Jua kusamehe ewe mwanandoa

bomouwa

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
1,149
798
Habari wanajamvi?

Mke na mume asubuhi moja wamegombana ndani ya nyumba. Mwanaume anadai kwamba mkewe ndio mwenye kosa na anapaswa kumuomba msamaha. Mke hakuona ni issue kwake na hakuona haja ya kusema "samahani" kwa mumewe.Hii ni kawaida kwa wanandoa na waliopo kwenye mahusiano, mmoja amefanya kosa ila analichukulia kirahisi rahisi tu.Baada ya siku tatu, mgomo baridi ukawepo ndani ya nyumba. Mwanaume anasema lazima mke wake amuombe samahani. Mke hataki kuomba msamaha. Mke angepika chakuka lakini mume hakula. Kila siku alikuwa akirudi na chakula tokea hotelini (take away).

Mke akasema kama noma na iwe noma, akahama kabisa chumba na kwenda kulala na watoto.Jumapili moja, walienda kanisani katika ibada. Kila mmoja alienda kivyake na gari yake. Ila ndani ya kanisa katika ibada walikaa pamoja wakijifanya kuwa ni wanandoa wanaopendana! Unafiki ulioje ndani ya nyumba ya Mungu! Mungu awasamehe Wanandoa wanaofanya hivi.

Lakini baada ya ibada mume alitangulia nyumbani na watoto wakati mkewe akisubiri kikao cha wanawake pale kanisani. Siku hiyo shetani aliamua aingilie kati ugomvi walioukaribisha ndani ya ndoa yao.Mume alikuwa amefika nyumbani tayari, alipoiangalia simu yake, mke wake alikuwa amempigia mara tatu. Hakujisumbua kumpigia baada ya kuziona missed calls. Bifu kali lilikuwepo.

Mkewe akadrive kurudi nyumbani baada ya lisaa limoja. Mume akamuona mlinzi wa mlangoni akifungua geti na huku simu yake ilikuwa ikiita pia. Aliiangalia na kuona ni namba ya mkewe. Na alikuwa kashaingia na gari katika garage ya kupack gari."Anapiga kwanini na wakati ashaingia nyumbani? Asilete mahaba yake ya kihindi hapa huu ni upumbavu na utoto!" Mume alisema na kuzipotezea calls za mkewe. Simu iliendelea kuita mume ndio kwanza akakunja nne akitazama sinema.

Baada ya nusu saa, mke hakuingia ndani. Kitu kikamwambia mumewe atoke nje akatizame kwanini mkewe haingii ndani. Bado yupo ndani ya gari? Ndio lazima atakuwemo ndani ya gari. Ila kabla akamwita mlinzi wa getini."Mama yupo ndani ya gari?" mume aliuliza, mlinzi akajibu " ndio madam amelala ndani ya gari"Mume akainuka mbio huku akipiga kelele kama mtoto "PUMU! PUMU! PUMU MUNGU WANGU, ITAKUWA IMEMKAMATA KAMA KAWAIDA YAKE, ATAKUWA ALISAHAU KIFAA CHA KUPUMULIA (INHALER)''.

Haraka haraka akaingia chumbani na kuchukua kifaa cha kupumulia (Inhaler). Alipofika nje katika gari baada ya kufungua mlango alihisi pumzi inataka kumtoka!Mkewe alikuwa ameegemea usukani wa gari hajitambui.Yeye pamoja na mlinzi walimbeba na kumweka siti ya nyuma na mume akaliondoa gari kwa kasi kuelekea hospitali ya karibu. Kufika hospitalini baada ya vipimo ikathibitika mke amefariki kwa PUMU.

Kama angepokea simu ya mkewe mapema inawezekana angeokoa maisha ya mkewe. Kama mtaacha ugomvi wenu ndani ya ndoa kwa muda mrefu hupelekea shetani kuingilia huo ugomvi na kusababisha matatizo makubwa.Mume alilia mno na kujilaumu kwa kuchangia kifo cha mkewe.Mungu mwenyewe anajua wake wangapi, waume wangapi, watoto wangapi katika familia wamefariki katika mazingira kama hayo ya kukosa msaada kwa sababu tu ya kuchukulia mambo kirahisi rahisi.

