Jubilee ya miaka 70 ya taifa la Israel na ufunguzi wa ubalozi wa Marekani katika jiji la Yerusalem

MWAISEMBA CR

Member
Apr 21, 2014
86
78
UHUSIANO WA JUBILEE YA MIAKA 70 YA ISRAEL NA KURUDI KWA YESU KULINYAKUA KANISA✳

*Na: Shujaa Charles Mwaisemba*

_▶SHEREHE YA MIAKA 70(JUBEILEE) YA TAIFA LA ISRAEL_
_▶UFUNGUZI WA UBALOZI WA MAREKANI HUKO JERUSALEM_
_▶MAANDAMANO YA WAPALESTINA DHIDI YA ISRAELI_

✍Ili kuweza kuelewa Msingi wa Somo letu,Ni muhimu kuelewa Matukio makuu matatu yaliyotabiriwa na Manabii na Yesu mwenyewe kuwa yatatokea Siku za mwisho kama dalili kuu za kuja kwa Bwana Yesu kulinyakua kanisa lake

*TUKIO LA 1⃣ : _WAYAHUDI WATARUDI KATIKA NCHI YA ISRAEL { YEREMIA 30:3}_*

Wayahudi walikuwa wametawanywa dunia nzima katika mwaka 70B.K,tokea wakati huo,kwa karibu miaka 2000 hawakuwa na nchi iliyokuwa yao wenyewe, ni kwasababu walimfanya Mungu dhambi .

Mara baada ya vita vya pili vya dunia,Mwaka 1945 kuisha Wayahudi kutoka pande zote walianza kujikusanya mmoja mmoja kwa namna kama wanaambia kuwa warudi kwenye nchi yao. Kulianza kufanyika mipango mingi kwenye mabunge na Nchi za Ulaya na marekani kuhusu Israel ndipo kwa ghafla ikiwa kama sauti ya kuambiana imewajia kwa wakati mmoja kuanza kurudi mmoja baada ya wengine na kuwakuta Wenyeji wao Wapalestina katika maeneo hayo

Waingereza pamoja na wamarekani waliwasaidia sana kuwafukuza Wapalestina maeneo Haya ya sasa Ya Israel ili kuwaruhusu Wanaisrael kufika maeneo hayo.Na kwa pamoja ndani ya Muda mfupi wanayahudi walikusanyika na kuwa wengi sana hata kupelekea kuanza kutaka tena Israel litambulike kama Taifa.

*TUKIO LA 2⃣: _ISRAEL LITAKUWA TAIFA TENA_*

Tukio hili litimia katika Mwezi *May 14, 1948* ambapo Israel ikaanza tena kutambulika kama Taifa huru baada ya kupotea katika Uso wa dunia kwa miaka mingi ya nyuma iliyopita .Na Eneo hilo kumilikiwa na Hawa Wapalestina kwa muda wote hivyo tangu wakati huo Wapalestina kufukuzwa kwa nguvu kuwapisha wayahudi sehemu yao ndipo kulipoanza uhasama wa muda mrefu baina ya mataifa haya mawili ambayo wote wanadai Ardhi hiyo ni milki yake.

Hivyo kumekuwepo na mapigano ya Muda mrefu dhidi ya Wayahudi(Wana Israel) na Wapalestina ambapo Israel wanazidi kujitanua kuchukua maeneo na mipaka yao ya zamani iliyokuwepo hadi kwenye maandiko hasa Mpaka kwenye Mji wa Yerusalem ambapo ndipo Ngome pia ya Wapalestina na Waislamu kote ulimwenguni maana ndipo kulipokuwepo Msikiti wao mkubwa unaoheshimika unaoitwa *AL-AQSA* Na huku Israel nao wakidai eneo hilo ni lao kwakuwa ndipo kulipokuwepo na Hekalu la Suleiman

*TUKIO LA 3⃣ : _JIJI LA YERUSALEM LITAKUWA HURU KUTOKA KWA MAADUI ZAKE_*

Kwa tukio hili ndio moyo halisi wa somo letu hili,Na hili ndio tukio pekee ambalo lilikuwa limebaki ambalo halijatimizwa kwa Muda mrefu, na hii ni kutokana na Sababu kwanza mpaka sasa Wapalestina bado wanaamini jiji la Yerusalemu lipo chini yao, maana ndipo Pia upo ule msikiti wa kiislamu

Hapa kuna mambo makuu mawili ya kujifunza na kuyaelewa kama Kanisa au Mtu yeyote anayesoma ujumbe huu na ujue jinsi yalivyo na uhusiano mkubwa na kuja kwa Bwana Wetu Yesu

*1⃣ JUBILEE YA MIAKA 70 YA TAIFA LA ISRAEL NA UFUNGUZI WA UBALOZI WA MAREKANI KATIKA JIJI LA YERUSALEM*

Tukio hili na la Muhimu sana na ni la kinabii kabisa ambalo kila mmoja hapaswi kulichukulia kisiasa na kuona kama ni la kawaida Kwani ndio Kutimia kwa tukio hili la Kuutambua Mji wa Yerusalem kama ndio makao Makuu ya Israel ndio tukio pekee lililokuwa limebaki kama Ishara kubwa ya Kurudi kwa Bwana Yesu kulinyakua kanisa

Jambo hili,la ajabu na la kushangaza,Cha ajabu yake limetokea wakati huu huu ambapo Taifa hili la Israel linatimiza miaka 70 tangu kuwapo kwake (1948-1918).Na cha ajabu leo 14/5/2018 ndio Israel inatimiza miaka 70 kamili ya Kuwepo kwake tangu Tarehe 14/5/1948.Kumbuka wakati nafundisha Somo la dhiki kuu!nilishafundisha maana ya 70 katika unabii jinsi ilivyo na maana kubwa kibiblia(Ikiwa hujajifunza kuhusu hilo wasiliana nami kwa namba hizo chini,nitakupatia masomo hayo niliyofundisha kwa urefu kuhusu miaka 70 hiyo na maana yake)

Sambamba na hili Rais wa Marekani, *Donald Trump* alizungumza maneno mazito ambayo yaliushangaza ulimwengu kwa kutamka Hadharani kuwa anautambua *JIJI LA YERUSALEM KAMA NDIO MAKAO MAKUU MAPYA KWA TAIFA LA ISRAEL BADALA YA TELHAVIV* . Na zaidi siku hii hii ya Leo (14/5/2018) ndio amefungua Ubalozi wake wa Marekani katika jiji hilo hilo la *YERUSALEM KAMA ISHARA YA KUUTAMBULISHA KWA DUNIA KUWA NDIO MAKAO MAKUU PA ISRAEL*

Kumbuka nilikuambia,Hapa Yerusalem ndipo pia Eneo linalomilikiwa na wapalestina kwa Muda mrefu na kudai ni eneo lao kwasababu ya kuwepo na msikiti mkubwa wa kislamu duniani *(Sehemu pa pili panaheshimika kwenye nguzo za kiislam)*

Hivyo Kama watakatifu tunapoyaona haya kuwa ndani ya Miaka 70 ya Israel ndipo jiji la Yerusalem kunaanza kutambulika kama Jiji la Israel badala ya Palestina,Basi ni wakati ambapo kama Kanisa tunapaswa kujua mwisho upo karibu sana na Yesu yupo karibu sana kurudi kuja kulinyakuwa Kanisa lake

Sipo kukwambia kwamba Yesu anarudi mwaka huu wa 70 wa Taifa la Israel (Hakuna anayejua Saa wala siku atakayorudi mwana wa adamu) ila nipo kukujulisha juu ya majira na dalili za kurudi kwake alizotuachia Yesu ambaye nae hakutaka tukose kuzijua ili Asije akarudi akatukuta hatujajiandaa Kwa kumlaki Bwana Yesu mawinguni

✍Ila ninachoweza kukwambia wewe unaesoma ujumbe kuwa Yesu yupo karibu kurudi wakati wowote kuanzia sasa maana tukio hili la mwisho limeanza kutimizwa leo hii tarehe 14/5/2018 ,hivyo ikiwa umerudi Nyuma huu ni wakati wa kumrudia upya Bwana,Ikiwa bado hujaojoka huu ni wakati wa kuokoka na Ikiwa umechoka huu na wakati wa kuinuka tena na kuanza upya,Ukiwa ni mtakatifu basi zidi kujitakasa zaidi maana siku tusiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu

✍Jambo lingine nililotaka kukumbusha,Kumbuka ikiwa Israel leo wameshalimiliki Jiji la Yerusalem kama jiji lao basi ujue linalofuata hapo ni kutaka kuubomoa huo *msikiti wa AL-AQSA* na kutaka kujenga tena Hekalu 3 la Suleiman ambapo ndipo litakaposimamishwa Chukizo la Uharibifu mahali patakatifu ambapo Mpinga Kristo atakuwa ameshadhihirishwa tayari.Hivyo unapata kuelewa ni jinsi gani tulivyokuwa tumeshamaliza muda wetu hapa duniani.Kumbuka matukio hayo ya kubomolewa kwa Msikiti na Kuja kwa mpinga Kristo hakutakuwa na Nguvu kabla kanisa Kunyakuliwa Hivyo kumbe kabla ya haya kutokea lazima sisi watakatifu tuwe tumeshanyakuliwa.

