Joto la uchaguzi Arumeru Magharibi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joto la uchaguzi Arumeru Magharibi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Mar 31, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Leo kwenye uwanja wa Azimio la Arusha kulikuwa na zoezi la kumsimika Bwana Godluck Ole Medeye ukamanda wa vijana Arumeru magharibi.Bwana G Medeye tayari katangaza atagombea ubunge katika jimbo la Arumeru magharibi linaloshikiliwa na Mheshimiwa Elisa Mollel.

  Sherehe zilianza na maandamano makubwa ya wafuasi wa Bwana Godluck ole Medeye waliokuwa wamevalia fulana zenye picha zake.


  Bwana Medeye ni mkurugenzi wa rasilimali watu Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) ana shahada ya uzamili MBA.Bwana Medeye ni mfuasi mwaminifu wa Edward Ngoyai Elowassa.

  Siasa za chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha na Manyara zimegawanyika katika makundi mawili makubwa.

  Kundi la kwanza ni lile la wabunge/wanasiasa wanaomuunga mkono Mheshimiwa E Lowassa.Kundi la pili ni lile la wabunge/wanasiasa wanampinga Lowassa likiongozwa na Mheshimiwa sendeka,Lekule Laiser,Elissa Mollel ambao wameunda mtandao wa kuwakinga dhidi ya mashambulizi ya Mheshimiwa Lowassa & Company.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ole Medeye aliwahi kuwa afisa utawala ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha miaka ya 80s na 90s alikuwa na nyodo sijui kabadilika nili nawashangaa watu wanampapatikia.

  Hafai kuwa mbunge huyu ni opportunist hana lolote leo kagawa mafulana ya kuwadanganya waarusha masikini ili awe mbunge.
   
 3. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Arusha James Ole Millya katumwana na Lowasa kumsaidia Ole Medeye awe mbunge wa Arumeru magharibi.
   
 4. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  UTEUZI wa nafasi za makamanda wapya wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkoa wa Arusha umekumbwa na "mauzauza" na malalamiko kutoka kwa wanachama wa jumuiya hiyo kwa kile kindachodaiwa kuwa viongozi kuwateua makamanda hao kwa malengo yao ya kisiasa.

  Tayari uteuzi huo umezua mgogoro mkubwa ndani ya jumuiya hiyo mkoani hapa ambapo baadhi ya viongozi wamekuwa wakionekana kupingana hadharani na maamuzi ya kamati ya utekelezaji ya mkoa.

  Wanaolalamikia uteuzi uliofanywa katika nafasi hizo ni wanachama, wajumbe wa Baraza Kuu na baadhi ya viongozi wa kamati za utekelezaji za wilaya na mkoa ambao wanadai hawakushirikishwa katika maamuzi hayo.

  Viongozi hao pia wanadaiwa kukiuka baadhi ya taratibu na kanuni katika uteuzi huo bila kufanya vikao vinavyotakiwa kwa mujibu wa kanuni hizo.

  Uteuzi unaolalamikiwa na vijana hao ni nafasi ya makamanda wapya kwa wilaya za Arumeru, Arusha na pia uteuzi wa nafasi hiyo kwa Mkoa wa Arusha.

  Katika Wilaya ya Arumeru, jumuiya hiyo imemteua Goodluck Ole Medeye kuchukua nafasi ya mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi, Elisa Molell aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

  [​IMG]

  Mbunge wa Arumeru Magharibi, Elisa Molell

  Medeye, ambaye ni Mfanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imeelezwa kuwa atawania nafasi ya ubunge katika jimbo la Arumeru Magharibi, na tayari anaendesha kampeni za chini kwa chini kuhakikisha kuwa Mollel harudi katika kiti hicho.

  Hata hivyo, Medeye bado hajapitishwa na Baraza Kuu la vijana wa wilaya hiyo ambalo tayari limeandika barua ya malalamiko kwenda makao makuu ya Jumuiya ya Vijana wakilalamikia kukiukwa kwa kanuni na taratibu za kumteua.

  Habari ambazo, hata hivyo, hazikuthibitishwa zilieleza kuwa Makao Makuu ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana tayari wameandika barua na kuwaelekeza viongozi wanaohusika kuanza upya mchakato wa kumtafuta kamanda wa wilaya.

