Ukisikia Mabeberu ni majambazi ni ukweli mtupu: Mahakama ya juu ya London imeipokonya Venezuela dhahabu ya dola bilioni moja

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,664
18,037
Mabeberu ni manyang'au!! ni majambazi, mbele ya pesa hayana simile!! Huwezi kuamini kuwa mahakama ya juu ya London imeamua kuwa dhahabu yote ambayo serikali ya Venezuela iliyokuwa imeiweka akiba kwenye benki kuu ya Uingereza imilikiwe na serikali ya Venezuela inayoongozwa na Juan Guaido.

Cha ajabu ni kuwa hakuna serikali ya Venezuela inayoongozwa na Juan Guaido. Maana Juan Guaido alishindwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika huko venezuela, lakini kwa kuwa Juan Guaido ni kibaraka wa mabeberu wa nchi za magharibi, serikali za mabeberu ziliamua kumtambua Juan Guaido kama ndio mshindi wa uchaguzi na zikamtambua kama rais wa Venezuela.

Kwa hiyo mali zote zilizokuwa za Venezuela zilizowekezwa huko Uingereza na Marekani zikawekwa chini ya madaraka ya kibaraka Guaido. Rais halali aitwaye Maduro akaamua kushitaki mahakama ya juu ya mjini London kuiomba iizuie serikali ya uingereza kupora mali zake kwa kumtumia kibaraka Guaido.

Hizi ndizo waswahili husema kesi ya Tumbili kula mahindi ya watu kupelekwa kwa Nyani!! Mahakama ya juu mjini London imeamua kuwa serikali ya "Rais" Guaido (asiyekuwa na nafasi yoyote Venezuela) ndiye mwenye mamlaka na dhahabu yote iliyoko benki uingereza yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni moja!

Kwa Mabeberu hiyo ndiyo demokrasia!! Wananchi waq Venezuela wanateseka kwa umaskini uliotokana na vikwazo vya mabeberu na ambao wameamua kupora pesa na dhahabu yao kwa kumtumia kibaraka wao Guaido!

Inasikitisha kuwa hao mabeberu ndiyo tunaowaita kama "washirika wa maendeleo" hapa nchini kwetu!! Mataifa mengi kwa sasa yameanza kushtuka kuweka akiba zao za fedha za kigeni kwenye mabenki ya mabeberu! Kilichowakuta pia mabilionea wa Urusi walioporwa mabilioni ya dola za kimarekaniu kwa kisingizio eti wako karibu sana na Putin!! Tusiwachekee mabeberu!!

London's High Court rules against Venezuela's Maduro in $1 billion gold battle​

LONDON, July 29 (Reuters) - London's High Court has rejected President Nicolas Maduro's latest efforts to gain control of more than $1 billion of Venezuela's gold reserves stored in the Bank of England's underground vaults in London.

It marked the latest victory for Guaido, who has won a series of legal clashes over the bullion after the British government recognised him rather than Maduro as the South American country's president.
 
Kwa nini waliweka dhahabu zao UK? ndo wakome wangeweka kwa kiduku wa n.korea au al asaad wa syria au kule iran, au russia ingekuwa poa.

Ila west wanaaminika aisee maana ndo kwenye hela na uhakika wa kuhifadhi hela au dhahabu au uwekezaji ndo maana hata majizi ya russia yameficha mapesa na kuwekeza western countries
 
Ukweli unaujua ila umeamua kuukwepa ili kuharalisha unachotaka. Kwa maelezo yako ina maana hiyo kesi wakati inafunguliwa ilikuwa inamhusu hasa Guaido. Na hukumu lazima itoke kumhusu Guaido.

Pili nani amewaambia mufiche mali za wananchi,pesa za wananchi, nchi nyingine?,il-hali nchi yenu ipo na ni huru?. Moja kwa moja hiyo ni mali ya wizi.

Tatu kwa vyovyote serikali ya Uingereza haiwezi kuitumia hiyo mali,kwa vyovyote itairudisha kwa wananchi wa Venezuela. Ila tu itairudisha baada ya kujirishisha uongozi uliopo Venezuela umetulia, na ni makini na si wa kifisadi
 
Kwa nini waliweka dhahabu zao UK? ndo wakome wangeweka kwa kiduku wa n.korea au al asaad wa syria au kule iran, au russia ingekuwa poa. Ila west wanaaminika aisee maana ndo kwenye hela na uhakika wa kuhifadhi hela au dhahabu au uwekezaji ndo maana hata majizi ya russia yameficha mapesa na kuwekeza western countries
Wewe unafikiri kwa kiduku ndio ingekuwa salama?. Sababu?. Hamjui tu kiduku ndio ana njaa ya hatari,ndio maana anashiliki hata vitendo vya kijambazi ili apate hela nchini mwake. Yeye amekazana tu ma-nukria,vita. Amesahau mambo mengi tu ya msingi nchi mwake. Pesa zote zimeishia kwenye ma-nukria.

