capacity charge
JF-Expert Member
- Mar 26, 2015
- 352
- 489
Umeona ehhHuyu aliondoka na mahakama. Lugakingira, Katiti, Mroso, Kyando baada yao basi
Prof njaa tu hamna kitu. Hivi vyeti alipelekaCarbood alipokuwa rafiki wa mahakama akaamua kuichinjia mbali hoja ya MGOMBEA BINAFS,leo ndo naelewa why aliichinjia mbali,kumbe mgombea binafs hana maslah na chama chake pendwa ambacho leo anakitumikia
IgweeHuyu aliondoka na mahakama. Lugakingira, Katiti, Mroso, Kyando baada yao basi
Brief History of Judge Mwalusanya
Full Name: James Lewis Mwalusanya
Date of Birth: 8th September,1943
Place of Birth: Kililila village in Mbeya Region’s Rungwe District
Education: Tosamaganga Secondary School, 1960
Cambridge School Certificate of Education Examination in 1962
Tabora School (A Levels) between 1963 - 1964
University of E. Africa, Dar es Salaam College (Bachelor of Laws - LL.B), 1965-1969
Other Training: Compulsory National Service training at Makutupora Camp in Dodoma in 1970
Pupilage with Rweyongeza and Co. Advocates of Dodoma in 1998
Career: Resident Magistrate Grade III in March, 1969
Puisne Judge of the High Court of Tanzania in September, 1984
Admitted as an Advocate of the High Court of Tanzania, in 1998
NB: He retired as a Judge of the High Court in 1997
Important Publication: Sheria ya Haki za Binadamu (1988); Upanuzi wa Demokrasia na Uimarishaji wa Haki za Binaadamu Katika Mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi Tanzania: Matumizi ya Katiba na Sheria Zilizopo ili Kudumisha Utulivu, Amani and Mshikamano (1993); Utaratibu wa Sheria wa Kutatua Migogoro ya Kazi: Pale Mfanyakazi Anaapoachishwa Kazi, Kufukuzwa Kazi, Kupunguzwa Kazi, Kupewa Likizo Isiyo na Muda Maalum na bila Malipo au Kustaafishwa kwa Manufaa ya Umma (1993); and Usheria ya Mirathi: Maswali na Majibu Kuhusu Haki za Wajane (1993).
Death: August 1, 2010.
Family: A widow, Bumi, and five children (Mpokigwa Emmanuel, Anna Gulila, Paulina Nabwike, Enelesi Deodatha and Ernest).
Kulikuwa na na J.Korosso na J.Mwaikasu.JAJI MWALUSANYA NA HUKUMU YA KUNYONGWA HADI KUFA.
Mwaka 1994 katika Mahakama Kuu kanda ya Dodoma mbele ya marehemu Jaji Mwalusanya, watu wawili Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula walikutwa na hatia ya kosa la mauaji. Hawa watu wawili waliua mtu na kupora mifugo yake. Walikutwa na kosa la mauaji ya kukusudia (murder) kinyume na kifungu cha 196 cha Penal Code Cap 16. Walitakiwa kupewa hukumu ya kifo kwa mujibu wa kifungu cha 197 cha Penal Code yaani kunyongwa mpaka kufa kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha Penal Code.
Kabla jaji James Mwalusanya hajatoa hukumu hiyo ya kuwanyonga wawili hawa, wakili wa Mbushuu na Sungula Wakili Rweyongeza aliibua hoja kuhusiana na adhabu ya kifo kwamba hukumu ya kifo ni kinyume kabisa cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara 13(6)(d) na (e) kwa maana kwamba hukumu ya kifo ni ya kikatili, ya mateso yaani inayotweza utu wa mtu na isiyo ya kibinadamu. Wakili Rweyongeza alienda mbali zaidi na kusema hukumu ya kifo ni kinyume cha Katiba ibara ya 14 inayotoa haki ya kuishi. Kwa hoja hizo aliiomba mahakama isitoe hukumu ya kifo kwa wateja wake kwani hukumu hiyo ni siyo ya kikatiba (unconstitutional).
Mheshimiwa Jaji Mwalusanya (kama alivyokuwa) alikubaliana moja kwa moja na hoja za wakili Rweyongeza kwamba hukumu ya kifo ni adhabu ya mateso, kinyume cha utu na ubinadamu na ya kikatili. Jaji Mwalusanya alisema ukatili wa hukumu ya kifo unaonekana katika utekelezaji wa hukumu kwani si wa kistaarabu hata kidogo, unapingana na Katiba yetu na pia na Haki za Binadamu.
Katika kusisitiza ubaya wa hukumu ya kifo Jaji Mwalusanya akaandika kwenye hukumu yake maneno haya, ninayanukuu: ".......the process as slow, dirty, horrible, brutal, uncivilized and unspeakably barbaric"
Jaji mwalusanya alisema hukumu ya kifo ni kinyume na ibara ya 14 ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inayotoa haki ya kuishi kwa kila mtanzania. Sababu zingine ni ucheleweshwaji wa utekelezaji wa hukumu hiyo ya kifo na mazingira mabaya ambayo wafungwa wanaosubiri kunyongwa huhifadhiwa.