  [​IMG]

  Mbunge wa Arusha mjini, Felix Mrema

  Uteuzi mwingine unaolalamikiwa ni wa nafasi ya ukamanda wa wilaya ya Arusha ambapo viongozi wa wilaya hiyo wamemteua Diwani wa Kata ya Olorien, Gaudance Lyimo kuchukua nafasi ya Felix Mrema.

  Vijana hao pia wanalalamikia uteuzi wa Anoj Shah mwenye asili ya Kiasia kuwa Kamanda wa Mkoa wa Arusha na kumtosa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Abrahman Kinana aliyekuwa kamanda kwa miaka 10.

  Wakizungumza na Raia Mwema mwishoni mwa wiki, kundi la vijana hao kutoka wilaya za Arusha na Arumeru ambao waliomba majina yao yahifadhiwe kwa sasa, walieleza kuwa viongozi wa jumuiya hiyo katika wilaya hizo na wale wa mkoa wamekiuka taratibu na kanuni katika uteuzi.

  Wakitoa mfano, vijana hao walieleza kuwa katika wilaya ya Arumeru, Katibu wa UV-CCM, Yasin Said Yasin aliteua jina la Medeye kwa maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Arusha, James Ole Millya bila ya kuwashirikisha viongozi wengine.

  "Hata Mwenyekiti wa UV-CCM wilaya ya Arumeru, Esther Maleko hakushirikishwa katika uteuzi huo na jina la Medeye lilipelekwa moja kwa moja makao makuu; huku viongozi wakikata jila la Elisa Mollel", alieleza mmoja wa vijana hao.

  "Viongozi wameondoa majina ya wabunge wawili (Felix Mrema, Elisa Mollel) kwa malengo ya kisiasa ili kuwanufaisha kisiasa wapinzani wao wanaotaka kugombea ubunge katika majimbo hayo mawili", alieleza.

  Mwanachama mwingine alidai kuwa viongozi hao wamefanya uteuzi huo kwa lengo la kuwaridhisha viongozi wa kisiasa na uteuzi huo pia umelenga kuwajenga kisiasa walioteuliwa ambao wana nia ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwakani.
  "Maamuzi haya yamefanyika bila kuzingatia maslahi ya vijana ila kwa lengo la kuwaridhisha viongozi wa kisasa katika mkoa wa Arusha ambao ndiyo wamekuwa wakiwafitini wenzao", alisema mjumbe huyo huku akisita kuwataja viongozi hao.

  Aidha, vijana hao pia wamelalamikia uteuzi wa nafasi ya Kamanda wa Mkoa wa Arusha ambapo habari zinadai kuwa nafasi hiyo amepewa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya utengenezaji vyandarua na bidhaa mbalimbali za plastiki, Anoj Shah mwenye asili ya Kiasia.

  [​IMG]

  Kinana, Mjumbe wa Kamati Kuu

  "Haingii akilini eti umwondoe Mzee Kinana ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na ana uzoefu mkubwa katika masuala ya Chama na kisha kumteua mfanyabiashara ambaye inawezekana hata si mwanachama wa CCM……sijui chama chetu kinaelekea wapi"?, alihoji mmoja wa vijana hao.

  Vijana hao pia wanamlalamikia Mwenyekiti wao Millya kuwa anatumiwa na baadhi ya wanasiasa wenye majina makubwa kuvuruga jumuiya hiyo kwa malengo ya kisiasa.

  Wanasema kwamba ili kufanikisha malengo yake amekuwa akiwatisha vijana wanaohoji masuala mbalimbali kuwa atawafungulia kesi polisi.

  "Hivi karibu Millya aliwatishia wajumbe wa wilaya ya Arumeru kuwa wale wanaopinga uteuzi wa Medeye watachukuliwa hatua za kisheria na wengine wataitwa kuhojiwa na kamati ya utekelezaji na kuchukuliwa hatua za kinidhamu…. sasa hapa demokrasia iko wapi", alisema kijana huyo kwa masikitiko.

  Akizungumzia malalamiko hayo, Katibu wa UV-CCM wilaya ya Arumeru, Yasin Said Yasin alieleza kuwa wanaolalamika hawana hoja za msingi kwa kuwa wao walifuata taratibu zote katika kufanya uteuzi wa Medeye.

  Akifafanua taratibu hizo, Yasin alieleza kuwa viongozi walipendekeza majina matatu ambayo ni ya Medeye, Mollel na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jeremiah Sumari ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi.