*2⃣ MAANDAMANO MAKUBWA YA WAPALESTINA DHIDI YA ISRAEL KUCHUKUA JIJI LAO LA YERUSALEM*

Kama mtu wa rohoni ni Muhimu kuelewa Pamoja matukio haya kwetu yanatupa kujiandaa na kunyakuliwa kanisa ua Kuja kwa Bwana Yesu kulinyakuwa Kanisa lakini upande wa Pili,utakuwa ni mwanzo mkubwa na endelevu wa kuzifungulia kazi za Mpinga Kristo kuanza kufanya kazi kwa nguvu kubwa kuliko wakati wowote *2THETHALONIKE 2:7*

Na moja ya Kazi za Mpinga Kristo zinazotenda kazi baada ya haya yote kutokea siku ya leo 14/5/2018 *(Ufunguzi wa ubalozi wa marekani &Jubilee ya miaka 70 ya Taifa la Israel)* ni hili la Maandamano ya nchi nzima ya wapalestina dhidi ya Israel Kupinga vikali Israel kuchukua jiji lao la Yerusalem

✍Maandamano haya yalianza muda mrefu(15/4/1948) tangu Mwanzoni kabisa mwa Taifa la Israel mara baada ya kutangwa ambapo Wapalestina walifukuzwa kutoka eneo lilikaliwa na israel yaliyopelekea kuketa janga kubwa la kupoteza watu zaidi ya 700,000.Lakini mwaka 1998 ndipo *Rais Yesser arafat* ndipo siku hiyo ikapewa jina la *Catastophe disaster au Siku ya Nakba(Kiarabu) au siku ya janga* ambapo imekuwa ikitumika kuhamashana ili kurudi tena nchini pao( Yaani Eneo wanalokaa Israel Sasa)

✍Ila Maandamano ya Mwaka huu ambayo yanaanza Rasmi leo (15/5/2018) ingawa tangu jana(14/5/2018) tayari walikuwa wameshayaanza ili kuzuia Haya matukio mawili yasitokee ya kusherekea Miaka 70 ya Taifa la Israel na kuzinduliwa kwa Ubalozi wa marekani palaYerusalemu ambapo ndipo pametangazwa kuwa ni Mjii kuu wa Israel ambapo mpaka sasa Wapalestina Maelfu kwa maelfu ya watu wamekusanyika Kuuzunguka Israel na kuta zote za Yerusalem ili kupinga maamuzi haya ya *Rais wa marekani Donald Trump* Kuufanya Yerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Na mpaka sasa watu zaidi ya 50 wamekufa kwenye maandamano hayo na watu zaidi ya 1400 wameumizwa vibaya na kujeruhiwa

Na Vuguvugu hili la maandamano linaloendelea mpaka sasa litakuwa ni Endelevu maana Sasa umekuwa si tu Ugomvi kati ya Israel na Palestina bali Mgogoro kati ya Mataifa yote ya Kiislam yaliyo chini OIC Kuisaidia Palestina katika Vita hivyo na Upande wa pili,Israel kusaidiwa na Marekani pamoja na Mataifa mengi ya kikristo ambayo yanataka kumuunga mkono mmarekani Kwa kufungua balozi zao hapo hapo Yerusalem

Hapa ndipo Mahali pa Msingi kufahamu kama Kanisa au kama watu wa Rohoni tusio vipofu,Kuacha kushabikia haya mambo kisiasa na Kushindana na *DONALD TRUMP* Na kumlaani kwa kitendo anachofanya cha Kuisaidia Israel kuupata mji mkuu wao wa Yerusalem.Kwa hili *Donald Trump(Rais wa Marekani)* anatumiwa na Mungu kwa viwango vya juu kutimiza unabii ule tuliouona Kuhakikisha *YERUSALEM UNAWEKWA HURU KUTOKA KWA MAADUI ZAKE(WAPALESTINA)*

Hivyo kama Kanisa tuyaonapo haya hatunabudi *KUIOMBEA AMANI ISRAEL*,Kumuombea Mmarekani na wote wanaoisadia Israel katika Vita hii na maandamano haya yaliyokusudiwa kufanyika kwa muda mrefu na wakati endelevu kupingana na Israel.Huu ni wakati kila aliye Upande wa Mungu kuitakia heri Israel,Kuiombea Amani na ndipo tutakapofanikiwa kama Maandiko yasemavyo

*♨{ ZABURI 122:6}*
*_" Utakieni Yerusalem Amani(Pray for Peace for Jerusalem) na wote wanaipenda watafanikiwa"_*

✍Ndugu zangu kuna baraka tele tutazipata kama tukiombea sana Israel wakati huu kuliko wakati wowote ndipo tutakapofanikiwa,Vinginevyo tutakaribisha Laana juu ya Laana juu yetu au juu ya nchi zetu.Hivyo tuendelee kukemea kazi za Mpinga Kristo zinazoaanza kufanya kazi nyakati hizi kabla Kanisa halijanyakuliwa,Tuombe na tukemee kuwa mipango yote inayopangwa juu ya Israel isipate kufanikiwa bali tukaone kweli wakiumiliki Mji wao kama ilivyotabiriwa

‍♂Je umejifunza nini Mpaka hapo? *IKIWA UMEBARIKIWA NA SOMO HILI* basi usiache kushare kwa wengine nao wayafahamu haya kama ulivyofahamu wewe.Share facebook,Share Whatsap group na kwa marafiki zako wote au ndugu zako wote,Ili nae apokee maonyo haya ili yamkini asije akaingia katika mtego wa kuilaani Israel na zaidi asije akaishi tu bila kufanya maandalizi ya maisha na Yesu akarudi bila kumnyakua

Ikiwa hujaokolewa ila baada ya somo hili unahitaji kuokoka basi wasiliana nami kwa namba hapo chini nami nitakuombea upewe Uwezo wa kushinda dhambi na kuokoka ila ikiwa pia umebarikiwa au una swali au unahitaji ushauri pia usisite kuwasiliana nami kwa namba hzio hapo chini. *MUNGU AKUBARIKI*

* Na: Shujaa Charles Mwaisemba*
*0712-054498/0759-420202*
_stmwaisembac@gmail.com_
 
*MFULULIZO WA MASOMO YANAYOHUSIANA NA KUTAMBULIWA KWA MJI WA YERUSALEM KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL*

*✳SOMO 1: KUFUTWA KWA TAIFA LA ISRAEL✳*

* Na:Shujaa Charles Mwaisemba*

* TANGAZO RASMI LA RAIS WA MAREKANI DHIDI YERUSALEM*

*UTABIRI WA YESU KUBOMOLEWA KWA HEKALU*

* KUFUKUZWA KWA TAIFA LA ISRAEL NA KUBOMOLEWA KWA HEKALU*

*1⃣UTANGULIZI*

Kwa muda mfupi sasa umepita kumekuwepo na mijadala mingi sana katika mitandao ya kijamii,Magroup ya whatsap na Forum mbalimbali kote duniani kujadili juu ya hili swala la Israel na Palestina hasa Kuhusu Marekani kuutambua Mji wa Yerusalem kama makao makuu ya Taifa la Israel na juu ya Marekani kuhamisha ubalozi wake kuupeleka Yerusalem

✍Jambo hili limechukua sura mpya sana katika vyombo vya habari na Magazeti na mijadala ya wiki nzima ambapo wengi wasio na maarifa ya Neno la Mungu wamechuliwa na Upepo na wimbi la roho ya Mpinga Kristo Kupinga vikali juu ya Uamuzi uliofanywa na Rais Marekani dhidi ya jiji Yerusalem.

