Juan Guaido wa Venezuela kufungwa miaka 30 jela

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Kiongozi wa upinzani Venezuela anakabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela

Feb 27, 2019 08:04 UTC
Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani aliyejitangaza kuwa rais wa mpito wa Venezuela anaandamwa na kifungo cha miaka 30 jela.
Hayo yamesemwa na Juan Carlos Valdez, Naibu Jaji wa Jopo la Haki la Mahakama ya Juu nchini humo katika mahojiano na shirika la habari la Sputnik la Russia na kuongeza kuwa, hatua ya Guaido ya kwenda Colombia mnamo Februari 22 ilikiuka agizo la kumtaka asitoke nje ya nchi, lililotolewa na Mahakama ya Juu nchini humo, na hivyo amejiweka katika hatari ya kufungwa miaka 30 jela.

Amefafanua kuwa, "Guiado ni mtu anayekwepa sheria. Kitendo cha kutoroka nchini kinyume cha sheria na kisha kurejea hukumu yake ni kifungo cha hadi miaka 30 jela."

Venezuela ilitumbukia katika mzozo wa kisiasa mwishoni mwa mwezi jana baada ya Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani kujitangaza kuwa rais wa muda wa nchi hiyo.

Hatua hiyo iliyotekelezwa tarehe 23 Januari 2019, iliungwa mkono na Marekani na nchi za Ulaya, huku serikali ya Caracas ikiitaja kuwa ni sawa na tangazo la mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais Nicolás Maduro.

Licha ya uungaji mkono wa hali na mali wa Marekani na kambi ya Magharibi kwa Juan Guaidó, lakini raia na jeshi la Venezuela pamoja na mataifa kama vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia, China, Mexico, Uturuki, Afrika Kusini na Italia wameendelea kumuunga mkono Rais Nicolás Maduro anayetambulika kisheria.

VENEZUELA
 
Maduro ana uvumilivu aisee angeku kwenye nchi ya malaika jiwe kama sio maiti basis angekuwa kilema.
 
Huyu Maduro nchi ataipeleka pabaya sana si muda mrefu tena, Na sasa ajaribu kumfunga jela Juan Guaido hapo ndio itakuwa tamati
 
Juan alitakiwa awe ameshanyongwa siku nyingi sana. Lakini cha kushangaza anabembelezwa na anaendelea kula bata na kusababisha mtafaruku.
 
Kiongozi wa upinzani Venezuela anakabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela
Feb 27, 2019 08:04 UTC
Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani aliyejitangaza kuwa rais wa mpito wa Venezuela anaandamwa na kifungo cha miaka 30 jela.
Hayo yamesemwa na Juan Carlos Valdez, Naibu Jaji wa Jopo la Haki la Mahakama ya Juu nchini humo katika mahojiano na shirika la habari la Sputnik la Russia na kuongeza kuwa, hatua ya Guaido ya kwenda Colombia mnamo Februari 22 ilikiuka agizo la kumtaka asitoke nje ya nchi, lililotolewa na Mahakama ya Juu nchini humo, na hivyo amejiweka katika hatari ya kufungwa miaka 30 jela.
Amefafanua kuwa, "Guiado ni mtu anayekwepa sheria. Kitendo cha kutoroka nchini kinyume cha sheria na kisha kurejea hukumu yake ni kifungo cha hadi miaka 30 jela."
Venezuela ilitumbukia katika mzozo wa kisiasa mwishoni mwa mwezi jana baada ya Juan Guaidó, kiongozi wa upinzani kujitangaza kuwa rais wa muda wa nchi hiyo.
Hatua hiyo iliyotekelezwa tarehe 23 Januari 2019, iliungwa mkono na Marekani na nchi za Ulaya, huku serikali ya Caracas ikiitaja kuwa ni sawa na tangazo la mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais Nicolás Maduro.
Licha ya uungaji mkono wa hali na mali wa Marekani na kambi ya Magharibi kwa Juan Guaidó, lakini raia na jeshi la Venezuela pamoja na mataifa kama vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia, China, Mexico, Uturuki, Afrika Kusini na Italia wameendelea kumuunga mkono Rais Nicolás Maduro anayetambulika kisheria.
Tags
VENEZUELA
Huyo ndio raisi ajaye,Madulo,asubili kuchomolewa na CIA,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata bila hivyo Us wameshapania kumtoa nadhani kizuizi pekee ni Moscow
Siyo mpole, anajua akifanya ujinga tu kule Washington watapata kisingizio kizuri cha kumvamia. Tena watamtwanga hataamini, maana sidhani kama kuna nchi inaweza ikashindana na Marekani kule Amerika Kusini halafu ikabaki salama.

