Joyce Ndalichako Amechemka, Ajipange!!!

Joyce Ndalichako Amechemka, Ajipange!!!



Kuna watu, kama Ndalichako wanasema eti wanasiasa wasiingilie kazi za elimu. Watendaji wa elimu wafanye wanavyotaka, wanasiasa wanyamaze tu, hata kama watendaji wamefanya madudu. Kutakuwa na umuhimu gani wa kuwa na wanasiasa? Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani anaongea sana kwa kujihami sawa na wanasiasa halafu haitaki siasa. Yeye ndiye mwanasiasa namba moja. Hatujawahi kuona Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani anayeongea ongea sana kama huyu.

Watendaji katika Wizara mbalimbali kama vile Elimu hususani Baraza la Mitihani wanavurunda kazi (mitihani) kila kukicha, wananchi na wabunge wanalalamika, wao kwa kujihami wanataka wasiingiliwe na wanasiasa. Je, kukosolewa ni kuingiliwa utendaji wao? Ukatibu utendaji SIO taaluma, ni cheo cha kupewa tu. Baadhi ya viongozi wa Baraza la Mitihani achieni ngazi kulinda heshima zenu.

Isingekuwa wanasiasa hadi leo kusingekuwa na sekondari za kata, wanafunzi wasingepata mikopo ya elimu ya juu kwa wakati kwa sababu ya watendaji wabovu kama wa Baraza la Mitihani. Kila mwaka wanafunzi watajinyonga kwa matokeo mabaya yanayosabibishwa na usahihishaji wa baraza ambao labda hata taaluma zao ni dhaifu.

Nashauri serikali wangechunguza background za taaluma za viongozi wa Baraza la Mitihani, nina wasiwasi kuwa ni fake).

Wanasiasa mhakikishe kuwa mnawadhibiti watendaji wote wabovu kulinda heshima ya taifa. Bravo Politicians.

Mzee wa kuchora zombie naona umeamua kujitokeza jumvini.
 
Ndalichako endelea kunyonga waislam na hiyo kamati yako ya kutunuku!
Na wote wanaokusifia ni wale wote ambao hawautakii mema uislam na waislam hapa tz.

Peleka udini wako huko huko usituletee hapa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
tuache hayo mengine ambayo ndalichako anayafanya kwa siri dhidi ya waislam,
nyinyi ambao mnamtetea ndalichako vp hii kashfa ya mtihani wa somo la islamic knowledge?
Mpaka waislam walivyotishia kwenda mahakamani ndio tume ikaundwa na kugundulika kuna makosa,
tukazugwa kuwa mkuu wa kitengo cha teknohama amefutwa kazi lakini wapi!
Jamaa kakaa mtaani kidogo tu.
Sasa hivi yupo ofisini anaendelea na maisha.
Marehemu kigoma malima allah amrehemu alifuta mpango wa kufanya mtihani kwa majina na kuweka mpango wa namba sababu waislam walikuwa wanadhulumiwa.
hili la juzi

Mimi huwq ninawashangaa sana haqa ndugu zangu Waislamu. Hivi mtu akipata A kwenye Islamic Knowledge anafaidikaje katika kuendelea elimu ya juu? Kama lile kosa lingetokea kwenye somo jingine ningeelewa wakipiga kelele. Lakini kwa hili siwaelewi kabisa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Shafiri
Huyu mama anajipalia makaa. Ametoa kauli hiyo wakati tayari kuna kikundi maalum cha wanasiasa kilichoundwa kumshughulikia kutokana na misimamo yake. Hivi sasa kuna mpango wa kuandaa maandamano makubwa ya kumng'oa unaoratibiwa na wanasiasa na tayari kuna uhamasishaji mkubwa unafanyika.

