Juan Guaido wa Venezuela kufungwa miaka 30 jela

Hii kitu nilimuelewa mpaka nikajishangaa mkuu, aiseee
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Given the current situation; that is easier said than done.
Huyo anajiandalia mazingira ya kuwa mkimbizi wa kisiasa!! Sitashangaa akiibukia kwenye ubalozi wa Taifa lolote la Magharibi linalomuunga mkono akiomba ukimbizi! Huyu ni msaliti sijapata kuona!! Yuko Tayari kukaribisha Taifa lenye lengo la kupora mafuta yao!
 
Vitimbwi vyote vya marekani kuhusu Venezuela vimekufa kifo cha Mende!! Ndio maana siku hizi hutawasikia tena wanazungumzia suala hilo kwa nguvu!! Hata vyombo vya magharibi kama BBc vimekaa kimya kwa aibu baada ya juhudi kubwa za marekani na uingereza kutaka kuingnguvuiza "misaada" Venezuela kwa nguvu kushindikana!! Propaganda za kutaka jeshi liasi zimeshindikana!!
 
Siyo mpole, anajua akifanya ujinga tu kule Washington watapata kisingizio kizuri cha kumvamia. Tena watamtwanga hataamini, maana sidhani kama kuna nchi inaweza ikashindana na Marekani kule Amerika Kusini halafu ikabaki salama.
Wamarekani ninaowajua...kama hawaoni hatari yoyote ya kuvamia...hawasubiri cha sababu. Kuna uwezekano mipini iliyowekwa na Russia na China kidiplomasia na kiusalama..bado inamtatiza. Ebu fikiria, US aingie kichwa kichwa pale Caracas...halafu atolewe nishai kama pale Damascus aibu wataiweka wapi...na hapo ndiyo itakuwa fursa ya nchi hizo za Amerika ya Kusini zitamgeuka US mara moja na kujitangazia uhuru kamili!!!(Nawaza)
 
Mkuu si umesema kule Amerika ya kusini(AK) US anawashirika wengi...sas wasi wasi wake nini ukanda kuchafuka wakati yeye ana wafuasi wengi!?
Nadhani kuna vitu vya muhimu sana ambavyo lazima tuviweke sawa hapa. Mosi, International Order is interconnected and affected by great power politics. Hakuna kitu kitakochofanywa na taifa kubwa halafu kisiwe na madhara kwa jumuiya ya kimataifa, iwe kisheria, iwe kiuchumi au kisiasa: Venezuela ni dhahiri kabisa hawezi kupigana na Marekani hata kama Urusi na Uchina wako pale.

Historia inatufundisha hivyo, na tunafahamu kwamba tukiitoa CUBA, Marekani amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuwashinda wakomunisti walipojaribu kupeleka ushawishi wao kule Amerika Kusini. CUBA alipona kwasababu ya makubaliano baina ya Krushchev na Kennedy kwamba isitishiwe tena kijeshi na uhuru wake uheshimike.

Sasa Marekani hata kama ana uwezo wa kuvamia kijeshi na kumwondoa Maduro lazima ifikirie mbele kwamba nini kitatokea Venezuela baada ya Maduro, na madhara yake kwenye siasa za kimataifa. Vivyo hivyo nikasema leo hata Urusi ana uwezo mkubwa sana wa kumtwanga Ukraine, Poland, Latvia na Lithuania ndani ya masaa tu, lakini unadhani kutakuwa hakuna madhara yoyote yale kwenye siasa za dunia ??

Pili, kuna jambo moja muhimu sana analolisemaga Prof John Mearshimer kwamba "History is never linear". Kuna mambo mengi yanaweza kutokea hapo katikati ambayo hata mataifa makubwa hayakutarajia kuyaona. Marekani amejifunza Afghanistani, Iraq, Libya na Syria kwamba kuvamia nchi na kupindua uongozi ni kitu kingine na kutengeneza mfumo mpya ni kitu kingine kabisa (Tena hichi cha pili ndicho kigumu kuliko vyote).