Tafadhali sana rafiki, usiache jua lizame huku bado ukiwa na hasira. Vyovyote vile itakavyokuwa tengeneza amani na mpendwa wako. Hakuna kitu kinauma katika maisha kuishi huku ukijua ulichangia kifo cha mtu fulani. Kumbukumbu hua haifutiki.Shuka katika farasi wako alie juu sana, omba msamaha pale ulipokosea. Kamwe hauwezi badilika jinsia yako kama utajishusha na kuomba msamaha.Ndoa ngapi zingeokolewa kama wanandoa kwa umoja wao wangeamua kula kwa pamoja papai nono?

Make a conscious effort today to keep your home intact. I pray you will never weep over your family.

Kwa niaba ya wanandoa wenzangu mimi bomouwa, tujali kiapo tulichoapa altareni.
 
Umesema vema sana mkuu, Ndoa za watu zione kwa nje tu huko ndani ni balaa sana...
 
'Samahani'...! Neno dogo lenye uzito mkubwa
29a5118a50b139408d27a517c79e4e35.jpg
 
Thanks Bomouwa for this nice stuff. Yani hapa niko sebuleni tumenuniana na na mke wangu. Nakua mzito sana kusema am sorry for overreacting coz yeye ndo kanikosea. f
Mkuu kama yeye ndiyo mwenye makosa kwa nini wewe umuombe msamaha? Wewe vunja ukimya mueleze alichokukosea labda hajui hata amekukwaza na baada ya kumweleza we kuwa kawaida kabisa...Wanaume huwa hatununi mkuu tunauchuna...Ila ni kweli ndoa zinachanga moto sana..
 
Jangoz!kama habari tajwa imekuingia,msamehe hata kama hajakuomba msamaha na usahau.. katika mahusiano kuna mengi na kiuhalisia NDOA inakua ngumu kama mme anataka kua juu na mke halikadhalika. LAKINI amini kitu hiki,ujinga ni funguo wa maemdeleo ya NDOA na kama katika mahusiano ya KIMUNGU namaanisha ndoa takatifu baasi Mungu lazima aonekane.
Kumbuka kuanza na Mungu kila uamkapo na.ukitubu mueleze matamanio yako katika ndoa yako na ukiamini basi Ndoa yako hautaichukia kamwe.
 
Jangoz!kama habari tajwa imekuingia,msamehe hata kama hajakuomba msamaha na usahau.. katika mahusiano kuna mengi na kiuhalisia NDOA inakua ngumu kama mme anataka kua juu na mke halikadhalika. LAKINI amini kitu hiki,ujinga ni funguo wa maemdeleo ya NDOA na kama katika mahusiano ya KIMUNGU namaanisha ndoa takatifu baasi Mungu lazima aonekane.
Kumbuka kuanza na Mungu kila uamkapo na.ukitubu mueleze matamanio yako katika ndoa yako na ukiamini basi Ndoa yako hautaichukia kamwe.
Ww unaweza kufanya hivyo?
 
Sio tu ninaweza,lakini katika kipindi cha miaka 5 huu wa sita ikifika july,tumeishi tukiwa na.milima.na.mabonde lakini nashukuru hua mimi ni mjinga sana na mechanism yangu inafanikisha sana kuepuka.migogoro isiyo na tija...
Nimempa mke wangu uhuru sana na hua namuomba.Mungu amuongoze haijalishi anautumia uhuru kwa kiasi gani iwe kwa mema au mabaya lakini la.msingi hua namtanguliza Mungu katika kunipa Hekima ya kuishi na mke wangu... kumbuka Mungu ameagiza kuishi na mwanamke wa busara..
 
Back
Top Bottom