Iran na Venezuela wasaini dili la trilioni 50 sisi tunauza bandari huku

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Iran ni taifa teule wallah wamesaini dili la trilioni 50 na Venezuela sisi tupo bize tunauza bandari zote za bara kwa waarab Shame on you Chief Hangaya Mangungo....Msisahau miaka ya juzi kati Iran na China walisaini dili la trilioni 927 halafu sisi tupo tunasubiria kupigwa mnada huku Iran na Urusi ni mataifa teule ya Mungu

Iran na Venezuela zasaini hati 19 za ushirikiano; mabadilishano ya kibiashara kufikia dola bilioni 20 sawa na kama trilioni 50 za kitanzania

Rais Ebrahim Raisi wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu na Venezuela zina uwezo wa kuongeza kiwango chao cha mabadilishano ya kibiashara kifikie cha thamani ya dola bilioni 20.

Rais Raisi amesema hayo katika kikao na waandishi wa habari akiwa na mwenzake wa Venezuela, Nicolas Maduro mjini Caracas jana Jumatatu, ambapo amesisitiza kuwa mataifa haya mawili yana uwezo wa kuimarisha mahusiano yao ya kiuchumi.

Kwa mujibu wa Raisi, mabadilishano ya kibiashara baina ya Iran na Venezuela miaka miwili iliyopita yalikuwa yenye thamani ya dola milioni 600, na kwamba hivi sasa kiwango hicho kimefikia dola bilioni 3, lakini kitaongezwa hadi dola bilioni 10 katika awamu ya kwanza.

Kuhusu uhusiano wa pande mbili wa Tehran na Caracas, Raisi amesema mataifa haya mawili yana uwezo wa kuboresha mahusiano yao kwa kuwa yana mambo yenye maslahi ya pamoja, maadui na mitazamo inayolandana hasa katika masuala ya uhuru na uadilifu.

Sayyid Ebrahim Raisi jana Jumatatu alianza ziara rasmi ya kuzitembelea nchi tatu za Amerika ya Latini za Venezuela, Nicaragua na Cuba akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Iran.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ameashiria kusainiwa hati 19 za makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa nchi mbili hizi katika nyuga tofauti na kueleza kuwa, Iran na Venezuela zina hamu na zimejitolea kwa dhati kuimarisha mahusiano ya pande mbili.

Hati mbalimbali za ushirikiano kati ya Iran na Venezuela zilizosainiwa jana mjini Caracas zinatazamiwa kuhakikisha kuwa mataifa haya mawili yanaboresha ushirikiano wao katika nyuga za tiba, nishati, utamaduni, habari na mawasiliano, elimu ya juu, bima, usafiri wa baharini, teknolojia pamoja na kilimo.

My take:Atakayeilaani Iran na Russia naye atalaaniwa....Atakayeibariki Israel na kuisifia naye atalaaniwa maana amebariki ushoga na kukuubali na wote tuseme.... "Ameeen".....

4c3mf897010fb12b25x_800C450.jpg
 
Hio dili hujui hata wamekubaliana biashara gani.hujui wanauiziana nn.ila umekimbilia kwenye t50 .samia nae kafanya hivo hivo unasema kauza bandari 🥸una matatizo ww
 
Hio dili hujui hata wamekubaliana biashara gani.hujui wanauiziana nn.ila umekimbilia kwenye t50 .samia nae kafanya hivo hivo unasema kauza bandari 🥸una matatizo ww
Duh alivyofanya samia tuambia ni mkataba wa muda gan ? Tunauza hisa ? Je zote au kiasi ? Tunakodisha? Au tunashare majukumu ndani ya bandari ? Au tunakarbisha kuboresha ? Je nini maslai yetu hapo ? Je hatuez bana hao wala 41 B na wengine tukapata angalau 1T ikaboresha Bandari kuanzia miundo mbinu mpaka watendaj wake ili tupate watu sahihi ndani ya mazingira sahihi ? Je katiba yetu inazungumzia nn juu ya uendeshaji mali za umma ? je Ssh katimiza matakwa ya katiba ?
 