✍Ni makusudi ya Mfululizo huu kwamba kila mmoja si tu awe na maarifa sahihi bali awe upande wa Mungu kuzipinga roho zote za Mpinga Kristo zinazoletwa kupinga Unabii wa Mungu usitimie au Mapenzi ya Mungu kwa Kanisa na Israel kwa Ujumla Usitimie.Hivyo ikiwa umeanza nami kwa somo hili hakikisha unafuatilia mpaka Mwisho wa Mfululizo huu ambao utakuwa na masomo kadhaa ambapo tutajifunza mambo mengi ya kibiblia na Unabii wa Miaka 70 juu ya Israel na kanisa na mengine Mengi ambayo Masikio yako yatawasha yakiyasikia kwamba Kumbe yaliandikaa kwenye biblia⁉

*2⃣ TANGAZO LA RAIS WA MAREKANI JUU YA YERUSALEMU*

Mwishoni kabisa wa mwaka 2017,Dec ,6 Rais wa Marekani, *DONALD TRUMP* Alitoa Tangazo kubwa la kutangaza Rasmi kuutambua Mji wa Yerusalem kuwa ni Makao makuu ya Israel, na kudai kuwa Yerusalem tangu Mwanzo Kabisa ulikuwa ni Israel na ulitambulika kama *MJI WA DAUDI {2SAMWELI 5:4-9 }* Jambo ambalo lilisisimua dunia kwa ujumla wake kwa Tamko hilo

Lakini baada ya Tamko na Tangazo hili kwa Ulimwengu,Yameinuka mataifa mengi ambayo yamesimama na kupinga vikali Marekani Kufanya hivyo kuwa eti wanahatarisha Amani ya dunia.Lakini ni Muhimu kuelewa Mataifa mengi hayo yanayopinga ni kwasababu ya Roho za Mpinga Kristo zinafanya kazi ndani yao wasijue undani wa maswala ya kiroho kwa jambo hilo

Ni muhimu kuelewa kuwa Kutangazwa kwa Yerusalem kama Makao makuu ya Israel,kuna viashiria vikubwa sana katika siku za Mwisho

*3⃣ UTABIRI WA YESU,KUBOMOLEWA KWA YERUSALEMU*

✍Mwisho Kabisa kabla ya Mateso yake Bwana Yesu akiwa anauingia Mji wa Yerusalemu katika huduma yake duniani *ALIULILIA MJI WA YERUSALEMU* akatamka maneno haya katika
*♨{ LUKA 19:41-44}*
_"Alipofika karibu aliuona mji, *akaulilia*,akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.Kwa kuwa siku zitakuja, *adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini* wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, *kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa* kwako. Yesu Atakasa Hekalu"_

Yesu aliwaeleza kuwa Yerusalem Mzima itabomolewa Kwakuwa Wayahudi walikuaa wakiringia sana hilo Hekalu la Suleiman ,Hawakuwa Tayari hata kumpokea Yesu kristo kama Masihi wao wala hawakumsikia kwa lolote lile ndio maana walikuwa waifanya hadi machukizo ndani ya Nyumba ya Mungu *(LUKA 19:45-46)*

Yesu alikuwa akitabiri na kusema kuwa Mji mzima wa Yerusalem utabomolewa na hekalu nalo litabomolewa wala halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa na ndivyo ilivyotokea

*4⃣ KUFUKUZWA KWA TAIFA LA ISRAEL NA KUBOMOLEWA KWA HEKALU*

Kufukuzwa kwa Taifa la Israel kulikuwa kwa Awamu 2 tofauti
Miaka karibu 30 baadae baada ya kauli ile ya Yesu Kama tulivyoisoma,Basi ilipofika Mwaka 66 -70 B.K wayahudi walifanya uasi dhidi ya Mfalme na Himya ya Kirumi iliyokuwa inatawala,Hivyo kulitokea mapambano makali yapata miaka 4 ya vita hiyo dhidi ya israel Mpaka kupelekea Hekalu Kubomolewa

Tamko likatolewa kuwa Wayahudi hawatakiwi Yerusalem na waliteswa sana wakati huo na kuonekana kama wahaini,Hivyo kupelekea wayahudi wengi wakaanza kukimbia kwenhe miji yao na nchi yao ingawa kulikuwepo na Wachache walioendelea kubaki kwenye maeneo na miji yao ambayo haikubomolewa yote ingawa hekalu lilikuwa limeshabomolewa

Baada ya Tukio la kwanza la kubomolewa kwa Hekalu lile la Suleimani,Mwaka 118 B.K , *Mfalme Hadrian* alitokea na kuwaambia wale waliobaki kuwa wanaweza kuwepo tena Yetusalemu na kuwaahidi kuwa wataweza tena kujenga lile hekalu

Lakini muda si mrefu baada ya Wayahudi kuanza kujenga jenga makazi yaliyokuwa yameharibiwa ndipo wakaanza kumdai Mfalme huyo atimize ahadi yake ili waanze kujenga hekalu ,Lakini mfalme akawa tayari amebadilisha mawazo
▶ Aliwaruhusu Kujenga hilo hekalu lakini sio Pale pa mwanzo bali ni mbali kabisa na Eneo lile,Jambo ambalo wayahudi walilipinga kabisa
▶ Akawabadilikia zaidi na ile ahadi kwamba angekuwa Rafiki yao hakuitimiza bali alikuwa kinyume nao kabisa

Mwaka 132 B.K Ndipo israel wakafanya Uasi Mkubwa mwingine dhidi ya Mfalme huyo wa kirumi ambao uliitwa *Bar-Kokhba Revolt*( uasi dhidi ya Serikali) ambao ulikuwa mkubwa kuliko ule wa mwanzo.Ndipo kulipofanyika vita nyingine kubwa kuliko ile ya mara ya kwanza mwaka 132-135B.K na na ule mji wote ukavunjwa vunjwa kabisa na watu wengi waliuwawa wala hakukusalia nyumba iliyobaki,

Walipigwa Marufuku kwa Myahudi kuwepo kwenye Nchi ile,hivyo kupelekea hao waliobakia,wakakimbia na kutawanyika sehemu mbalimbali duniani ili litimie Neno lililotabiriwa katika unabiii kuwa *_" Israel watakapokuwa wameasi,watatawanywa na kwenda kila mahali kwenye kona zote za dunia"_*
*♨{EZEKIELI 36:16-19}*
_Tena, neno la BWANA likanijia, kusema,Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokaa katika nchi yao wenyewe, *waliitia uchafu kwa njia yao na kwa matendo yao*. Njia yao mbele zangu ilikuwa kama uchafu wa mwanamke wakati wa kutengwa kwake.Kwa hiyo *nalimwaga hasira yangu juu yao,* kwa ajili ya damu waliyoimwaga juu ya nchi, na kwa sababu wameitia uchafu kwa vinyago vyao. *Nikawatawanya katika mataifa, wakatapanyika katika nchi nyingi; kwa kadiri ya njia yao, na kwa kadiri ya matendo yao*, naliwahukumu."_

*♨ {KUMBUKUMBU 28:64}*
_" *BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia*; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe."_

Hivyo ndivyo Israel walivyotawanywa na kufukuzwa katika Taifa lao na ndivyo hekalu hilo la suleiman na makao yao yote yalivyobomolewa bila kubakia jiwe juu ya jiwe lilisalia kule kama Yesu alivyosema ndivyo ilivyopelekea Tangu wakati huo Wayahudi walitawanyika na kwenda Pande zote nne za dunia kwani wengine walienda Afrika,Wengine Urusi,wengine Ulaya na mwisho wengine wakaenda Marekani baadae sana

Hapo ndipo hilo Taifa likafutwa na kutokuwepo tena kama Taifa la Israel,Bali Mfalme aliyekuwepo aliita jina jipya mji huo *AILIA-CAPITOLINA*

⚠ Ndugu yangu hapa ninapohitimisha kuhusu hili hatuna budi kujifunza kitu Kimoja ambacho nasi kitupe taadhari Kuwa Neno lolote alilolisema Yesu lazima litimie.ikiwa alisema Yerusalem itabomolewa wala lisisalie jiwe juu ya jiwe na kweli kihistoria na kimaandiko yakatimia

Oooh ndugu yangu unayefuatilia somo hili tusiyapuuze maneno ya Yesu aliyosema na kutabiri juu kuja kwake kulinyakuwa kanisa safi lisilo na doa wala waa *WAEFESO 5:25-27*,Tusipuuze tukawa kama hawa wana israel bali ndio uwe wakati wa kujiandaa kwa utakatifu ambao pasipo huo hakuna mgu atayemuona Mungu.Huu si wakati wa kuendelea kung'ang'ania dini zetu badala ya kutafuta wokovu Kwa kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha.Si wakati wa kuendelea na wokovu vuguvugu,unafanya dhambi sirini ila kanisani unajionyesha ni mtakatifu

⚠Kama yalivyowajiria mabaya wayahudi kwa kutawanywa kutoka katika nchi yao ndivyo ambapo Mungu nae atakapokufukuza utoke mbele zake uende kwenye moto wa milele pamoja na shetani kwa maana uliyapuuza maneno kama haya yanayokutaka utubu ,uliyapuuza maneno kama haya yanayo yanayokuonya kuwa usiishi maisha ya unafiki na maisha ya Uvuguvugu,Ya kufanya dhambi sirini! *ACHA NAKWAMBIA ACHA‼* Mungu amekupenda ndio maana amekula nafasi usome ujumbe huu ili utubu, *USIPUUZE‼*.Ikiwa utahitaji kuanza upya na Bwana Yesu basi wasiliana nami kwa namba hizo hapo chini nami nitakuombea utapewa uwezo wa kushinda dhambi‼

*USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU ZINAZOFUATA ZA MFULULIZO HUU*

♨Kwa mawasiliano Zaidi
* Na:Shujaa Charles Mwaisemba*
*0712054498/0759420202*
_stmwaisembac@gmail.com_
 
matthew 24:36 But of that day and hour knoweth no man, no, not the angels of heaven, but my Father only.
 