Mkuu Shafiri, hivi watu hawaelewi kwamba Tanzania ikileta siasa kwenye mitihani basi itakuwa imejiua yenyewe? Thamani ya elimu yetu itakuwa imeshuka Kimataifa? Na hata wanasiasa wetu watakuwa wanyonge kimataifa? Watoto wanapojinyonga kwa kufeli mtihani ni kutokana na kulelewa vibaya n kukosa elimu bora. Watoto waliopata elimu bora na mitizamo bora na maadili mema hawawezi kukata tamaa hata kufikiria kujinyonga. Mtoto aliyepata elimu stahiki haswa haswa atajua kwamba kufeli mtihani darasa la saba au kidato cha nne/sita sio mwisho wa kusoma kwa sababu unaweza kusoma bila kupitia mikondo ya darasani hadi ukapata shahada ya Chuo Kikuu ambako ndiko shule huishia.
Si sahihi kumshambulia Dr Ndalichako kwa sababu yeye hutoa utahini tu kama vile CAG anavyotoa hati chafu na safi ya matumizi ya fedha za serikali. Dr Ndalichako anavyotoa matokeo na kulaumiwa kama yanakuwa mabovu mnamsumbua bila sababu. Kwa mfano marekebisho ya gheresha yaliyofanyika kwa mitihani ya kidato cha nne ya hivi karibuni yalitoa darajala A wangapi? Kushuka kwa elimu hakutokani na matokeo ya mtihani tu. Mchawi anayeloga wanafunzi waweze kufaulu au kufeli ni mwalimu wake na uwepo au kutokuwepo kwa vitabu. Sasa hao wachawi wapo wa kutosha huko shuleni? Ni Dr Ndalichako ndiye anawapeleka? Mbona watanzania wanampangia Dr Ndalichako majukumu ambayo siyo yake? Wanataka aachie waibe mitihani na kuvujisha kama zamani, kabla ya yeye kuingia NECTA? Tafadhali tusirudishwe tulikotoka. Hatujasahau bado kadhia ile. Kuna Maofisa Elimu wa Mikoa na Wilaya waliwahi kupoteza kazi kwa kuvujisha mitihani. Kumzonga Dr Ndalichako ni kumtisha, aogope na alegeze kamba watu wauze mitihani, Tanzania ipate wataalamu feki (walimu, madaktari, mainjia, wanasiasa, wafanyakazi feki na mwisho wakulima feki). Mimi naomba tumwache Dr Ndalichako afanye kazi. Ni mtanzania anayetaka kuona Tanzania ina wataalamu wenye uwezo wa kushidana na wale wa kutoka mataifa mengine duniani.
 
tuache hayo mengine ambayo ndalichako anayafanya kwa siri dhidi ya waislam,
nyinyi ambao mnamtetea ndalichako vp hii kashfa ya mtihani wa somo la islamic knowledge?
Mpaka waislam walivyotishia kwenda mahakamani ndio tume ikaundwa na kugundulika kuna makosa,
tukazugwa kuwa mkuu wa kitengo cha teknohama amefutwa kazi lakini wapi!
Jamaa kakaa mtaani kidogo tu.
Sasa hivi yupo ofisini anaendelea na maisha.
Marehemu kigoma malima allah amrehemu alifuta mpango wa kufanya mtihani kwa majina na kuweka mpango wa namba sababu waislam walikuwa wanadhulumiwa.
hili la juzi
Waziri Kawambwa ana jibu hili juu ya huo Mtihani wa Islamic Knowledge:

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MALALAMIKO DHIDI YA MATOKEO YASOMO LA ISLAMIC KNOWLEDGE KATIKA MTIHANI WAKIDATO CHA SITA 2012
1.0 UTANGULIZI
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha sita 2012 yaliyotangazwa rasmi tarehe 01/05/2012. Tarehe 28/5/2012 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipokea barua kutoka Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu yenye Kumb. Na. BSK/W/012/01 ya tarehe 22/5/2012 iliyoeleza kutoridhika na ufaulu wa watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge kwa kuwa waliona matokeo yaliyotangazwa hayakuwa na uhalisia wa uwezo wa wanafunzi. Kutokana na barua hiyo, Serikali ilifanya uchunguzi kwa kuangalia mambo yafuatayo:

. Kulinganisha alama za watahiniwa zilizojazwa katika vituo vya usahihishaji mitihani na zile zilizohifadhiwa katika Kompyuta, yaani database ya Baraza la Mitihani ili kubaini kama kuna tofauti yoyote; na
. Kulinganisha alama za somo la Islamic Knowledge zilizochakatwa na Mfumo wa Kompyuta na sampuli ya alama zilizokokotolewa kwa kutumia kikokotozi (calculator).