Tatu, anachokifanya Vladmir Putin pale Venezuela ni kilekile ambacho alikifanya Krushchev miaka ya 50 baada ya Marekani kuweka makombora ya Jupiter na Thor kule Uturuki kwenye mpaka wa Urusi ya Kisovieti. Nikita Kruschev alisema hivi "I will show Americans how it feels to have weapons of mass destruction placed on your door step" akapeleka makombora kule CUBA. Lakini ukweli ambao ni mchungu ni huu, Urusi mbali na CUBA na Bolivia unadhani anaweza kupambana na Marekani kirahisi rahisi tu ?
Mfano wako wa Syria ni dhahiri kabisa, lakini kuna kitu cha muhimu umekisahau kabisa: Umoja ambao ulikuwa unapingana na Assad na Urusi ulikuwa umevunjika wenyewe tokea mwanzo.

Waandishi wakubwa wa siasa za Mashariki ya Kati kama Sharmine Narwani wanasema hivi: Washikrika wakuu wanaompinga Assad walikuwa hawazungumzi lugha moja. Qatar alikuwa anazungumza lugha moja na Uturuki, lakini amegombana na Saudi Arabia na Marekani. Uturuki anampinga Assad lakini Marekani anawaunga mkono Wakurdi ambao ni adui wa Uturuki. Saudi Arabia na Qatar walikuwa hawaelewani kabisa, huku Marekani akitaka kumuua Raisi wa Uturuki" Leo hii Marekani amesema anaunda kikosi kipya chenye wapiganaji kama 30000 ili kumpiga Assad lakini Uturuki kasema atawatandika kwasababu ni magaidi. Upande mwingine Qatar na Iran wanaanza kuzungumza lugha moja.

Maswali:
  1. Hivi unadhani Uturuki angekuwa upande wa Marekani tokea mwanzo unahisi Urusi angefurukuta kirahisi ?? Kwanza kupita pale kwenye The Bosphorous kuelekea Meditteranean Sea ingekuwa ni rahisi ?? Hii ni moja ya sababu mpaka leo Uturuki amekataa kusaini ule mkataba uitwao The United Nations Convention on the law of the Sea of 1982.
  2. Kupambana na waasi ilikuwa ni lazima ndege za Urusi zitumie anga la Uturuki. Uturuki alivyotungua ndege ya Urusi mambo yalikuwa siyo mambo na Putin alichukia sana. Lakini unadhani kwanini Putin aliamua kumuokoa Erdogan asife wakati CIA walipotaka kumfanyizia ??(Putin alitumia huu mwanya kuendelea kuwagawanya)
  3. Unadhani kwanini Marekani ilifika mbali sana na kuamua kumpindua Erdogan ?? Unadhani utawala ambao ungewekwa baada ya Erdogan ungekuwa ni rafiki kwa Urusi, Iran na Syria ?? Unadhani Urusi angeendelea kutumia anga la Uturuki ??
  4. Turudi kule Amerika Kusini: Unadhani kuna nchi ya Amerika Kusini ambayo inaweza kumsumbua au kumpinga Marekani akisema chochote dhidi ya Venezuela ukiwatoa CUBA na Bolivia ?? Unadhani Urusi atakuwa na nguvu ile ile aliyonayo kule Ulaya Mashariki na Mashariki ya Kati ??
Hebu tujadili.....
 
Ngoja niseme tu kuwa Malcom Lumumba upo juu sana siasa za kimaifa, yaani navutiwa kusoma michango yako, ila za huku kwa jiwe vepeee!?
 
Nikitoka villa park nitakuja kubisha

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Sasa mjadala utoke wap tena aliyakuwa umeeleza vizuri na kwa fact lkn pale kwa China siwezi kukubari aise japo najua atashinda lakini kwa mbinde saana
Kama unataka kubishana nenda kwenye vijiwe vya kahawa, lakini kama unataka mjadala nakukaribisha kwa mikono miwili.

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Asante sana mkuu kwa bandiko lako hili. Niwie radhi kwa kuchelewa kujibu hoja zako kimjadala kama ulivyozianisha kwenye bandiko. Hoja zako nimekubaliana nazo; zile ambazo nimezitazama kiutofauti nimezipa herufi kuanzia (a) mpaka (f) kwenye nukuu na utofauti huo nimeueleza hapa chini. Pia maswali yako nimeyajibu kwa mtirirko ule ule ulioutoa.
Karibu .
---
(a) Nikirejea maandamano ya juzi kati mpakani mwa Colombia na Venezuela pale darajani...'proxy wa US' walidhibitiwa na Polisi na wananchi wa Venezuela. Nawaita proxy lakini kiukweli mizigo ya USAID hisingefika pale mpakani bila usindikizwaji wa 'contractors' waliopata mafunzo kwenye ardhi na majeshi ya Marekani. Indirectly, Venezuela amejaribu kupambana na US na kwa matokeo ya awali, Maduro anaongoza dhidi ya Trump na washirika wake.

