JPM tusaidie watumizi wa internet, makampuni yanatunyonga

JPM tusaidie watumizi wa internet, makampuni yanatunyonga

Egwugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,558
Reaction score
8,555
Toka mwezi huu umeanza kusema kweli ni majuto, vifurushi tunavyonunua kila siku mda unaisha vikiwa havijaweza kutumika kutokana na mitandao kuwa chini kupitiliza. Hatuelewi hasa ni nini hii lakini itoshe kusema pesa zetu za mb zimeibiwa na kuchezewa mno mwezi huu. Serikali kama ipo tunaomba walifanyie kazi hili, mitandao na makampuni yote wameamua kutunyonga sie wateja wao. Haiwezekani mtu unahangaika zaidi ya masaa 5 kila siku kupata internet tena kwa mbinde wakati pesa ni zetu na vifurushi tumenunua.

Huu ni wizi wa makusudi kabisa
 
SEMA MTANDAO UNAOKUPA SHIDA NA WAPI? BE SPECIFIC

Toka mwezi huu umeanza kusema kweli ni majuto, vifurushi tunavyonunua kila siku mda unaisha vikiwa havijaweza kutumika kutokana na mitandao kuwa chini kupitiliza. Hatuelewi hasa ni nini hii lakini itoshe kusema pesa zetu za mb zimeibiwa na kuchezewa mno mwezi huu. Serikali kama ipo tunaomba


walifanyie kazi hili, mitandao na makampuni yote wameamua kutunyonga sie wateja wao. Haiwezekani mtu unahangaika zaidi ya masaa 5 kila siku kupata internet tena kwa mbinde wakati pesa ni zetu na vifurushi tumenunua.

Huu ni wizi wa makusudi kabisa
 
We unaishi wapi... Kolomije? Mbona town tunapata 4G
4G iko maeneo machache sana hapa nchini, maeneo mengi inapatikana 3G. Kuna wakati nilienda kilimanjaro kipindi flani 4G bado haikuwepo hivyo ikawa ni mwendo wa mdogo mdogo kubembeleza internet japo kwa sasa nasikia ipo.
 
SEMA MTANDAO UNAOKUPA SHIDA NA WAPI? BE SPECIFIC
Airtel, Voda & Halotel yote ni majanga. Uenda tukawa tunatofautiana lakini hiyo isiwe sababu pekee kwamba hili tatizo halipo kwa wengine. Siwezi kuwa eneo lile lile kipindi fulani mtandao unakuwa smart alafu baadae eneo hilo hilo mtandao unasumbua kupita maelezo ukasema eti kisa niko koromije, basi kama ni hivyo siku za nyuma isingekuwa kinyume chake. Na hivi navyoandika niko home hapa Tz ndo yanakotokea haya, sielewi walioko huko koromije sasa
 
Sasa kama kila siku mnailalamikia tu serially na kufungia mitandao ngumu...bora tupige ela ya kodi tu
 
Aisee nasikitika kukwambia kuwa hilo ombi lako halitapata ufumbuzi hata kidogo coz uliyemwomba mwenyewe alishasema kuwa anatamani hata hiyo Internet isingekuwepo. Yaani akiamka hata kesho asikute Internet ili madili yapigike vizuri.
 
Elezea pia matumizi yako ni yapi ili hoja yako iwe na nguvu.
Unataka niseme nilikuwa natumia 10Gb kwa.siku alafu sahivi imeshuka hadi 1Gb kwa siku ndo utaelewa siyo? Alafu kila mmoja si ana uwezo wa kuelewa simu yake ina nini ama unahisi matumizi yako ndo yangu? kinachomake sense ni serikali kutumia vyombo vyake kufanya uchunguzi make sie watumiaji nafasi yetu ni kuhabarisha mamlaka husika ili zifatilie endapo kuna ukweli watumiaji wasaidiwe kwa namna iliyokuwa bora zaidi... only that.
 
Mi eneo naloishi siku za Mwanzo Internet ilikuwa na speed sana.
Yaani kabla hujaclick tayari imeishafungua. Mpaka nikawa nasema hawa voda mbona wananipendelea hivyo.
Kimbembe kimeanza mwezi wa 9, ni mwendo 'E tu'.
Unaweza kuclick kisha ukaenda dukani kwa Mangi mpaka ukarudi bado haifungua.
 
Toka mwezi huu umeanza kusema kweli ni majuto, vifurushi tunavyonunua kila siku mda unaisha vikiwa havijaweza kutumika kutokana na mitandao kuwa chini kupitiliza. Hatuelewi hasa ni nini hii lakini itoshe kusema pesa zetu za mb zimeibiwa na kuchezewa mno mwezi huu. Serikali kama ipo tunaomba walifanyie kazi hili, mitandao na makampuni yote wameamua kutunyonga sie wateja wao. Haiwezekani mtu unahangaika zaidi ya masaa 5 kila siku kupata internet tena kwa mbinde wakati pesa ni zetu na vifurushi tumenunua.

Huu ni wizi wa makusudi kabisa

Mkuu acha hili la kutafuta internet, issue inakuja pia kwenye MB unazopewa! Nilitaka kucheck kama hawa jamaa Ni wa kweli, nikaistall Data Manager. Hii data manager inakwambia umetumia MB ngapi kila APP kwenye simu, in short inahesabu! Nikanunua 2GB, baada ya three days nacheck salio wanasema nimebakiza MB 730, Data Manager inaniambia MB zimetumika ni 500 tu! In short hawa jamaa wanajua watu wengi don't monitor! Nimewapigia wakasema yalikuwa makosa tu ya 'mtandao' wamerudisha MB zilizopelea!
 
Nipo chini ya mnara wa halotel lkn network ina katakata kila baada ya sekunde kadhaa..

Na huenda halotel ukawa mtandao hovyo kuwahi kutokea hapa nchini!
 
Kwa kweli naunga mkino hoja...Mimi hapa nipo hapahapa Mji muhimu wa Tanzania yaani kwa Dar lakini intaneti ni sawa na hamna.

Hali hii imeanza mwezi wa tisa iv. Mtandao ninaotumia ni Airtel. Yaani haifungui. Sàa zingine unashtukia alama ya data zimewashwa inatoweka kabisa na ndo kwisha kabisa mpaka uzime data uwashe tena kaalama kanarudi ila mtandao haushiki!!! Au unakuwa extremely slow.

Kwa upande wa Voda mtandao siyo mbsya sana kama Airtel ila sasa data ukiweka mfano GB1ndani ya nusu saa zimeshaisha na haujadownload kitu bali una-surf tu mtandaoni, yaani wanakera na wananyonya wateja kama mimi!

Vyombo husika help me out...
 
hiyo mitandao yote ningekuwa mimi ningefuta ni wezi kuliko wale wa kariakoo.
 
Hivi kwa mfano kama mimi najua kwenye simu ndipo sehemu muhimu zaidi iliyobakia ambako utapata habari zangu za kunichafua na pengine hata wewe kupatumia kunichafua ukiniomba nikurushie salio nitakurushia kweli?
 
Back
Top Bottom