Vip, Watumishi wa Bwana/Wakristo hawapo wa kuchangia hii mada au mada haina uhalisia????
Anyway Thanks kwa ubarikio
 
UHUSIANO WA JUBILEE YA MIAKA 70 YA ISRAEL NA KURUDI KWA YESU KULINYAKUA KANISA

*Na: Shujaa Charles Mwaisemba*

_SHEREHE YA MIAKA 70(JUBEILEE) YA TAIFA LA ISRAEL_
_UFUNGUZI WA UBALOZI WA MAREKANI HUKO JERUSALEM_
_MAANDAMANO YA WAPALESTINA DHIDI YA ISRAELI_

Ili kuweza kuelewa Msingi wa Somo letu,Ni muhimu kuelewa Matukio makuu matatu yaliyotabiriwa na Manabii na Yesu mwenyewe kuwa yatatokea Siku za mwisho kama dalili kuu za kuja kwa Bwana Yesu kulinyakua kanisa lake

*TUKIO LA : _WAYAHUDI WATARUDI KATIKA NCHI YA ISRAEL { YEREMIA 30:3}_*

Wayahudi walikuwa wametawanywa dunia nzima katika mwaka 70B.K,tokea wakati huo,kwa karibu miaka 2000 hawakuwa na nchi iliyokuwa yao wenyewe, ni kwasababu walimfanya Mungu dhambi .

Mara baada ya vita vya pili vya dunia,Mwaka 1945 kuisha Wayahudi kutoka pande zote walianza kujikusanya mmoja mmoja kwa namna kama wanaambia kuwa warudi kwenye nchi yao. Kulianza kufanyika mipango mingi kwenye mabunge na Nchi za Ulaya na marekani kuhusu Israel ndipo kwa ghafla ikiwa kama sauti ya kuambiana imewajia kwa wakati mmoja kuanza kurudi mmoja baada ya wengine na kuwakuta Wenyeji wao Wapalestina katika maeneo hayo

Waingereza pamoja na wamarekani waliwasaidia sana kuwafukuza Wapalestina maeneo Haya ya sasa Ya Israel ili kuwaruhusu Wanaisrael kufika maeneo hayo.Na kwa pamoja ndani ya Muda mfupi wanayahudi walikusanyika na kuwa wengi sana hata kupelekea kuanza kutaka tena Israel litambulike kama Taifa.

*TUKIO LA : _ISRAEL LITAKUWA TAIFA TENA_*

Tukio hili litimia katika Mwezi *May 14, 1948* ambapo Israel ikaanza tena kutambulika kama Taifa huru baada ya kupotea katika Uso wa dunia kwa miaka mingi ya nyuma iliyopita .Na Eneo hilo kumilikiwa na Hawa Wapalestina kwa muda wote hivyo tangu wakati huo Wapalestina kufukuzwa kwa nguvu kuwapisha wayahudi sehemu yao ndipo kulipoanza uhasama wa muda mrefu baina ya mataifa haya mawili ambayo wote wanadai Ardhi hiyo ni milki yake.

Hivyo kumekuwepo na mapigano ya Muda mrefu dhidi ya Wayahudi(Wana Israel) na Wapalestina ambapo Israel wanazidi kujitanua kuchukua maeneo na mipaka yao ya zamani iliyokuwepo hadi kwenye maandiko hasa Mpaka kwenye Mji wa Yerusalem ambapo ndipo Ngome pia ya Wapalestina na Waislamu kote ulimwenguni maana ndipo kulipokuwepo Msikiti wao mkubwa unaoheshimika unaoitwa *AL-AQSA* Na huku Israel nao wakidai eneo hilo ni lao kwakuwa ndipo kulipokuwepo na Hekalu la Suleiman

*TUKIO LA : _JIJI LA YERUSALEM LITAKUWA HURU KUTOKA KWA MAADUI ZAKE_*

Kwa tukio hili ndio moyo halisi wa somo letu hili,Na hili ndio tukio pekee ambalo lilikuwa limebaki ambalo halijatimizwa kwa Muda mrefu, na hii ni kutokana na Sababu kwanza mpaka sasa Wapalestina bado wanaamini jiji la Yerusalemu lipo chini yao, maana ndipo Pia upo ule msikiti wa kiislamu

Hapa kuna mambo makuu mawili ya kujifunza na kuyaelewa kama Kanisa au Mtu yeyote anayesoma ujumbe huu na ujue jinsi yalivyo na uhusiano mkubwa na kuja kwa Bwana Wetu Yesu

* JUBILEE YA MIAKA 70 YA TAIFA LA ISRAEL NA UFUNGUZI WA UBALOZI WA MAREKANI KATIKA JIJI LA YERUSALEM*

Tukio hili na la Muhimu sana na ni la kinabii kabisa ambalo kila mmoja hapaswi kulichukulia kisiasa na kuona kama ni la kawaida Kwani ndio Kutimia kwa tukio hili la Kuutambua Mji wa Yerusalem kama ndio makao Makuu ya Israel ndio tukio pekee lililokuwa limebaki kama Ishara kubwa ya Kurudi kwa Bwana Yesu kulinyakua kanisa

Jambo hili,la ajabu na la kushangaza,Cha ajabu yake limetokea wakati huu huu ambapo Taifa hili la Israel linatimiza miaka 70 tangu kuwapo kwake (1948-1918).Na cha ajabu leo 14/5/2018 ndio Israel inatimiza miaka 70 kamili ya Kuwepo kwake tangu Tarehe 14/5/1948.Kumbuka wakati nafundisha Somo la dhiki kuu!nilishafundisha maana ya 70 katika unabii jinsi ilivyo na maana kubwa kibiblia(Ikiwa hujajifunza kuhusu hilo wasiliana nami kwa namba hizo chini,nitakupatia masomo hayo niliyofundisha kwa urefu kuhusu miaka 70 hiyo na maana yake)

Sambamba na hili Rais wa Marekani, *Donald Trump* alizungumza maneno mazito ambayo yaliushangaza ulimwengu kwa kutamka Hadharani kuwa anautambua *JIJI LA YERUSALEM KAMA NDIO MAKAO MAKUU MAPYA KWA TAIFA LA ISRAEL BADALA YA TELHAVIV* . Na zaidi siku hii hii ya Leo (14/5/2018) ndio amefungua Ubalozi wake wa Marekani katika jiji hilo hilo la *YERUSALEM KAMA ISHARA YA KUUTAMBULISHA KWA DUNIA KUWA NDIO MAKAO MAKUU PA ISRAEL*

Kumbuka nilikuambia,Hapa Yerusalem ndipo pia Eneo linalomilikiwa na wapalestina kwa Muda mrefu na kudai ni eneo lao kwasababu ya kuwepo na msikiti mkubwa wa kislamu duniani *(Sehemu pa pili panaheshimika kwenye nguzo za kiislam)*

Hivyo Kama watakatifu tunapoyaona haya kuwa ndani ya Miaka 70 ya Israel ndipo jiji la Yerusalem kunaanza kutambulika kama Jiji la Israel badala ya Palestina,Basi ni wakati ambapo kama Kanisa tunapaswa kujua mwisho upo karibu sana na Yesu yupo karibu sana kurudi kuja kulinyakuwa Kanisa lake

Sipo kukwambia kwamba Yesu anarudi mwaka huu wa 70 wa Taifa la Israel (Hakuna anayejua Saa wala siku atakayorudi mwana wa adamu) ila nipo kukujulisha juu ya majira na dalili za kurudi kwake alizotuachia Yesu ambaye nae hakutaka tukose kuzijua ili Asije akarudi akatukuta hatujajiandaa Kwa kumlaki Bwana Yesu mawinguni