Wewe wacha kupotosha, bandari ipi iliyouzwa?

Mtaumia sana, waarabu ndiyo wanadunda hivyo.
Inasikitisha kuona uni inamtia mwafrika wehu , nliona chapisho moja a china linasema waafrika wanatapeliwa kupitia dini , akija mzungu mkristo anampa kila kitu sasa hv wanakuja wazungu waislam wamewehuka wanataka uza nchi kbs na hawajastuka hlf baadae tunalia hatuendelei kisa ukolon wakati ukolon tunaurudisha wenyew , nchi za kiislam zinavunja mikataba na hiyo kampun ila waislam wetu hapa ndo wapo mbele kutetea huo ujinga
 
Binadam.

. Vipi, swali langu linekuwa gumu sana kwako? Jifikirie.
Hajitambui huyo , dini imemtoa akili , anajihisi ni muarabu , bado waafrika tutaendelea kusota sana mpk vitukuu ndo vitakuja kujielewa wao ni nan
 
Tena tunaona raha mpaka ndani ya roho.

Utakufa nacho kijiba cha roho.
Ila hao hawajafuata uislam wamekuja kimkakati , najua ww ni mjing ila vitukuu vyako wataurekebisha ujinga wako , kama akina Nyerere walivyorekebisha ujinga wa babu zao , Trump alisema bad waafrika hatuna uwezo wa kujitawala kbs , dini unapewa dini unauza uhuru wako , bure kbs , aya nayaandika hapa wapo wavaa kobaz wataanza yaepewa baada ya miaka 50 baada ya kuona mwarab anataka nn kwetu
 
Duh alivyofanya samia tuambia ni mkataba wa muda gan ? Tunauza hisa ? Je zote au kiasi ? Tunakodisha? Au tunashare majukumu ndani ya bandari ? Au tunakarbisha kuboresha ? Je nini maslai yetu hapo ? Je hatuez bana hao wala 41 B na wengine tukapata angalau 1T ikaboresha Bandari kuanzia miundo mbinu mpaka watendaj wake ili tupate watu sahihi ndani ya mazingira sahihi ? Je katiba yetu inazungumzia nn juu ya uendeshaji mali za umma ? je Ssh katimiza matakwa ya katiba ?

Mkuu cc ni mashahid dhid vitu vinavotokea serikali ikiwa inaendesha mfn shirika la ndege tumeweka bei gani.na matokeo yake tunaona hasara kila cku,tukija Tanesco hali ile ile.sasa kwann kampuni kubwa kama hio tusiingie nayo mkataba wa kuendesha hio bandari cc tukapta faida yetu tena kubwa kuliko mwanzo.hapo mkuu utasema tumeibiwa
 
Ila hao hawajafuata uislam wamekuja kimkakati , najua ww ni mjing ila vitukuu vyako wataurekebisha ujinga wako , kama akina Nyerere walivyorekebisha ujinga wa babu zao , Trump alisema bad waafrika hatuna uwezo wa kujitawala kbs , dini unapewa dini unauza uhuru wako , bure kbs , aya nayaandika hapa wapo wavaa kobaz wataanza yaepewa baada ya miaka 50 baada ya kuona mwarab anataka nn kwetu

Kwan hio kampuni imeanza kuendesha bandari ya hapa tuh.je hizo nchi nyingine nazo zimetapeliwa au ?
 
Hilo dili ni kama lile la Korosho la Kabudi na Wakenya.
 
Hio dili hujui hata wamekubaliana biashara gani.hujui wanauiziana nn.ila umekimbilia kwenye t50 .samia nae kafanya hivo hivo unasema kauza bandari 🥸una matatizo ww
Labda watauziana uranium lkn anko Sam anawapimia tu.
 
Back
Top Bottom