2.0 MATOKEO YA UCHUNGUZI
. Baada ya kupitia hatua za uhakiki kuhusu usahihishaji na utoaji wa matokeo, ilibainika kuwa alama za mwisho katika somo la Islamic Knowledge zilizokokotolewa na Mfumo wa Kompyuta ZILITOFAUTIANA
na alama zilizopatikana kwa kutumia kikokotozi. Uchunguzi zaidi uliofanyika kwa lengo la kubaini chanzo cha tatizo katika uchakataji wa matokeo hayo kwenye Mfumo wa Kompyuta ulionesha kuwa uchakataji uliotumika awali kutoa matokeo ya mwaka 2012 ulitumia jumla ya “Paper” tatu kama ilivyokuwa mwaka 2011.
. Kutokana na mabadiliko ya Fomati ya Mtihani wa somo la Islamic Knowledge yaliyoanza kutumika rasmi katika Mtihani wa Kidato cha Sita 2012, mtihani huo kwa sasa una “paper” mbili na siyo “paper” tatu.

Hivyo, tofauti ya alama iliyobainika imetokana na Mfumo wa Kompyuta kuendelea kutumia “paper” tatu katika kupata wastani wa alama za mwisho badala ya kutumia “paper” mbili.

3.0 HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI
. Baada ya kugundua dosari hiyo kwa somo la Islamic Knowledge, uhakiki ulifanyika kwa masomo yao yote ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2012 yaliyokuwa na “paper” zaidi ya moja ili kujiridhisha endapo uzito sahihi ulitumika katika kupata wastani wa alama za watahiniwa. Matokeo ya uhakiki huo yalionesha kuwa alama sanifu zilizokokotolewa na mfumo wa kompyuta ni sawa na alama zilizokokotolewa na Kikokotozi. Hivyo hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo mengine.
. Matokeo ya somo la Islamic Knowledge yaliyotangazwa awali yamerekebishwa kwa kutumia Paper mbili kama inavyotakiwa ili kuendana na mabadiliko ya Fomati ya somo hilo. Marekebisho hayo yaliridhiwa na Baraza la Mitihani katika Kikao chake Maalum kilichofanyika tarehe 31/05/2012. Aidha, Kikao kati ya wajumbe wa Baraza la Mitihani na wawakilishi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu kilifanyika tarehe 31/05/2012 ambapo walielezwa kuwa Wakuu wote wa Shule wenye watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge wataandikiwa barua rasmi kufahamishwa kuhusu marekebisho yaliyofanyika na barua hizo ziliandikwa tarehe 01/06/2012. Pia walifahamishwa kuwa matokeo yao yote ya masomo mengine hayana dosari yoyote na yanabaki kama yalivyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania. Matokeo hayo yamewekwa kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani na pia yatatangazwa kwenye magazeti.
. Pamoja na marekebisho hayo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaunda Kamati ya wataalamu kuiwezesha serikali kujiridhisha zaidi na hatua zilizochukuliwa na Baraza la Mitihani ili kuepuka dosari ya aina hiyo isijitokeza tena kwa siku zijazo.
. Viongozi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu waliridhika na hatua zilizochukuliwa na Wizara na wameandika barua ya kuishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu namna walivyoshughulikia malalamiko yao.

4.0 HATMA YA WANAFUNZI WALIOREKEBISHIWA MATOKEO KATIKA MAOMBI YA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU
Wizara inapenda kuwahakikishia watahiniwa waliorekebishiwa matokeo yao kwamba, kwa kuwa zoezi la usajili bado linaendelea hadi tarehe 30/06/2012, waliorekebishiwa matokeo yao watapata fursa ya kuwasilisha maombi ya kujiunga na vyuo vikuu endapo wana sifa stahiki. Aidha, kwa upande wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, maombi ya mikopo hufanyiwa kazi rasmi baada ya Tume ya Vyuo Vikuu kukamilisha mchakato wa udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu. Hivyo, hapatakuwa na athari yoyote kwa watahiniwa husika kupata mikopo endapo watakidhi vigezo vinavyotakiwa.