Ila ninachoweza kukwambia wewe unaesoma ujumbe kuwa Yesu yupo karibu kurudi wakati wowote kuanzia sasa maana tukio hili la mwisho limeanza kutimizwa leo hii tarehe 14/5/2018 ,hivyo ikiwa umerudi Nyuma huu ni wakati wa kumrudia upya Bwana,Ikiwa bado hujaojoka huu ni wakati wa kuokoka na Ikiwa umechoka huu na wakati wa kuinuka tena na kuanza upya,Ukiwa ni mtakatifu basi zidi kujitakasa zaidi maana siku tusiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu

Jambo lingine nililotaka kukumbusha,Kumbuka ikiwa Israel leo wameshalimiliki Jiji la Yerusalem kama jiji lao basi ujue linalofuata hapo ni kutaka kuubomoa huo *msikiti wa AL-AQSA* na kutaka kujenga tena Hekalu 3 la Suleiman ambapo ndipo litakaposimamishwa Chukizo la Uharibifu mahali patakatifu ambapo Mpinga Kristo atakuwa ameshadhihirishwa tayari.Hivyo unapata kuelewa ni jinsi gani tulivyokuwa tumeshamaliza muda wetu hapa duniani.Kumbuka matukio hayo ya kubomolewa kwa Msikiti na Kuja kwa mpinga Kristo hakutakuwa na Nguvu kabla kanisa Kunyakuliwa Hivyo kumbe kabla ya haya kutokea lazima sisi watakatifu tuwe tumeshanyakuliwa.

* MAANDAMANO MAKUBWA YA WAPALESTINA DHIDI YA ISRAEL KUCHUKUA JIJI LAO LA YERUSALEM*

Kama mtu wa rohoni ni Muhimu kuelewa Pamoja matukio haya kwetu yanatupa kujiandaa na kunyakuliwa kanisa ua Kuja kwa Bwana Yesu kulinyakuwa Kanisa lakini upande wa Pili,utakuwa ni mwanzo mkubwa na endelevu wa kuzifungulia kazi za Mpinga Kristo kuanza kufanya kazi kwa nguvu kubwa kuliko wakati wowote *2THETHALONIKE 2:7*

Na moja ya Kazi za Mpinga Kristo zinazotenda kazi baada ya haya yote kutokea siku ya leo 14/5/2018 *(Ufunguzi wa ubalozi wa marekani &Jubilee ya miaka 70 ya Taifa la Israel)* ni hili la Maandamano ya nchi nzima ya wapalestina dhidi ya Israel Kupinga vikali Israel kuchukua jiji lao la Yerusalem

Maandamano haya yalianza muda mrefu(15/4/1948) tangu Mwanzoni kabisa mwa Taifa la Israel mara baada ya kutangwa ambapo Wapalestina walifukuzwa kutoka eneo lilikaliwa na israel yaliyopelekea kuketa janga kubwa la kupoteza watu zaidi ya 700,000.Lakini mwaka 1998 ndipo *Rais Yesser arafat* ndipo siku hiyo ikapewa jina la *Catastophe disaster au Siku ya Nakba(Kiarabu) au siku ya janga* ambapo imekuwa ikitumika kuhamashana ili kurudi tena nchini pao( Yaani Eneo wanalokaa Israel Sasa)

Ila Maandamano ya Mwaka huu ambayo yanaanza Rasmi leo (15/5/2018) ingawa tangu jana(14/5/2018) tayari walikuwa wameshayaanza ili kuzuia Haya matukio mawili yasitokee ya kusherekea Miaka 70 ya Taifa la Israel na kuzinduliwa kwa Ubalozi wa marekani palaYerusalemu ambapo ndipo pametangazwa kuwa ni Mjii kuu wa Israel ambapo mpaka sasa Wapalestina Maelfu kwa maelfu ya watu wamekusanyika Kuuzunguka Israel na kuta zote za Yerusalem ili kupinga maamuzi haya ya *Rais wa marekani Donald Trump* Kuufanya Yerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Na mpaka sasa watu zaidi ya 50 wamekufa kwenye maandamano hayo na watu zaidi ya 1400 wameumizwa vibaya na kujeruhiwa

Na Vuguvugu hili la maandamano linaloendelea mpaka sasa litakuwa ni Endelevu maana Sasa umekuwa si tu Ugomvi kati ya Israel na Palestina bali Mgogoro kati ya Mataifa yote ya Kiislam yaliyo chini OIC Kuisaidia Palestina katika Vita hivyo na Upande wa pili,Israel kusaidiwa na Marekani pamoja na Mataifa mengi ya kikristo ambayo yanataka kumuunga mkono mmarekani Kwa kufungua balozi zao hapo hapo Yerusalem

Hapa ndipo Mahali pa Msingi kufahamu kama Kanisa au kama watu wa Rohoni tusio vipofu,Kuacha kushabikia haya mambo kisiasa na Kushindana na *DONALD TRUMP* Na kumlaani kwa kitendo anachofanya cha Kuisaidia Israel kuupata mji mkuu wao wa Yerusalem.Kwa hili *Donald Trump(Rais wa Marekani)* anatumiwa na Mungu kwa viwango vya juu kutimiza unabii ule tuliouona Kuhakikisha *YERUSALEM UNAWEKWA HURU KUTOKA KWA MAADUI ZAKE(WAPALESTINA)*

Hivyo kama Kanisa tuyaonapo haya hatunabudi *KUIOMBEA AMANI ISRAEL*,Kumuombea Mmarekani na wote wanaoisadia Israel katika Vita hii na maandamano haya yaliyokusudiwa kufanyika kwa muda mrefu na wakati endelevu kupingana na Israel.Huu ni wakati kila aliye Upande wa Mungu kuitakia heri Israel,Kuiombea Amani na ndipo tutakapofanikiwa kama Maandiko yasemavyo

*{ ZABURI 122:6}*
*_" Utakieni Yerusalem Amani(Pray for Peace for Jerusalem) na wote wanaipenda watafanikiwa"_*

Ndugu zangu kuna baraka tele tutazipata kama tukiombea sana Israel wakati huu kuliko wakati wowote ndipo tutakapofanikiwa,Vinginevyo tutakaribisha Laana juu ya Laana juu yetu au juu ya nchi zetu.Hivyo tuendelee kukemea kazi za Mpinga Kristo zinazoaanza kufanya kazi nyakati hizi kabla Kanisa halijanyakuliwa,Tuombe na tukemee kuwa mipango yote inayopangwa juu ya Israel isipate kufanikiwa bali tukaone kweli wakiumiliki Mji wao kama ilivyotabiriwa

‍♂Je umejifunza nini Mpaka hapo? *IKIWA UMEBARIKIWA NA SOMO HILI* basi usiache kushare kwa wengine nao wayafahamu haya kama ulivyofahamu wewe.Share facebook,Share Whatsap group na kwa marafiki zako wote au ndugu zako wote,Ili nae apokee maonyo haya ili yamkini asije akaingia katika mtego wa kuilaani Israel na zaidi asije akaishi tu bila kufanya maandalizi ya maisha na Yesu akarudi bila kumnyakua

Ikiwa hujaokolewa ila baada ya somo hili unahitaji kuokoka basi wasiliana nami kwa namba hapo chini nami nitakuombea upewe Uwezo wa kushinda dhambi na kuokoka ila ikiwa pia umebarikiwa au una swali au unahitaji ushauri pia usisite kuwasiliana nami kwa namba hzio hapo chini. *MUNGU AKUBARIKI*

* Na: Shujaa Charles Mwaisemba*
*0712-054498/0759-420202*
_stmwaisembac@gmail.com_
Siasa nyiiiiingi maneno mazito......alioooongea trump, kusema nautambua Jerusalem Kama mji mkuu Nini uzito wa neno Hilo....
 
Mahubili mazuri sana,, ila research more kuhusu hilo taifa..thread yako haijawa na evidence zakutosha zaidi ya mistari michache ya bible yakimapokeo na maneno mengi without facts, so namalizia kwa kusema bado hauna mashiko...kama sijakosea upo kwenye process za kutafuta waumini kwenye kanisa lako...good luck with that.
 
Ikiwa hujaokolewa ila baada ya somo hili unahitaji kuokoka basi wasiliana nami kwa namba hapo chini nami nitakuombea upewe Uwezo wa kushinda dhambi na kuokoka ila ikiwa pia umebarikiwa au una swali au unahitaji ushauri pia usisite kuwasiliana nami kwa namba hzio hapo chini. *MUNGU AKUBARIKI*

* Na: Shujaa Charles Mwaisemba*
*0712-054498/0759-420202*
_stmwaisembac@gmail.com_
siyo mahara pake kutafuta waumini wakukuchangia sadaka
 
Yesu asiporudi ndani ya miaka 500 ijayyo kwa mfano, It seems mtaanza kuichukia Israel nyinyi!
Maana uhusiano wenu na Israel siyo wa kiutu au kiundugu, bali mnataka kuitumia ili Yesu aje awanyakue!, lisipotokea hilo mtaitosa Israel nyinyi!.