Swali kwa nini iwe wakahifadhi nchi nyingine?si nchini mwao?
 
Ili

kurahisisha miamala ya kibiashara na kuweza kuitumia kama dhamana ya mikopo kwa urahisi.
 
Ukweli unaujua ila umeamua kuukwepa ili kuharalisha unachotaka. Kwa maelezo yako ina maana hiyo kesi wakati inafunguliwa ilikuwa inamhusu hasa Guaido. Na hukumu lazima itoke kumhusu Guaido...
Hili ndilo jibu sahihi.

Mabeberu pamoja na madhaifu yao wanajitambua sana.

Tukumbuke waliturufishia chenji ya rada
 
Uelezee uchaguzi uliompa ushindi Maduro dhidi ya Guaido. Isijekuwa kama wetu wa 2020 au 2019 serikali za mitaa.

Tuelezee vizuri
 
Ukweli unaujua ila umeamua kuukwepa ili kuharalisha unachotaka. Kwa maelezo yako ina maana hiyo kesi wakati inafunguliwa ilikuwa inamhusu hasa Guaido. Na hukumu lazima itoke kumhusu Guaido.

Pili nani amewaambia mufiche mali za wananchi,pesa za wananchi, nchi nyingine?,il-hali nchi yenu ipo na ni huru?. Moja kwa moja hiyo ni mali ya wizi.

Tatu kwa vyovyote serikali ya Uingereza haiwezi kuitumia hiyo mali,kwa vyovyote itairudisha kwa wananchi wa Venezuela. Ila tu itairudisha baada ya kujirishisha uongozi uliopo Venezuela umetulia, na ni makini na si wa kifisadi
Sijui hata ume-comment Nini?kwa hio pesa za urusi,dhahabu zao ambazo pia zimeshiliwa na ma-bank ya US+Western countries yaliibiwa Na serikali ya Russia halafu yakafichwa huko sio?
 
Mabeberu ni manyang'au!! ni majambazi, mbele ya pesa hayana simile!! Huwezi kuamini kuwa mahakama ya juu ya London imeamua kuwa dhahabu yote ambayo serikali ya Venezuela iliyokuwa imeiweka akiba kwenye benki kuu ya Uingereza imilikiwe na serikali ya Venezuela inayoongozwa na Juan Guaido.

Cha ajabu ni kuwa hakuna serikali ya Venezuela inayoongozwa na Juan Guaido. Maana Juan Guaido alishindwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika huko venezuela, lakini kwa kuwa Juan Guaido ni kibaraka wa mabeberu wa nchi za magharibi, serikali za mabeberu ziliamua kumtambua Juan Guaido kama ndio mshindi wa uchaguzi na zikamtambua kama rais wa Venezuela.

Kwa hiyo mali zote zilizokuwa za Venezuela zilizowekezwa huko Uingereza na Marekani zikawekwa chini ya madaraka ya kibaraka Guaido. Rais halali aitwaye Maduro akaamua kushitaki mahakama ya juu ya mjini London kuiomba iizuie serikali ya uingereza kupora mali zake kwa kumtumia kibaraka Guaido.

Hizi ndizo waswahili husema kesi ya Tumbili kula mahindi ya watu kupelekwa kwa Nyani!! Mahakama ya juu mjini London imeamua kuwa serikali ya "Rais" Guaido (asiyekuwa na nafasi yoyote Venezuela) ndiye mwenye mamlaka na dhahabu yote iliyoko benki uingereza yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni moja!

Kwa Mabeberu hiyo ndiyo demokrasia!! Wananchi waq Venezuela wanateseka kwa umaskini uliotokana na vikwazo vya mabeberu na ambao wameamua kupora pesa na dhahabu yao kwa kumtumia kibaraka wao Guaido!

Inasikitisha kuwa hao mabeberu ndiyo tunaowaita kama "washirika wa maendeleo" hapa nchini kwetu!! Mataifa mengi kwa sasa yameanza kushtuka kuweka akiba zao za fedha za kigeni kwenye mabenki ya mabeberu! Kilichowakuta pia mabilionea wa Urusi walioporwa mabilioni ya dola za kimarekaniu kwa kisingizio eti wako karibu sana na Putin!! Tusiwachekee mabeberu!!

London's High Court rules against Venezuela's Maduro in $1 billion gold battle​

LONDON, July 29 (Reuters) - London's High Court has rejected President Nicolas Maduro's latest efforts to gain control of more than $1 billion of Venezuela's gold reserves stored in the Bank of England's underground vaults in London.