Jaji Mwalusanya baada ya kupinga vikali kifungu cha sheria cha kanuni ya adhabu ya makosa ya jinai (Penal Code) kifungu cha 197 na kukitangaza kuwa kinapingana na Katiba yaani Unconstitutiona
l, aliwahukumu Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula kifungo cha maisha jela kila mmoja badala ya hukumu ya kifo.
Jaji Mwalusanya alizaliwa tarehe 8/9/1943 huko mkoani Mbeya wilayani Rungwe na kufariki tarehe 1/10/2010 akiwa anaishi mkoani Dodoma ambako ndiko alikoweka makazi yake ya kudumu.
Kwa wanaopenda kusoma maswala ya kisheria watakubaliana nami kuwa huyu Mnyakyusa alikuwa maarufu sana katika utetezi wa maswala ya Haki za Binadamu, na hata hukumu zake nyingi zilijipambanua hivyo. Wakati wa uhai wake aliandika machapisho na vitabu vingi sana, baadhi yake ni pamoja na hivi vifuatavyo:
*Sheria ya Haki za Binadamu (1988)
*Upanuzi wa Demokrasia na Uimarishaji wa Haki za Binaadamu Katika Mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi Tanzania: Matumizi ya Katiba na Sheria Zilizopo ili Kudumisha Utulivu, Amani and Mshikamano (1993)
*Utaratibu wa Sheria wa Kutatua Migogoro ya Kazi: Pale Mfanyakazi Anaapoachishwa Kazi, Kufukuzwa Kazi, Kupunguzwa Kazi, Kupewa Likizo Isiyo na Muda Maalum na bila Malipo au Kustaafishwa kwa Manufaa ya Umma (1993)
*Sheria ya Mirathi: Maswali na Majibu Kuhusu Haki za Wajane (1993).
Je unataka kujua zaidi kuhusu historia ya Mnyakyusa huyu? Kama jibu ni ndiyo, basi endelea kuniombea ili mpango wangu wa kukiandika kitabu cha "WANYAKUSA MASHUHURI" ufanikiwe. Kwenye kitabu hicho utajua mengi kuhusu Wanyakyusa wengi waliopata kuwa mashuhuri kwenye mambo mbalimbali ya kielimu, kiutamaduni, kisiasa, kiuchumi, kijamii na kadhalika.
Ahsanteni sana, ndaga fijo!!
[emoji767] Lusako
RIP Jaji wa ukweli.
Brief History of Judge Mwalusanya
Full Name: James Lewis Mwalusanya
Date of Birth: 8th September,1943
Place of Birth: Kililila village in Mbeya Region’s Rungwe District
Education: Tosamaganga Secondary School, 1960
Cambridge School Certificate of Education Examination in 1962
Tabora School (A Levels) between 1963 - 1964
University of E. Africa, Dar es Salaam College (Bachelor of Laws - LL.B), 1965-1969
Other Training: Compulsory National Service training at Makutupora Camp in Dodoma in 1970
Pupilage with Rweyongeza and Co. Advocates of Dodoma in 1998
Career: Resident Magistrate Grade III in March, 1969
Puisne Judge of the High Court of Tanzania in September, 1984
Admitted as an Advocate of the High Court of Tanzania, in 1998
NB: He retired as a Judge of the High Court in 1997
Important Publication: Sheria ya Haki za Binadamu (1988); Upanuzi wa Demokrasia na Uimarishaji wa Haki za Binaadamu Katika Mfumo wa Demokrasia ya Vyama Vingi Tanzania: Matumizi ya Katiba na Sheria Zilizopo ili Kudumisha Utulivu, Amani and Mshikamano (1993); Utaratibu wa Sheria wa Kutatua Migogoro ya Kazi: Pale Mfanyakazi Anaapoachishwa Kazi, Kufukuzwa Kazi, Kupunguzwa Kazi, Kupewa Likizo Isiyo na Muda Maalum na bila Malipo au Kustaafishwa kwa Manufaa ya Umma (1993); and Usheria ya Mirathi: Maswali na Majibu Kuhusu Haki za Wajane (1993).
Death: August 1, 2010.
Family: A widow, Bumi, and five children (Mpokigwa Emmanuel, Anna Gulila, Paulina Nabwike, Enelesi Deodatha and Ernest).
Usipoteze nguvu zako kumjibu,achana nae. Watu wa vile huwa aidha hawajielewi au wana stress wanatafuta pa kuangukia.Ulikuwa unayasoma ili iweje?
Wote wamefanya kazi mahakama kuu MbeyaKulikuwa na na J.Korosso na J.Mwaikasu.
Wadilifu Wa ukweli.mmoja ametangulia kupumzika.RIP.
kwa kweli ndio maana hospitali huwa zina dipatiment mbalimbali kama vile meno, macho, AKILI, wajawazito n.kYote hayo yanatusaidia nini kwa sasa Iitapwa au umemkumbuka tu Judge Mwalusanya na kulazimisha tuijue familia yake na watoto wake,