5.0 HITIMISHO
. Napenda kuhitimisha kwa kuwasihi wazazi, walezi, wanafunzi na jamii kwa ujumla kuwa na imani na Baraza la Mitihani la Tanzania kama chombo chetu chenye dhamana kisheria ya kuendesha mitihani nchini. Hapakuwa na hujuma yoyote iliyofanyika kwa watahiniwa ambao matokeo yao yamerekebishwa. Kosa lililojitokeza ni la kibinadamu, halikufanywa kwa makusudi wala kwa lengo lolote la kuhujumu kundi fulani la watahiniwa. Marekebisho yameshafanyika na matokeo stahiki yameshatolewa. Aidha, uhakiki uliofanyika kwa masomo yao mengine unaonesha kuwa hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo yote.
. Kutokana na dhana ya baadhi ya watu kuwa kunakuwa na upendeleo kwa baadhi ya watahiniwa wa makundi fulani katika usahihishaji napenda kuwakumbusha kuwa wakati wa mitihani, watahiniwa huandika namba zao za mitihani na siyo majina. Katika taratibu za usajili wa Baraza la Mitihani hakuna kipengele chochote kinachomtaka mtahiniwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa. Vilevile, utaratibu unaotumika kuwapata wasahihishaji huzingatia uwezo wao kitaaluma na uzoefu kazini. Aidha, katika fomu ya mapendekezo ya uteuzi wa wasahihishaji hakuna mahali popote ambapo Mkuu wa Shule
hutakiwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa ya mwalimu anayependekezwa kusahihisha mitihani.
. Utaratibu unaotumika kusahihisha mitihani hautoi mwanya wa upendeleo. Katika kudhibiti uwezekano wa kupendelea mtu yeyote kila msahihishaji husahihisha swali moja tu na kisha humpatia msahihishaji mwingine asahihishe swali linalofuata. Aidha, kila msahihishaji hutakiwa kuweka vifupisho vya majina yake (initials) ili ufuatiliaji uweze kufanyika kadri itakavyohitajika. Pia uhakiki wa usahihishaji hufanyika kwa lengo la kujiridhisha na usahihi wa kazi na kuhakikisha kuwa kila mtahiniwa amepata alama anazostahili. Dosari zinazobainika zimekuwa zikirekebishwa katika mchakato wa usahihishaji na wasahihishaji wanaobainika kuhusika na dosari hizo wamekuwa wakichukuliwa hatua stahiki mara zinapobainika.
. Pamoja na hayo niliyoyaeleza nina taarifa kuwa yanapangwa maandamano ambayo yanalenga suala hili hili la kutoridhika na matokeo ya awali ya somo la Islamic knowledge. Kwa kuwa suala hili limeshapatiwa ufumbuzi, nawasihi wananchi wajiepushe kushiriki maandamano hayo kwa sababu suala la msingi lililo wafanya watake kuandamana limeshatolewa maelezo. Hivyo, maandamano hayo hayatakuwa na tija.

IMETOLEWA NA DKT SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAREHE 07/06/2012
 
]
Kweli kabisa kwani ameweza kukiendeleza kile kilichoasisiwa na wenzake cha kukandamiza jamii flani na kuipendelea nyingine

Acha wivu wa kike mamdogo Ndalichako is the best mathematician and she always stands on what she believe that is true.
 
na mwaka huu mtakoma na uislam wenu. Hivi maprofesa wote na dr wote hawa tz nyie mna hao tu? Shule, hospitali, na vyuo mna
Ha ha ha!
Wapo wengi sana lakin nje ya nchi wamejichanganya na wametulia tu, subiri uraia pacha uruhusiwe ndio utakapowaona Waislamu wasomi wakija kufanya vitu.
 
Ndalichako is one of the best brains in Tanzania for your information. Acha afanye kazi yake, maana yupo sahihi kabisa. Keep it up Joyce.

Aaah fantastic. Basi kama huyu best brain naona nchi imejaa mambumbu. Udaktari wake na wasiwasi ni ule wa kufanyiwa thesis au jamaa walipata sana mpaka wakamaward hiyo PhD.
 
Ha ha ha!
Wapo wengi sana lakin nje ya nchi wamejichanganya na wametulia tu, subiri uraia pacha uruhusiwe ndio utakapowaona Waislamu wasomi wakija kufanya vitu.
Kwa kadiri ya mawazo yako CV ya Katibu Mtendaji mpya wa NECTA, haitaji elimu yoyote wala uadilifu wowote. Anahitajika tu ahakikishe pasi za Wakristo na Waislamu zinalingana. Bila kuangalia uhalisia.