  "Majina hayo matatu ndiyo yaliyojadiliwa na Kamati ya Utekelezaji na kupelekwa mkoani ambao nao waliyapeleka Umoja wa Vijana Taifa na baada ya kuchujwa jina la Medeye ndilo lililorudishwa na kwa sasa tunasubiri Baraza Kuu likae ili limpitishe rasmi kuwa Kamanda wa Wilaya", alisema Katibu huyo.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UV-CCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya alieleza kuwa mgogoro huo unakuzwa na baadhi ya wanachama wakorofi, na kwamba uteuzi wote ulipita kwenye vikao halali vya jumuiya hiyo.

  "Kama viongozi wanaolalamika wana hoja za msingi, basi wawe jasiri na wajitokeze hadharani na sisi tutawajibu kwa hoja; kwani tunaamini kuwa tulizingatia vigezo vyote muhimu katika uteuzi", alisema Millya.

  Millya, ambaye ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Simanjiro linaloshikiliwa na Mbunge machachari, Christopher Ole Sendeka alisema kwamba Kamanda aliyeteuliwa kushika nafasi ya mkoa pia ana uwezo mkubwa.

  "Tumemwondoa Kinana kwa kuzingatia majukumu mengine mazito aliyonayo katika chama na anaweza kukosa muda wa kuhudumia vijana kutokana na majukumu hayo, na huyu tuliyemteua tunaamini ana uwezo mkubwa", alisema.

  Hata hivyo, wakati Millya akisema kuwa Kinana ana majukumu mengine na anaweza kukosa muda wa kuwahudumia vijana wa mkoa wa Arusha, Shah ambaye ni mfanyabiashara maarufu mjini Arusha, mara nyingi huishi nje ya nchi na amekuwa akitumia muda mwingi katika shughuli zake za kibiashara.

  Wanaoteuliwa kuwa makanda wa jumuiya za vijana mara nyingi huwa na majukumu ya kusadia kifedha shughuli mbalimbali za vijana na pia kusuluhisha migogoro inayotokea ndani ya jumuiya na kuimarisha CCM katika ngazi zote.

  Nafasi hizo pia zina ushawishi mkubwa miongoni mwa vijana; hasa nyakati za kampeni za uchaguzi wa nafasi mbalimbali za ndani ya chama na ile ya ubunge, na ndiyo maana uteuzi unaofanywa huleta malalamiko na hata vurugu katika maeneo mengine.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Umasikini wa fulana utawamaliza Wana-Arusha!

  Elisa Mollel si mbunge mzuri anyway na ameshapatikana na kashfa ambazo japo hazikumtia hatiani, lakini hata hivyo nafasi yake haimfai Madeye ambaye anaonekana kuja na gia ya kutanguliza fedha na bling bling za buku-jero kwa masikini!
   
 6. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako PakaJimmy,

  Jana nilishuhudia wafuasi wa Bwana Ole Medeye wakitwangana makonde maeneo ya uwanja wa Sheckh Amri Abed mpaka polisi wakaingilia kati.

  Nashindwa kuelewa sheria ya kudhibiti rushwa katika uchaguzi itakavyofanyakazi kwasababu jana fedha zilikuwa zinagawanywa hadharani.
   
 7. k

  kay1 Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu madeye alikuwepo tcra, ni fisadi jingine , kala sana pale sasa anagawa hela arusha ambazo kachota tcra, siku zake zinahesabika. Ni mshenzi sana sana mimi ni mmaasai na ninamjua fika huyu bwana. Huko bungeni patakuwa padogo yani ni copy and paste ya lowassa
   
 8. k

  kay1 Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Madeye hafai kaulizeni wafanyakazi wenzake pale tume. Ana wafuasi wake pale tume ya mawasiliano . Ni mfitina na anapika majungu ile mbaya. Muogopeni sana ana chuki mno mno
   
 9. k

  kay1 Member

  #9
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yani mara mia afadhali ya lowassa kuliko huyu. Kuna uncle mmoja pale tcra kila mtu anamjua ni moto wa kuotea mbali lakini alimpokonya nafasi yake ya kazi baada ya huyu uncle kwenda kuongeza ujuzi huko majuu , akampa kilaza mmoja mpare ambaye kashindwa kazi ttcl. Ni mshenzi sanaaaaaaaaaaa huyu baba. Hafai kabisa anachezea maisha ya watu hivi hivi . Mwehu sana huyu
   
