
Nampongeza. Na sina uhakika kama ana undugu wa damu na Askofu Mkuu mstaafu wa Anglikan Tanzania, Askofu John Ramadhan, ambaye nae kwasasa anaishi huko Zanzibar. Namtakia baraka za bwana ktk kazi yake hiyo ya kiimani.
 
Mungu akuzidishie baraka Padre Ramadhani, umetumia karama zako vema, Mungu awe nawe daima
 
Hebu anayefahamu taratibu za kupata viongozi wa Kanisa la Anglikana atudadavulie hapa.
 
Mtaalamu wa kupiga kinanda,enenda uongoze vema wanakondoo kama ulivyokua Judiciary..

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nampongeza. Na sina uhakika kama ana undugu wa damu na Askofu Mkuu mstaafu wa Anglikan Tanzania, Askofu John Ramadhan, ambaye nae kwasasa anaishi huko Zanzibar. Namtakia baraka za bwana ktk kazi yake hiyo ya kiimani.


Hao ni ndugu wa damu, alielezea yeye mwenyewe kwenye makala yake kwnye moja ya magazeti. pia alisema babake alikuwa ni miongoni mwa wasomi wachache wa mwanzo hapa nchini km kumbu2 zangu ziko swsw
 
Mungu amsaidie katika taranta hii mpya. Namfahamu yeye kama muumini mzuri wa kanisa lake na ametumika sana kuhubiri injili kupitia kwaya ya kanisa la st.Alban akapagawisha kinanda.

Nimefurahishwa na maamuzi yake na kanisa kwa ujumla kwani anawapa ujumbe wastaafu kuwa ukistaafu mtumikie mungu na sio siasa. Wanasiasa wazuri wanaianza career hiyo mapema sio ukishachoka ofisini mwishoe unaishia kusema ndiooooooo bungeni hata kama hoja ni ya kuwanyonga watz wenzio
 
Askofu mkuu mstaafu John Ramadhani ni baba yake mdogo padri Augustino Ramadhani.
 
Nampongeza. Na sina uhakika kama ana undugu wa damu na Askofu Mkuu mstaafu wa Anglikan Tanzania, Askofu John Ramadhan, ambaye nae kwasasa anaishi huko Zanzibar. Namtakia baraka za bwana ktk kazi yake hiyo ya kiimani.

Mkuu hata mie nilishawahi kusikia kuwa ni ndugu wa damu na huyo Askofu mstaafu... J. Ramadhan
 
Ana nafasi kubwa ya kuendesha kanisa vizuri maana alishawahi kuua akiwa mwanajeshi na alishawahi nyonga akiwa jugde mkuu na mwimbaji akiwa mpiga kinanda - huoni raha hiyo????
 
Jamaa kachanganya madawa haswa

1. Brigadier General
2. Chief Justice
3. Padre

No wonder akawa Arch Bishop wa Anglican na hili kanisa linahitaji mtu kama huyu mana limeyumba sana.
Congratulations
 
Mimi nadhani ni mchungaji na si Padre maana cheo cha padre utumika kwa Kanisa Katoliki na si rahisi kukipata, unakisotea miaka na miaka.
 
Hongera mh.A. Ramadhani,Mungu akubariki katika kazi yako mpya.
 
kama hujui nyamaza au uliza usiropoke tu

Hajaropoka ni ukweli.
Daraja la Upadre liko kanisa Katoliki tu, Wanaofutia , ni Wachungaji au Wainjilisti, Kwa hio huyo jaji mstaafu sio padri bali ni Mchungaji, Mwandishi wa habari kashindwA kutofautisha Watumishi wa Katoliki na Anglican.
 
Back
Top Bottom