Trump hawataki kwenye nchi yake, wewe unasema tumuunge mkono!. Kweli mtumwa ni mtumwa tu
 
MWAISEMBA CR labda nikuulize umejuaje kama hawa waisraeli waliorudi ndio waisraeli halisi ina maana yale makabila yaliyopotea mmeshayapata mpaka useme wamesharudi israel???

Swali jingine hao waliorudi 90% ni Ashkenazi mbao mpaka leo kuna mjadala kma ni waisraeli halisi au ni wayahudi kwa kubadilisha dini tu maana hakuna ushahidi kama ashkenazi wana damu ya yakobo zaidi ukisoma historia yao utagundua walitoka ukoo wa japhet je ina maana hili hulifahamu

3. Hivi utajuaje kama ni unabii wa Mungu umetimia sasa?? What if ni agenda ya PROJECT BLUE BEAM kutuaminisha unabii umetimia ili watuletee YESU FEKI mawinguni??? Maana sijaona makabila yale 10 yakirudi bado sijaona nabii aliyewarudisha zaidi ya mafreemason wachache kutoka uingereza..... Je tutafahamuje ni Unabii wa Mungu na sio kuna wajanja wachache wanacheza na maandiko ili kutuzuga unabii unatimia ili kuwapa Hawa Israel feki uhalali wa kuitawala PALESTINA

Embu tusaidie na haya maswali
 
  • Msingi wa dini ya kiyahudi unasemaje?
  • Uhusiano wa Uyahudi na Yesu (Ukristo) unasemaje?
  • Uhusiano wa Uyahudi na Uislamu unasemaje?
  • Wayahudi wanamwamini Yesu kama mwana wa Mungu?
  • Wayahudi wanamwamini Mohammad S.A.W kama mtume?.
 
Kama sikosei hapo instruction pekee ni ANSWER ALL QUESTIONS

Umetisha kama radi mkuu... Ngoja tusubiri majibu
 
Mahubili mazuri sana,, ila research more kuhusu hilo taifa..thread yako haijawa na evidence zakutosha zaidi ya mistari michache ya bible yakimapokeo na maneno mengi without facts, so namalizia kwa kusema bado hauna mashiko...kama sijakosea upo kwenye process za kutafuta waumini kwenye kanisa lako...good luck with that.
Umeniwahi mkuu
 
Evidence zipi unazotaka zaidi y ushahidi wa kihistoria na kimaandiko?
 
MFULULIZO WA MASOMO YANAYOHUSIANA NA KUTAMBULIWA KWA MJI WA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL

✳ SOMO 2⃣: UMOJA WA MATAIFA KULITAMBUA TAIFA LA ISRAEL KWA KURA✳

Na: Shujaa Charles Mwaisemba

▶KUREJESHWA TENA KWA TAIFA LA ISRAEL

▶KURA YA UMOJA WA MATAIFA JUU TAIFA LA ISRAEL
▶KURA YA BUNGE LA ISRAEL JUU YA JIJI LA YERUSALEMU

1⃣ UTANGULIZI

✍Kama tulivyokwisha kuona jinsi Taifa la Israel lilivyobomolewa kama Yesu alivyosema na Hekalu kubomolewa,Basi leo tena tunaendelea kuangalia mambo mengine kadhaa yaliyoendelea mpaka kupelekea Kurudi tena kwa Taifa la Israel kama Taifa kamili. Ikiwa hujapata somo la 1⃣ la mfululizo huu hakikisha unawasiliana nami ili kuweza kuendelea kuelewa mwendelezo wa matukio yaliyofuata.

*2⃣ KUREJESHWA TENA KWA TAIFA LA ISRAEL*

Kama tulivyotangulia kusema Mungu alikwisha sema kuwa Israel itatawanywa kona zote za dunia pale ilipomfanya Bwana Dhambi ndivyo hivyo hivyo Bwana ndiye aliyesema pia atalirudisha tena Taifa lake na kuwa Taifa kamili kwa wakati wake.

Hivyo tuliona jinsi Israel walivyofukuzwa na Kwenda kila kona na wakazaliana sana vizazi kwa vizazi vilipita lakini Mungu aliposema atawatawanya alitoa ahadi kuwa Siku za mwisho zitakuja ambayo atawakusanya tena na kurudisha katika nchi yao

*♨{EZEKIELI 36:24}*
_"Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami *nitawakusanya* na kuwatoa katika nchi zote, na *kuwarudisha* katika nchi yenu wenyewe."_

Na moja kati ya kiashiria kimoja kikubwa cha siku za mwisho ni Kurudi kwa Taifa la Israel kwa Muujiza Mkubwa,Jambo lililoshangaza dunia.

Mwishoni mwa karne ya 19 kulitokea jambo la ajabu miongoni wa Wayahudi walikuwa wametawanyika duniani kote, ingawa hawakuwa na na mawasiliano kati yao lakini roho fulani ikamwagwa juu yao
Ingawa walikuwa duniani kote lakini utamaduni wao haukubadilika.Wazazi walikuwa wanawahadithia watoto wao na watoto wao wanawahadithia watoto wao toka kizazi kimoja mpaka kingine juu ya ahadi ya Mungu ya kuwarejesha na kuwapa Kaanani kuimiliki

*♨{ ZABURI 78:1-11}*
_"............................Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu, Ambayo baba zetu walituambia.Hayo hatutawaficha wana wao, Huku *tukiwaambia kizazi kingine, Sifa za BWANA, na nguvu zake, Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya*.Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo, Na sheria aliiweka katika Israeli. Aliyowaamuru baba zetu Wawajulishe wana wao,............................Ili kizazi kingine wawe na habari, Ndio hao wana watakaozaliwa. Wasimame na kuwaambia wana wao.............................Naam, wasiwe kama baba zao, Kizazi cha ukaidi na uasi. Kizazi kisichojitengeneza moyo, Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.................."_

Hivyo kwa muda wote waliokaa pande zote watoto walikuwa wamewafundishwa na kukumbushwa juu ya ahadi za Bwana.
Walikuwa wakiteswa na kuuliwa sana wakiwa nchi za jirani pande zote za dunia lakini bado walijua watarudi kwenye nchi yao.
Mwishoni mwa karne ya 19,baada ya miaka karibu 1800 Yerusalemu ilipobomolewa,Ndipo ilipomwagwa roho juu ya wana Israel(Wayahudi) wote kutoka pande zote walipo kila mmoja wakaaanza kupata mawazo ya kubuni na namna ya kurudi bila mawasiliano na wale wa upande mwingine

Kulitokea kitu kinachoitwa *ZIONIST MOVEMENT* juu ya wayahudi ambacho ndicho kilianza kuhamasisha wayahudi kurudi tena kwenye nchi yao na kuyachukia makazi waliyokuwa waishi katika pande zote za dunia bali wakaanza kurudi kwa Kasi kubwa sana

*3⃣ KURA YA UMOJA WA MATAIFA JUU YA TAIFA LA ISRAEL*

✍ Vuguvugu la hilo la wanaisrael lilipoendelea kwa nguvu kurudi kwenye Nchi yao ambayo wakati huo ilikuwa chini ya utawala wa waingeleza,Mwaka 1947 ndipo Umoja wa mataifa ilipigwa kura ambayo ndiyo ilikuwa mwanzo wa Taifa la Israel kutambulika mwakani baadae

✍Tarehe 29 Nov 1947 ndipo kulifanyika kura katika UMOJA WA MATAIFA ambao ulijadili juu ya makazi hayo ya Eneo hilo la Israel ambalo yalikuja na kufanya Mwaka uliofuata Taifa la Israel kuja kuwa Taifa Kamili

✍ Tarehe 14 May 1948 ndipo Israel wakatangaza kuwa ni Taifa na Kuitwa tena *TAIFA LA ISRAEL* kama lilivyokuwa mwanzo baada ya miaka 1800 toka mwaka 135 B.K

✍Jambo hili la Taifa la Israel kutangazwa kuwa kama Taifa halikukubalika na mataifa mengi ya wakati huokama ilivyolewa wanavyopinga haya Lakini siku ile ile 14/5/194 walivyotangazwa kama Taifa,Rais wa Taifa la Marekani wakati huo, *RAIS HARRY TRUMAN* ndiye aliyekuwa Rais wa kwanza nae kusimama kusema analitambua Taifa la Israel

✍Ingawa nchi nyingi hazikukubaliana na kuafikiana na Rais huyo wa Marekani kwa Uamuzi alioufanya wa kuitambua Israel kama Taifa Lakini Israel wakapata Nguvu sana,Na baadae mataifa mengi nayo yakaanza kuwatambua kama Taifa Kamili.