 10. k

  kay1 Member

  #10
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yani ana nyodo ya fedha acha maslaha, lakini huko alikokwenda ndio atajua kama nyanya ni mboga au kachumbari..... Ni katili sana nimepata nyepesi nyepesi zake. Ni katili noma . Yani ofisi aliigeuza kuwa nyumbani kwake mshenzi sana, watu wanasheherekea kuondoka kwake.... Mwizi, fisadi lingine hilooooooooooooooooooooo. Ni jirani yetu hapa ni kweli kamwaga hela sana za rushwa. Swali kazitoa wapi?
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  MKuu Ngongo,
  Tutafutane mkubwa tukasherekee ukombozi wa jimbo letu la Arusha mh. God Bless Lema.......
   
 12. k

  kay1 Member

  #12
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh hii jamiiforum ni kiboko... yani mdau unachosema hapo juu ni kweli kabisa, huyo uncle wa TCRA nampata fika ana nyumba Masaki na muda mwingine huwa anaishi Masaki ila familia yake ipo Mbezi Beach kwahiyo anaendaga Mbezi Beach pia kupumzika na familia yake. Yani nampata kinoma.

  Mke wake alikufa muda, sasa akaoa mwingine ila ana watoto wawili wako uingereza ila mmoja aliondoka mwaka wa jana, wacha arudi tumvishe pete wabongo. Yeah huyo mpare nampata pia mfupi na anaongea haraka utafikiri kasuku inawezekana ni kilaza kweli.... jamiiforum ni nooooomaaa mbaya watu wana data achaaaaa
   
 13. k

  kay1 Member

  #13
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Madeye yupi wanajamvini wenzangu? yule wa tcra? nchi imekwisha kama ndio yule yani ni rostam wa pili. tobaaaaaaaaaa
   
 14. k

  kay1 Member

  #14
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  In short, madeye hafai hivi mmeona hiyo rushwa aliyoitoa huko arusha? Yani elfu ilikuwa kama sh.100, we acha maslaha kabisa. Angalizo: Hela kapata wapi? Tume lazima iundwe kuchunguza hizi pesa
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kama majungu vile? hakuna ushahidi.
   
 16. k

  kay1 Member

  #16
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we unayesema hakuna ushahidi, unamjua madeye vizuri? na ushahidi upi unaotaka hapa. humu JF hakuna majungu ni ukweli tu. na hao akina lowassa mpaka kesho wanatuhumiwa wizi lakini wanataka ushahidi. unajua huyu mtu alichowafanyia watu huko alikotoka kabla ya kuwa mbunge? kaa kimya kama huna jipya:A S-baby:
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Asante kwa taarifa hii. Inasemekana kuwa habari hii ina ukweli kwa asilimia 98.
  Bungeni kafika na atakutana na vichwa vikali vya chadema. Atakufa kabla ya kufika mbali.
   
 18. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako crashwise,

  Mkuu nilishasheherekea tangu j3 lakini msimamo wangu kuhusu Godbless Lema uko pale pale.Kuna mambo unaweza kuyarekebisha kidogo hasa kipengele cha elimu tafadhali sana mshaurini Lema apige shule itakuja kumsaidia sana mbele ya safari kama atataka kuwa mwanasiasa mahiri.

  Mkuu nasikia Mama kakimbilia mahakamani tusipuuze hili limeshawahi kutokea enzi za Makongoro Nyerere uchaguzi ukirudiwa chance ya upinzani kushinda ni ngumu sana.Moja ya sababu kubwa nilizokuwa nikimtilia shaka Lema ni hii kuburuzwa mahakamani na ya pili ni kuuza ubunge nadhani utakubaliana na mimi J3 kama si wananchi kusimama imara ubunge ungekwenda CCM.

  Mkuu niko kwenye hatua za mwisho nitatoa ripoti jinsi kampeni za ubunge zilivyokwenda na kwanini Lema alishinda na Batilda na Lyimo walishindwa.Mkuu nategemea utatoa mchango wako bila ushabiki hasa ukizingatia tayari mbunge kashapatikana.
   
 19. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Medeye ni kibaraka cha EL
   
Loading...