Richard irakunda
JF-Expert Member
- Oct 23, 2018
- 3,660
- 4,383
Safi saana umeeleza vizuri sanaMoscow siku hizi hapigani vita za kiitakadi kama umoja wa kisovieti. Hapa ni maslahi tu ya kiuchumi na mzani wa nguvu, ujamaa dhidi ya ubepari hakuna siku hizi. Kule Syria Urusi hakwenda kulinda ujamaa bali maslahi yake ya kiuchumi. Kule Ukraine Marekani ameenda kwasababu za maslahi ya kiuchumi na siyo vita dhidi ya wajamaa.
Ujamaa umekufa na hauna nguvu tena kwenye dunia hii ya sasa, kule Venezuela Uchina na Urusi wanapiga kelele kwasababu wana maslahi mapana ya kiuchumi. Wameikopesha sana serikali ya maduro kipindi kile imekutwa na majanga ya kiuchumi. Juzi hapa ameenda Uchina kuomba mkopo na kukubaliana kwamba watalipa mkopo kwa kutumia mafuta. Hii ni neema kwa Uchina.
Mbali na hilo imegundulika kwamba Venezuela ndiyo nchi yenye mafuta mengi hapa duniani, Uchina atayataka na Marekani anayataka.
Upande wa pili wa shilingi kama Marekani atafanikiwa kukamata utajiri wa mafuta wa Venezuela unategemea Urusi atapona kwenye soko la dunia la mafuta ?? Marekani atakuwa anacheza na bei za mafuta kama anavyofanya kule Saudi Arabia ili kuwaumiza warusi ambao asilimia zaidi ya 50% ya pato la taifa hutegemea mafuta.
Kuna mambo ya kuyaangalia sana, Urusi kupambana na Marekani kule Venezuela ni ngumu sana kwasababu mbali na Cuba sidhani kama ana washirika wenye nguvu. Kule Syria ilikuwa ni rahisi kwasababu alikuwa na washirika vyuma kama Iran, Lebanon na Hezbollah. Venezuela ni tofauti kidogo kwasababu Marekani ndiyo ana washirika wengi sana ambao wameizunguka Venezuela. Colombia na Venezuela wanashare mpaka wa kilomita zaidi ya 2000. Vikosi vya Marekani viko Columbia mpaka sasa.
Mwisho kabisa Marekani anacheza vizuri kwasababu anajua kama Venezuela itachafuka basi ule ukanda wote utachafuka kama ilivyo mashariki ya kati. Colombia hatapona. Serikali ya maduro ikianguka kutakuwa na ombwe la madaraka ambalo litapelekea makundi madogo madogo kuzaliwa, biashara haramu kutoka colombia na wimbi la wakimbizi ambalo kama likienda Colombia basi lazima kitanuka tu....
Sasa kama ni maslahi yao basi watamsaidia maduro kufa kupona na kwa bahati nzuri China this time now lazima aingie mazima ili kurinda maslahi yake sasa tayari urusi ana mshirika mwenye nguvu
All in all hii Venezuela ni muhimu saana kwa urusi na China kuliko USA alafu hawa Colombia nchini kwao si kuna kundi la waasi wanaotaka kuangusha utawala?
Sent using my iPhone using jamiiforum app