*4⃣ KURA YA BUNGE LA ISRAEL JUU YA JIJI LA YERUSALEM*

Lakini Mwaka 1950,Kumbuka wamekwend katika nchi mbalimbali duniani na hivyo wamerudi wakiwa na Mfumo wa Kidemocrasia wameuleta sasa katika nchi yao ya Israel.Hivyo mara baada ya Taifa lao kutambuliwa ndipo walipoweka mfumo wa kiserikali ambao ulikuwa na Bunge ambalo linaitwa *KNESSET*

Kwa mara ya kwanza Bunge la Israel 23 January 1950 likatangaza tena bungeni baada ya kuwa wamepiga kura katika bunge lao na kura 62 kwa 2 (Matokeo ya kura za bunge la Israel)Wakakubaliana katika Bunge hilo kwa kura hizo kuanzia Tarehe hiyo Kwamba *YERUSALEM NDIO UTAKUWA MJI WAO MKUU WA ISRAEL*

Katika maazimio hayo wakasema itakuwa ni Yerusalemu isiyoweza Kugawanyika yaani Yerusalem nzima katika eneo lake lote ambayo inatajwa katika mipaka ya Yerusalemu kama ilivyo katika Maandiko
Swala hili pia lilipingwa vikali sana na mataifa mengi kwamba Yerusalem kuwa mji mkuu wa Israel tangu wakati ule.Wakati huo Israel walikuwa sehemu kubwa wapo katika Yerusalemu Magharibu na huku Yerusalemu Mashariki walikuwa wanakaa waarabu wa Aina mbalimbali

Usikose kufuatilia Somo la 3⃣ la mfululizo huu ambapo utajifunza mambo mengine mengi kuhusu vita vilivyofuata baadae vya israel na mataif yote ya waarabu na jinsi Marekani walivyopiga kura ya kuitambua Yerusalem.Kwa leo tuishie hapa

Ila Kuna mambo nataka tujifunze na tutafakari tunapohitimisha somo hili,Kwanza tumeona kumbe tangu Mwanzo kama ilivyo leo maamuzi yote yaliyokuwa Yanafanywa yalikuwa yanaonekana yanapigwa kwa nguvu na mataifa mengi lakini kwakuwa ni wakati wa Bwana hivyo kupinga kwao hakukuzuia Taifa la Israel kuanzishwa na kurudishwa kama Neno la Bwana linavyosema

Pia kwako wewe unayesoma Ujumbe huu,Mungu anataka akuambie kuwa Kama aliweza kuwatawanya Israel na sasa akawarudisha Na kuwa kama taifa na kuwapenda kama mwanzo,Basi hata wewe Mungu anakupenda anataka kukurudisha katika Imani majira haya ya mwisho mwisho wa dunia.

Yamkini ulikuwa unampenda san Mungu hapo mwanzo ila sasa Umerudi Nyuma,Umechoka,Unafanya mambo ya kidunia na kuishi maisha ya Uchafu kama mataifa,Huu ni wakati wa Bwana wa kuwarudisha tena walio wake Kabla Kristo Yesu hajarudi!Unaposoma Ujumbe huu Ikiwa ulirudi Nyuma na Kuacha wokovu au unaishi maisha ya Uvuguvugu,Nasema Na wewe kuwa *RUDI KWA BWANA,RUDI KWA BWANA,RUDI KWA BWANA*.Mungu bado anarehema na anakupenda ndio maaana kalileta somo hili kwako

Na Ikiwa Wewe unajifahamu hujaokoka,Huna uwezo wa kushinda dhambi,Unajitahidi kuacha dhambi fulani lakini unajikuta unarudi pale pale!Ni wakati wa kumaliza vizuri,Mungu anaangalia sana Umaliziaji wa mtu si uaanzaji!Ni kweli ulianza vibaya,ni kweli umefanya dhambi nyingi wewe unazijua lakini ikiwa utakubali Kutubu dhambi zako ,Mungu hatakumbuka dhambi zako zote ulizotenda,.Hata kama uliua au umefanya uasherati ana uzinzi sana,Hata kama ulitoa mimba n.k,Mungu atakupokea kama alivyowapokea Taifa la Israel

Hivyo ikiwa unahitaji msaada wowote wa kirohi kama Kukuombea upewe uwezo wa kushinda dhambi basi wasiliana na mimi kwa namba hiyo hapo chini,Nami nitakuombea na ikiwa umerudi nyuma au unatamani kuishi maisha ya kumpendeza Mungu ila unajikuta unaanguka anguka basi pia wasiliana na mimi nitakushauri na kukuombea pia ili tumalize Safari hii pamoja!!

*MUNGU AKUBARIKI SANA*

Kwa mawasiliano Zaidi
* Na:Shujaa Charles Mwaisemba*
*0712054498/0759420202*
_stmwaisembac@gmail.com_
 
MFULULIZO WA MASOMO YANAYOHUSIANA NA KUTAMBULIWA KWA MJI WA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL

✳ SOMO 2⃣: UMOJA WA MATAIFA KULITAMBUA TAIFA LA ISRAEL KWA KURA✳

Na: Shujaa Charles Mwaisemba

KUREJESHWA TENA KWA TAIFA LA ISRAEL

* MFULULIZO WA MASOMO YANAYOHUSIANA NA KUTAMBULIWA KWA MJI WA YERUSALEMU KAMA MAKAO MAKUU YA ISRAEL

*✳ SOMO 3⃣ : MAREKANI KUPITISHA SHERIA YA KUITAMBUA YERUSALEMU✳*

* Na: Shujaa Charles Mwaisemba*

*VITA YA ISRAEL KUTEKA YERUSALEMU MASHARIKI*
*BUNGE LA MAREKANI KUPITISHA SHERIA YA KUITAMBUA YERUSALEMU*
*UTOFAUTI WA TRUMP NA MARAIS WA MAREKANI WALIOMTANGULIA*

*1⃣ UTANGULIZI*

Kama tulivyokwisha kuona katika somo lililotangulia jinsi Bunge la Israel lilivyopitisha sheria juu ya Jiji laYerusalemu kuwa ndio makao yao makuu na kudai Yerusalemu Yote isiyoweza kugawanyika yaani Yerusalem mashariki na Yerusalemu Magharibi.Leo tutaendelea kutokea hapo ikiwa hukuweza kufuatilia mfululizo uliopita ili kuweza kuelewa zaidi yaliyo mbele yetu basi utawasiliana nami kwa Namba hapo chini ili nikupatie mfululizo uliopita.

*2⃣ VITA YA ISRAEL KUTEKA YERUSALEMU MASHARIKI*

Mara baada ya ile sheria kupitishwa kwenye bunge la Israel kulianza kufanyika jitihada nyingi za kuanza kutaka kurudisha Baadhi ya maeneo yao ambayo tulieleza yalikuwa yanakaliwa na Waarabu wapalestina na wengineo hasa Yerusalemu Mashariki

Lakini ilipofika mwaka 1967 Kulitokea vita vikali ambavyo ni vya siku 6 tu ambapo Israel ilipambana na waarabu combine (Palestina,Syria,Urusi n.k) ambao wameizunguka pande zote ila kwa ajabu sana Kataifa hako Kadogo kamoja kaliwapiga vikali na kuwasambaratisha vikali na wakateka Yerusalemu Mashariki pia ikawa mikononi mwao

Hivyo sasa wao wakahesabu Yerusalemu yote sasa ni kwao yaani Yerusalemu Magharibi na Yerusalemu Mashariki,Lakini dunia karibu yote ikawa inawahesabu kama wavamizi na miaka yote hiyo kumekuwepo na ushindani mkubwa katika eneo hilo na ndio chanzo cha Mgogoro huu Mkubwa kati ya Palestina na Israel.