(b) Marekani hii ambayo imevunja JCOPA (Joint Comprehensive Plan of Action )ya Iran katika P5+1, pia US hii ambayo imevunja mkataba wa kutengeneza makombora ya masafa marefu na Russia, nakadhalika tena ikitamba kuwa yenyewe ni "exceptional country" unatarajia iheshimu mikataba baina ya nchi mbili bila kuwa na sababu zinazoiogopesha? Unaweza kuuliza mbona sasa US kavunja hiyo mikataba na Russia huyo huyo anayemlinda Cuba. Jibu ni kuwa US anavunja mikataba ambayo haimletei madhara. Kavunja huo wa Makombora kwa sababu anajua 'doctrine ya ulinzi ya Russia' inasema Russia itatengeneza silaha za kujilinda na 'kujibu' mashambulizi. Mkuu unadhani ni kwa nini, US anahangaika na North Korea? Ni kwa sababu NK katangaza atashambulia, hata subiri kushambuliwa. Nadhani tupo wote hapa. Nakuhakikishia US akijiridhisha kuwa hakutakuwa na madhara anaweza kuivamia Cuba muda wowote.

(c) Lakini kwa ufuatiliaji wangu mdogo wa masuala haya ya historia ya ulimwengu naweza kuboresha theory ya Prof. John kwa kusema " History is never linear nor non-linear but generic". Ndiyo.Hata Tanzania tunaweza ku'generate' historia ya kushangaza ulimwengu; trust me.

(d) Mimi nadhani US kajifunza nchini Syria tu kuwa hawa Russia na washirika wake siyo wale wa mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzo mwa 1990 (ka'prove' theory yangu hapo juu (c); ha ha aaa). Hata hivyo, ni kueleze kuwa US ananufaika sana na 'kutotengenezeka mfumo madhubuti wa kusimamia serikali anazoziangusha'...Na kuhakikishia. US anafanya yote haya kwa nchi alizozivamia na washirika wake ili ziendelee kuwa 'volatile' kwa minajiri ya kubakiza majeshi yake pale kurahisisha uporaji wa rasilimali za nchi husika wakati huo huo akirahisisha mikakati yake ya 'kumonitor' nchi anazotilia mashaka kupinga interests zake. Mkuu zichunguze nchi zote alizovamia na tazama majirani wa nchi hizo na uhusiano wao na US (Ni mawazo yangu haya yanaweza kupingwa).

(e) Na ukweli mchungu wa ninachokiamini ni hiki...anaweza kupambana naye kirahisi (60%) ila si kirahisi rahisi (100%) kama ulivyosema. Sababu, ni kuwa siku za nyuma kidogo ilijulikana kuwa nchi yenye uchumi mkubwa na jeshi kubwa lenye vifaa vingi vya kijeshi ndiyo pekee inaweza kuamua hatima ya ushindi wa vita; lakini kwa dunia ya leo; vita vinaamliwa na ubora wa teknolojia ya silaha za kijeshi(siyo wingi wa vifaa), wingi wa wanajeshi 'intellect' wa nchi husika katika medani ya vita, ujasiri na ari ya wanajeshi wa nchi husika, na ubora wa ukusanyaji wa taarifa muhimu za kiintelijensia na ki'usalama' (Zinaweza kuwepo factors nyingine lakini ninazozijua ni hizi); Katika hivi nilivyotaja Marekani kaachwa mbali na Russia. Tena kwenye ukusanyaji taarifa za kiintelijensia Russia yuko mbali mno...na hii ndiyo inampa 'upper hand' kwenye maamuzi yake mengi kiasi cha kushangaza. Issue ya Erdogan haikuwa ya kawaida (Waasi wote wa Erdogan walikusanywa kama kuku aliyepigwa na 'mdondo')!!!