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Hata bila hivyo Us wameshapania kumtoa nadhani kizuizi pekee ni Moscow

Sent using my iPhone using jamiiforum app
Moscow ana nguvu na ushawishi lakini sidhani kama na nguvu kiasi hicho kule Amerika Kusini kama ambavyo ana nguvu kule Syria. Sema Marekani anaogopa kwamba akiivamia Venezuela basi anaweza hatarisha hata usalama wake mwenyewe hivyo anacheza kwa akili sana. Kushindana na Marekani kule Amerika Kusini ni sawa na kushindana na Urusi kule Ulaya Mashariki au Uchina kule bahari ya Uchina Kusini.

Ngumu sana kushindana na Marekani kwenye The Western Hemishphere ndiyo maana Lex Tillerson alisema kwamba hata biashara za Uchina zinahatarisha usalama na maslahi yake. Kiufupi The Munroe Doctrine bado inaendelea kufanya kazi, Urusi ya Kisovieti ilijaribu kupeleka ukomunisti kule Amerika Kusini lakini Marekani akatengeza makundi ya wauza unga, waasi na madikteta ili kuwavuruga kabisa wakomunisti.

Unakumbuka Nicaragua miaka ya 1980's ilivyosimbuliwa na magaidi ?? Au tusiende mbali, unakumbuka walivyovamia Panama na kumtoa Manuel Noriega ?? Hatari sana...
 
Fact lkn this time ushawishi wa Moscow unapenya kwa kasi sana
Pia hapa hili game limeshakuwa kati ya capitalist vs socialist

Kubwa zaidi jeshi na raia wengi bado wapo na maduro kibaya zaidi usa kaboronga saana kuanzia Iraq to Libya so haaminiki

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Fact lkn this time ushawishi wa Moscow unapenya kwa kasi sana
Pia hapa hili game limeshakuwa kati ya capitalist vs socialist

Kubwa zaidi jeshi na raia wengi bado wapo na maduro kibaya zaidi usa kaboronga saana kuanzia Iraq to Libya so haaminiki

Sent using my iPhone using jamiiforum app
Moscow siku hizi hapigani vita za kiitakadi kama umoja wa kisovieti. Hapa ni maslahi tu ya kiuchumi na mzani wa nguvu, ujamaa dhidi ya ubepari hakuna siku hizi. Kule Syria Urusi hakwenda kulinda ujamaa bali maslahi yake ya kiuchumi. Kule Ukraine Marekani ameenda kwasababu za maslahi ya kiuchumi na siyo vita dhidi ya wajamaa.

Ujamaa umekufa na hauna nguvu tena kwenye dunia hii ya sasa, kule Venezuela Uchina na Urusi wanapiga kelele kwasababu wana maslahi mapana ya kiuchumi. Wameikopesha sana serikali ya maduro kipindi kile imekutwa na majanga ya kiuchumi. Juzi hapa ameenda Uchina kuomba mkopo na kukubaliana kwamba watalipa mkopo kwa kutumia mafuta. Hii ni neema kwa Uchina.

Mbali na hilo imegundulika kwamba Venezuela ndiyo nchi yenye mafuta mengi hapa duniani, Uchina atayataka na Marekani anayataka.

Upande wa pili wa shilingi kama Marekani atafanikiwa kukamata utajiri wa mafuta wa Venezuela unategemea Urusi atapona kwenye soko la dunia la mafuta ?? Marekani atakuwa anacheza na bei za mafuta kama anavyofanya kule Saudi Arabia ili kuwaumiza warusi ambao asilimia zaidi ya 50% ya pato la taifa hutegemea mafuta.

Kuna mambo ya kuyaangalia sana, Urusi kupambana na Marekani kule Venezuela ni ngumu sana kwasababu mbali na Cuba sidhani kama ana washirika wenye nguvu. Kule Syria ilikuwa ni rahisi kwasababu alikuwa na washirika vyuma kama Iran, Lebanon na Hezbollah. Venezuela ni tofauti kidogo kwasababu Marekani ndiyo ana washirika wengi sana ambao wameizunguka Venezuela. Colombia na Venezuela wanashare mpaka wa kilomita zaidi ya 2000. Vikosi vya Marekani viko Columbia mpaka sasa.

Mwisho kabisa Marekani anacheza vizuri kwasababu anajua kama Venezuela itachafuka basi ule ukanda wote utachafuka kama ilivyo mashariki ya kati. Colombia hatapona. Serikali ya maduro ikianguka kutakuwa na ombwe la madaraka ambalo litapelekea makundi madogo madogo kuzaliwa, biashara haramu kutoka colombia na wimbi la wakimbizi ambalo kama likienda Colombia basi lazima kitanuka tu....

CC: Wick uje huku Cousin
 
Back
Top Bottom