Wapalestina wakidai Eneo lao na waisrael wakidai ni Eneo lao(Nitaeleza kwa Kina kwenye Somo jingine *NANI NI MMILIKI HALALI WA ENEO HILO?KATI YA PALESTINA NA ISRAEL❓*).Ila kwa ufupi kama Wanafunzi wa Biblia hatuna budi kuele
wa *WAPALESTINA NI AKINA NANI❓*

WAPALESTINA ni Wafilisti Kibiblia(Philistine)!Maanake wale wakina Goriathi wale ndio wapalestina wenyewe.Wale hawajawai kuwa Israel.Ukiangalia Biblia yako huwaoni wakina Goliathi kama wamiliki halali wa Israel(Haikuwa nchi yao).Kwahiyo tangu wakati ule ilikuwa ni shida sana baina ya waisrali na wapalestina

*3⃣ BUNGE LA MAREKANI KUPITISHA SHERIA YA KUITAMBUA YERUSALEMU*

Baada ya Muda mrefu na Mgogoro huu wa Wapalestina na Israel kuzidi kuwa gumzo kwa ulimwengu wote juu ya umiliki wa Ardhi na hasa jijila Yerusalem.Taifa kama La marekani limemekuwa likikaa chini kujadili na kutafuta kwa kusoma vitabu historia juu ya jiji la Yerusalem na nchi hii kwa mipaka yake na Kugundua kuwa Yerusalemu ni Mji wa Israel tangu awali ulikuwa ukijulikana kama *MJI WA DAUDI 2 SAMWELI 5:4-9*

Hivyo ilipofika Mwaka 1995,Bunge la Marekani likaleta hoja hii bungeni na kuijadili kisheria Ikiwa kama Yerusalemu ni makao makuu ya israel au la❓Lakini baada ya mjadala huo wote,Bunge lote la marekani lifikia kufanya azimio la pamoja kwa kupitisha sheria ya Kuitambua *YERUSALEMU KAMA MJI MKUU WA ISRAEL* kw sheria kwa kura nyingi sana za bunge

Lakini pamoja na Kupitishwakwa sheria hiyo tangu mwaka 1995,ila utelelezaji wakendio ulikuwa ni shida sana kwasababu ulikuwa na vitisho vya kila namna kutoka kila kona kila mahali kwamba Marekani wakitangaza tu rasmi kwamba wanaitambua Yerusalemu kama Makao makuu ya Israel basi itapelekea machafuko makubwa sana duniani .Kumbuka Marekani walipitisha Sheria kuwa Yerusalemu ni Mji usiogawanyika yaani Yerusalem Masharikona Yerusalemu Magharibi zote ni Yerusalem iliyo chini ya Israel)

Ukizingatia Ndani ya Yerusalemu Masshariki ndio kuna Msikiti mkubwa unaoitwa *MSIKITI WA ALAQSA(DOME OF THE ROCK)* mahali ambapo waislamu wote kote duniani wanapahesabu kama sehemu pa 2 pa utakatifu baada ya Macca

Kwahiyo ilikuwa ni mgogoro mkubwa kwa marekani kutangaza hiyo juu ya sheria waliyoipitisha.Bunge lote la Marekani wamekuwa wakitamani hivyo kwa miaka tangu wakati huo kuona utekelezaji wa Sheria hiyo ya kuitambua Yerusalemu kama Mji mkuu wa israel ukitimizwa na maraisa waliokuwa wakiingia madarakani

Marais wote waliokuwepo tangu wakati uke,Walikuwa wanapigia debe ahadi hiyo kuitekeleza lakini,Nani mwenye ubavu wa kutangaza hivyo❓ Kwa kuwaza chuki atakayoipata dunia yote,kwasababu kila kilichokuwa kinagusiwa ilionyesha ilikuwa ni hali tete

Kwahiyo Marais tangu nyakati zile za kina *Bill Clinton, George W Bush, Barack Obama* wote hawa utaona ukiingia Youtube,utaona hotuba zao za za kampeni zote walikuwa hasa wanasisitiza kuwa wataitambua Yerusalemu kama Makao Makuu ya Israel.Walitamka hivyo marais hao wote niliowataja ili kupata kura za wengi katika Maeneo yale ya waktisto wengi marekani ambapo wengi ni Wapentekoste ,lakini utekelezaji wake ndio ulikuwa mgumu

Kwahiyo walikuwa wanahairisha utekelezaji wake kila baada ya miezi 6,Na wamekuwa wakifanya hivyo tangu wakati ule

*4⃣ UTOFAUTI WA DONALD TRUMP NA MARAIS WALIOMTANGULIA*

* AHADI YA TRUMP YA UTEKELZAJI WA SHERIA ILE KWA WAMAREKANI NA WAYAHUDI*

Rais wa Marekani, *Donald Trump* tangu awali katika Kampeni zake zote vile vile akaahidi kwa uzito mkubwa na nguvu kubwa akasema Sasa hilo ambalo limewashinda wengine wote,Yeye atalifanya na hatajali Ushindani wowote utakalojitokeza,Akazidi kuwahakikishia Israel kwamba hilo atalifanya bila uoga wowote

* HESHIMA YA WAYAHUDI NCHINI MAREKANI KWA AHADI HIYO*

Kwa Muda mrefu wayahudi waliopo nchi marekani wamekuwa wakiheshimika sana sana hivyo ahadi ile ilikuwa pia inawalenga wayahudi wote waliopo Nchini marekani.Kwahiyo israel wote wakawa wanasubiri alivyoingia Trump madarakani mwanzoni mwa mwaka 2017 Kama sheria ilivyo ikifika miezi 6 inabidi tena kuhaitisha utekelezaji wake (mpaka wakati huo msimamo wa bunge ulikuwa nu ule ule)Kwasababu ukipinga tu msimamo wa Bunge itakuwa vigumu kupata kura kwa Wakristo wa wamarekani

Kumbuka Marekani kuna wayahudi wengi sana na wayahudi kwa watu wanaowafahamu kuwa kote duniani ni watu wenye akili kupindukia,Ni watu ambao wamebarikiwa kwa ajabu sana.
▶Wanasayansi wengi wakubwa unaowasikia wamefanya mambo ya uvumbuzi wa vitu vingi huko marekani ni Waisrael.
▶Madakrari bingwa wakubwa sana na maalumu hi waIsrael
▶Watu wengi kwenye fani nyingi marekani ni wanaisrael
Kwahiyo ni watu wanaoheshimika sana sio tu Maraekani bali nchi nyingi sana kama sweden Kwa mfano wametengewa sehemu au eneo maalum kwa waisrael pekee na kupewa mazingifa mazuri kuliko hata raia wenyewe kwasababu ya uwezo wao na akili zao za ubunifu ambayo huwezi kuyaona kwa mtu mwingine wa kawaida kuweza kuyabuni kwa jinsi ambavyo wamebarikiwa na Mungu n.k.Wamepewa ulinzi kwa namna isiyo ya kawaida kwa mataifa mengi hata kule ulaya

Kwahiyo Bunge la marekani likikuwa haliwezi pia kusimama kinyume na Israel kwa gharama yoyote ila tatizo ndio ilikuwa ni nani atangaze?Kwasababu kutangaza hivyo ni kama Kutangaza vita duniani kote

Hivyo hata kwa Trump alivyoingia kukawa na uzito fulani ingawa alikjwa amedhamiria tangu mwanzo lakini hivyo hivyo kutoka kila kona,kila mahali wakamwambia tu ukithubutu kufanya hivyo utakuwa umetangaza machafuko katika dunia yote.Na ilivyopita miezi 6 nae vile vile akahairisha utekelezaji wake ile sheria ya mwaka 1995 mara ya kwanza

Lakini hatimaye ndiye alikuwa Rais wa Kwanza na wakipekee kuweza kutangaza jambo hilo ambalo lilisisimua duni.Usikose kufuatilia somo linalofuata Ambalo nitakueleza nini kilifanyika kabla ya kutangaza huku alikokufanya na kilichompa nguvu zaidi ya kutangaza tofauti na Marais wenzake wote waliopita❓ Usikose kufuatilia Sehemu ijayo ya mfululizo huu ambapo pia nitakueleza Maana ya70 Kibiblia inavyohusishwa na nyakati za Mwisho

Nashukuru kwa kufuatilia mpaka hapo,Unaweza kushare ujumbe huu kwa magroup mengine na watu wengine.ila Pia ikiwa unahitaji ushauri!una maswali Au unahitaji Kuokoka kutokana na Haya uliyoyafuatilia na unaamua Kutaka kuacha dhambi.Basi wasiliana nami kwa namba hizo hapo chini nami nitakuombe utaoewa uwezo wa kushinda Dhambi

*MUNGU AKUBARIKI*

♨Kwa mawasiliano zaidi
* Na:Shujaa Charles Mwaisemba*
*0712054498/0759420202*
_stmwaisembac@gmail.com_
 
Kama sikosei hapo instruction pekee ni ANSWER ALL QUESTIONS

Umetisha kama radi mkuu... Ngoja tusubiri majibu
Akiyajibu nitarudi kumsikiliza!.
Natumai roho ya unayemuamini itakusaidia kuyajibu hayo maswali yangu MWAISEMBA CR lest assure ukishindwa nijibu basi wewe na huyo unayemuamini ni UONGO!.
 
Back
Top Bottom