It marked the latest victory for Guaido, who has won a series of legal clashes over the bullion after the British government recognised him rather than Maduro as the South American country's president.
Kwani nini fedha na dhahabu za Venezuela ziwekwe kwenye Bank ya Uingereza na sio Bank ya Venezuela?🤔
 
Ukweli unaujua ila umeamua kuukwepa ili kuharalisha unachotaka. Kwa maelezo yako ina maana hiyo kesi wakati inafunguliwa ilikuwa inamhusu hasa Guaido. Na hukumu lazima itoke kumhusu Guaido.

Pili nani amewaambia mufiche mali za wananchi,pesa za wananchi, nchi nyingine?,il-hali nchi yenu ipo na ni huru?. Moja kwa moja hiyo ni mali ya wizi.

Tatu kwa vyovyote serikali ya Uingereza haiwezi kuitumia hiyo mali,kwa vyovyote itairudisha kwa wananchi wa Venezuela. Ila tu itairudisha baada ya kujirishisha uongozi uliopo Venezuela umetulia, na ni makini na si wa kifisadi

You are making sense
 
Njaa zao ndio zimewakost..kwanini wakahifadhi dhahabu kwa mabeberu?

#MaendeleoHayanaChama
Tukio hili linatoa somo kwa nchi zinazoendelea (third World)mkombozi wao ni kujiunga na alliance ya BRICS hakuna jinsi.

Nikisema baadhi ya mataifa ya magharibi hayana "UTU" watu hawanielewi wanafikiri nakuwa driven na chuki binafsi-hiyo si kweli hata kidogo.
 
Wewe unafikiri kwa kiduku ndio ingekuwa salama?. Sababu?. Hamjui tu kiduku ndio ana njaa ya hatari,ndio maana anashiliki hata vitendo vya kijambazi ili apate hela nchini mwake. Yeye amekazana tu ma-nukria,vita. Amesahau mambo mengi tu ya msingi nchi mwake. Pesa zote zimeishia kwenye ma-nukria.

Swali kwa nini iwe wakahifadhi nchi nyingine?si nchini mwao?
Jamani!! Je,wewe umewahi kitembelea Taifa la Korea kaskazini ukaona jinsi miji yao ilivyo jengeka pia vijiji vyao na wakazi wake wanavyo ishi,je,uliwahi kushuhudia wakorea kaskazini wakifa njaa??

Ushauri wangu - wakati mwingine tuwe tunakuwa makini sana kuhusu taarifa/habari tunazo letewa na media za magharibi ambazo nyingi niza kuwachota akili wasomaji/wasikilizaji kwa kuzisema sema vibaya nchi ambazo hazitaki kufuata siasa za magharibi zenye uchonganishi na unyonyaji - wanataka masaa yote uwe hewala bwana (yes man), ufanye unacho ambiwa/elekezwa bila ya kuhoji swali ie ukoloni mambo leo.

Wangapi wanajuwa kwamba Korea kaskazini imeendelea sana katika fani ya sayansi na teknolojia hasa Information Technology na sayansi ya Roketi, mwaka juzi hapa Amerika ililalamika sana kwamba wataalamu wa tehama wa Kiduku walifanikiwa kuhack sensitive files za wizara ya ulinzi ya Merikani pia mafaili ya viwanda vya kuunda silaha zikiwemo ndege na roketi yaani servers zinazo hifadhi mafaili ya viwanda hivyo nayo yalipakuliwa - mtu unakaa unajiuliza hivi si Merikani usema taifa la Korea Kaskazini si lolote si chochote ni mbumbubu tu hata raia wake ulala mitini, sasa hawa mambumbubu walifanikiwaje kupakuwa taarifa muhimu kutoka kwenye Servers za Taifa ambalo ndilo babalao kweye nyaja za sayansi na teknolojia!!

Mwisho nataka niwambieni kwamba Korea kasikazini inaunda smartphones za hali za juu, wanaunda vile vile computer na tablets na kikubwa zaidi walibuni/code system software za kwao (operating system) zinazo tumika ku-run application program zao,je,ni mataifa mangapi Duniani yaliyo wahi kubuni na kufanikisha kucode a trurily independent Operating systems za Computer na simu, mataifa mangapi yamefanikiwa kuunda landbased au Submarine launched ICBM zikiwa zime sheheni thermonuclear payloads - ni mataifa machache sana.

Bottom line ni kwamba taifa la Korea Kaskazini si la kubezabeza.
 
Funzo kubwa sana hilo kwa hizi nchi zilizobakia ya kuwa usimwamini beberu
Nalog off  Z
 
Back
Top Bottom