Hapo ndipo atakuwa anatenda haki.
 
Aaah fantastic. Basi kama huyu best brain naona nchi imejaa mambumbu. Udaktari wake na wasiwasi ni ule wa kufanyiwa thesis au jamaa walipata sana mpaka wakamaward hiyo PhD.
Kwa taarifa yako Dr. Ndalichako tangu anasoma Tabora Girls yeye ni best student Form IV 1982 na Form VI 1985. Uliza yeyote aliyepitia huko nyakati hizo.

University of Dar es Salaam alisoma Bachelor of Education (Mathematics) akapata First Class. Wakati anafanya final Exams za mwaka wa mwisho alikuwa mgonjwa, akalazimisha afanye akitokea Dispensary na akapata A zote. Waliosoma naye UDSM na kumaliza 1990 watashuhudia.

Alipata Scholarship kwenda kusoma Alberta University, Edmonton - Canada, na huko amesomea mambo ya Mitihani (Educational Evaluation and Measurement) MSc. na PhD. Amefundisha UDSM tangu 1996 mpaka alipochaguliwa kuwa ES wa NECTA.

Mpaka sasa hapa Tanzania ni yeye peke yaka ana PhD ya Educational Evaluation and Measurement.

Wakati akiwa UDSM amekuwa Director wa University Consultancy Bureau (the post that is reserved for the smartest), amekuwa Head wa Department ya Educational Psychology, amekuwa consultant wa JICA, UNESCO na UNICEF.

Wakati Luhanga ni VC Dr. Ndalichako ameteuliwa kwenye tume nyingi tu kuchunguza na kushauri mambo ya dharura.

I am 100% sure that, anybody who knows Dr. Ndalichako will not doubt about her competency. But if you wait for these
attachment.php


attachment.php


attachment.php



You will always doubt. Because you just let others think and decide for you.
 
Mkataa pema pabaya panamwita! Watanzania tumeamua kukataa mema kwa kuwashambulia watendaji mahiri na wenye kujituma sasa tusubiri matokeo ya mbegu hizi tulizopanda
 
Ha ha ha!
Wapo wengi sana lakin nje ya nchi wamejichanganya na wametulia tu, subiri uraia pacha uruhusiwe ndio utakapowaona Waislamu wasomi wakija kufanya vitu.

rubish....mbona hao watoto wa kiislamu wanaosoma shule za serikali, kikristu za watu bnafsi wanafaulu vyema tu...angalieni aina yawaalimu mnaoajiri na ratibisheni wanachofundisha....
 
na mwaka huu mtakoma na uislam wenu. Hivi maprofesa wote na dr wote hawa tz nyie mna hao tu? Shule, hospitali, na vyuo mna

Ungekuwa umenielewa ungeandika hivi '' HAO WALISOMA WAKATI WA MUASISI WA MFUMO KRISTO NYERERE''
 
Ndalichako endelea kunyonga waislam na hiyo kamati yako ya kutunuku!
Na wote wanaokusifia ni wale wote ambao hawautakii mema uislam na waislam hapa tz.
Nchi hii waislamu wanaonewa mpaka kwenye virabu vya pombe. Nchi hii waislamu wataachwa kuonewa pale viongozi wote wa seikalini watakapokuwa waislamu tena wenye msimamo mkali. Ebu cheki sasa hivi rais muislamu, makamu muislamu na waziri wa ELIMU ambaye ndiyo mtendani mkuu wa wizara ni muislamu bado watu wanalalamika kuonewa. Juma mtanda ambaye alikuwa mwalimu wangu wa Gs pale kwiro high school anaelewa kwa mfumo wa usahihishaji wa mitihani haiwezekani kumpendelea mtu maana hakuna jina la mtu linaloandikwa kwenye mitihani wowote. Katika kusahihisha mtihani kila msahihishaji husahihisha swali moja tu hivyo hakuna namna ya kumpendelea mtu. Other wise mseme wanafunzi wa kiislamu wawe wanatungiwa mitihani ya kwao itakayekjwa rahisi rahisi hilo linawezekana kuwafikiria maana wanapoteza muda mwingi kwenye madrassa. Mitihani yako ya kumaliza ELIMU ya msingi itungwe kwa mfano wa shwali hili

mfano: Rais wa kwanza wa Tanzania aliitwa mwalimu Julius Kambarage Nyere-- (a)lra. (b) re. (c) ru (d) ro
Hapa watafaulu wote.
 