(f) Hii inaweza kuwa sahihi kabisa, ila ukiliangalia kwa mapana yake unaweza ukagundua kuwa ni 'tricks' zile zile za US kupenda 'volatile environment' kama nilivyoeleza hapo juu kwenye (d). Hii inamsaidia kuwa na uwezo wa kuwachezea anavyotaka washirika wake. Pia US anajua hawa waarab wakiongea 'lugha' moja wanaweza kumsumbua kwenye kupitisha maamuzi yake kwenye vikao vyake na wao. Hivyo, katika hili si shangai.
===
Maswali uliyoweka: Majibu yangu ni kama ifuatavyo:-
  1. Mkuu, Uturuki na US walikuwa wamoja mwanzoni kabisa mwa mgogoro wa Syria, ndiyo maana mafuta yaliyokuwa yanaibwa Syria na IS yalikuwa yanasafirishwa kwenda Uturuki huku US 'akitazama kwa jicho la karibu' (Unamkumbuka the late Mc Cain wa US). Russia alikuwa tayari ana bases zake pale Syria mashariki mwa bahari ya Mediterranean; pia Russia alikuwa na usafiri wa haraka wa kusafirisha mizigo yake kupitia 'njia za panya- Caspian sea, Iran, kaskazini mwa Iraq na kutua Syria' hasa kwa kutumia ndege kubwa ambazo hazihitaji 'water body' ya Turkey.
  2. Hii ni kweli, hasa baada ya Iran kuwakatalia Russia wasitumie ardhi yao kurusha makombora nadhani dhidi ya IS. Iran ilichukia kutokana na vyombo vya habari vya Russia kuonyesha kuwa sasa Russia ina'influence' kubwa huko Iran baada ya Russia kuruhusiwa kutumia ardhi ya Iran.
  3. Erdogan, ahaminiki kwao (NATO) na ni US aliyewashinikiza EU wamnyime uanachama wa EU Turkey; jambo hilo lililomkasirisha sana Edorgan (akaona anadharauliwa) na Ergogan akaona Russia hawamnyanyapai ingawa walikwamisha juhudi zake za kufufua Ottoman Empire. Ukweli ni kuwa Mapinduzi yale yangekuwa ya umwagaji damu mkubwa sana; na utawala ule ungeedelea kuwepo kwa nguvu za NATO. Na sote tunajua Nato (actually US) hana urafiki kwa Urusi, Iran wala Syria. Urusi angeendelea kutumia njia ya panya (rejea jibu namba moja) ambayo ingemgharimu sana...labda angelazimika kutumia manoari zake pale Caspian sea...na risk ya makombora kuwa 'astray' kumpiga asiyetakiwa ingekuwa kubwa sana, ingawa wana mfumo wao mzuri wa GLONASS. Ukweli hali ingekuwa ngumu kidogo ingawa alikuwa na washirika Hesbollah (Lebanon), na Iran na wasyria wenyewe.
  4. Pia Peru anaweza kumpinga US; nimeshuhudia mara kadhaa msimamo wa Peru dhidi ya drafts za Marekani katika mijadala ya UNSC ingawa kidiplomasia zaidi. Nguvu ya Russia kwa sasa inabebwa na factors nilizotaja kwenye kujibu hoja yako niliyoipa namba (e) hapo juu (kama lakini unakubaliana nazo). Nguvu hizi za Russia zinatosha kumzuia US pakubwa sana.
----
Nadhani nimejadili vya kutosha. Mkuu, pamoja na wanaJF wengine nina imani mtakuwa na la kuhoji, kuongeza na kadhalika katika kuboresha mjadala huu. Asanteni sana.
 
Still, Bolton told Tapper that the US is not afraid to go it alone. “In this administration we’re not afraid to use the phrase ‘Monroe Doctrine,’” he said. “This is a country in our hemisphere and it’s been the objective of American presidents going back to Ronald Reagan to have a completely Democratic hemisphere.”

US wants ‘broad’ regime-change coalition on Venezuela – Bolton
===
Hizi imani zao, Wamarekaniz zitawaponza. Kwa dunia ya sasa sidhani kama US inamtaji wa kusimamia 'doctrine' hii sawa sawa huko Amerika ya Kusini. Ukizingatia China anavyoinuka, hata hivyo hiyo doctrine iliwalenga Ulaya na si Asia (just curious)!
 
Kashafungwa😆😆😆😆😆😆
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…