Juma mtanda ambaye alikuwa mwalimu wangu wa Gs pale kwiro high school anaelewa kwa mfumo wa usahihishaji wa mitihani haiwezekani kumpendelea mtu maana hakuna jina la mtu linaloandikwa kwenye mitihani wowote. Katika kusahihisha mtihani kila msahihishaji husahihisha swali moja tu hivyo hakuna namna ya kumpendelea mtu. Other wise mseme wanafunzi wa kiislamu wawe wanatungiwa mitihani ya kwao itakayekjwa rahisi rahisi hilo linawezekana kuwafikiria maana wanapoteza muda mwingi kwenye madrassa. Mitihani yako ya kumaliza ELIMU ya msingi itungwe kwa mfano wa shwali hili

mfano: Rais wa kwanza wa Tanzania aliitwa mwalimu Julius Kambarage Nyere-- (a)lra. (b) re. (c) ru (d) ro
Hapa watafaulu wote.
Waislamu hawalalamikii usahihishaji!

Ningekushauri uyapitie madai ya Waislamu kupitia vyombo vya Waislamu,
 


Kuna watu, kama Ndalichako wanasema eti wanasiasa wasiingilie kazi za elimu. Watendaji wa elimu wafanye wanavyotaka, wanasiasa wanyamaze tu, hata kama watendaji wamefanya madudu. Kutakuwa na umuhimu gani wa kuwa na wanasiasa? Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani anaongea sana kwa kujihami sawa na wanasiasa halafu haitaki siasa. Yeye ndiye mwanasiasa namba moja. Hatujawahi kuona Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani anayeongea ongea sana kama huyu.

Watendaji katika Wizara mbalimbali kama vile Elimu hususani Baraza la Mitihani wanavurunda kazi (mitihani) kila kukicha, wananchi na wabunge wanalalamika, wao kwa kujihami wanataka wasiingiliwe na wanasiasa. Je, kukosolewa ni kuingiliwa utendaji wao? Ukatibu utendaji SIO taaluma, ni cheo cha kupewa tu. Baadhi ya viongozi wa Baraza la Mitihani achieni ngazi kulinda heshima zenu.

Isingekuwa wanasiasa hadi leo kusingekuwa na sekondari za kata, wanafunzi wasingepata mikopo ya elimu ya juu kwa wakati kwa sababu ya watendaji wabovu kama wa Baraza la Mitihani. Kila mwaka wanafunzi watajinyonga kwa matokeo mabaya yanayosabibishwa na usahihishaji wa baraza ambao labda hata taaluma zao ni dhaifu.

Nashauri serikali wangechunguza background za taaluma za viongozi wa Baraza la Mitihani, nina wasiwasi kuwa ni fake).

Wanasiasa mhakikishe kuwa mnawadhibiti watendaji wote wabovu kulinda heshima ya taifa. Bravo Politicians.

nDUGU YANGU KWA JINSI MATE YANAVYOKUTOKA UTAFIKIRI UNATAKA KUKALIA KITI HICHO, SUBIRI SIKU IKIFIKA UTAPEWA.
 
Ndalichako endelea kunyonga waislam na hiyo kamati yako ya kutunuku!
Na wote wanaokusifia ni wale wote ambao hawautakii mema uislam na waislam hapa tz.

kama unafamilia naisikitikia sana. hv kwanini mnatanguliza huu udni wenu sana

Hivi akili yako ikosawa kweli? unajua majukumu ya baraza la mitihani! unayajua majukumu ya joyce ndalichako kwenye baraza hilo?

moja yashule za kiislam TAQWA sec hapo mwnza mbona zpo vizuri tu toka zamani! badala yakutafuta sababu rudini kwenye shule zenu mjitazame

huyu mama ni best ever! kama mnataka kufaulu burebure muue elim kwa sabab ya dini shame on you
 
Back
Top Bottom