CCM joto la 2020 lapanda kupita kiasi

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,247
24,113
Kipindi : Msumari wa Moto
OLE MEDEYE: RAIS KIKWETE ALITUVURUGA/LOWASSA HANA FEDHA/ALITAKA KUMBEBA MEMBE



Goodluck Ole Medeye alijiunga na Umoja wa Vijana wa 1968 uliofahamika kama TANU Youth League, 1977 aliiona CCM ikizaliwa kufuatia TANU na ASP kuungana. 1992 mfumo wa vyama vingi kuzaliwa.

Hivyo anaifahamu CCM kwa miongo zaidi ya mitano yaani miaka 52 sasa. Mwaka 2015 aliona na kushuhudia mvurugano ktk uteuzi wa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM . Ole Medeye anasema hakupata kuona hali hiyo ya mvurugano ndani ya CCM mwaka 1995, si 2000 wala 2005 hata 2010. Ila mwaka 2015 CCM iliyumba na kuacha kufuata katiba ya chama kanuni na mazoea.

Wabunge wa CCM Mpya hata ktk vikao vya ndani yaani party caucus huku milango na madirisha yamefungwa bila waandishi wa habari bado wanahofu na staili mpya ya kuweka nidhamu ndani ya chama hivyo wabunge wanaCCM hawawezi kumsema Waziri Mkuu au kumshauri Rais kwa kuogopa kukatwa majina yao 2020

Kwenye Msumari wa Moto wiki hii Charles William na David Rwenyagira wanakutana uso kwa uso na aliyekua Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pia Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi (2010 - 2015), Goodluck Ole Medeye ambaye anafunguka mengi kuhusu nyadhifa alizowahi kuzitumikia.

Ole Medeye ambaye kwa sasa ni mwanachama wa kawaida tu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), pia anakumbushia jinsi mchakato wa kuchuja wagombea Urais wa chama hicho mwaka 2015 ulivyosababisha mpasuko mkubwa miong
Source : Wasafi Media
 
Ccm ipate joto na ikibidi iyeyuke kabisa Kama ilivyokuwa KANU ya Kenya na isirejee tena tanganyika! Chama gani kinachoshindwa kuusimamia uchumi kwa miaka 50+ licha ya nchi kujaliwa raslimali lukuki? Kife kabisa tena kwa aibu!
 
Godluck Ole Medeye.

Nikimfahamu Ole Medeye kuanzia miaka 1990s wakati huo akifanyakazi ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha kama ofisa utawala/utumishi.

Nakumbuka wakati huo Mkuu wa Mkoa alikuwa Col Tarimo na RDD alikuwa Ritahiwa sijui kama jina liko sahihi sana.Ole Medeye alikuwa akisimamia idara ya afya katika masuala yote ya ajira,kupanda cheo na kuhamisha watumishi wa Idara ya Afya.

Ole Medeye aliacha kazi yake rasmi ya kusimamia Idara ya afya na kukimbilia kazi ya usaidizi Mkuu wa Mkoa.Watumishi wa Idara ya Afya walijikuta wakikosa msaada kwasababu Medeye mara nyingi alipenda kazi za kumsaidia Mkuu wa Mkoa kwakuwa zilikuwa na maslahi zaidi hasa safari za Wilaya mbali mbali.Ifahamike wakati huo Mkoa wa Arusha ulikuwa mkubwa kweli kweli kabla Mkoa wa Manyara haujazaliwa.

Katika mambo ambayo ninayakumbuka sana kuhusiana na Medeye ni tabia yake ya kujikweza,kudharau wengine na kupenda sana kuanzisha migogoro.Tabia hii pia ilijitokeza wakati akiwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Ardhi.

Kabila la Waarusha walikuwa na utamaduni wa kukutana eneo la Arusha Technical College ambalo ni maalumu kwa ajili ya mila zao_Ole Medeye akiwa Mbunge aliandaa mkutano kwa lengo la kupambana na Lema Godbless ambaye ni Mchagga kwamba wachagga wamejazana sana Arusha,wamenunua ardhi nyingi na kwamba sasa ni wakati wa waarusha kutawala mji wao.Hii vita inafanana kwa kiasi fulani vita aliyoianzisha Mbunge wa zamani Mzee Solomon Ole Saibul akitaka wachagga na wapare waondoke Arusha jambo ambalo Mwl Nyerere alilikataa kwa hoja nzuri na ndio ukawa Mwisho wa Ole Saibul kisiasa kwani aliyekuwa mshindani wake Marehemu Mzee Mbagga alimwangusha.

Ukifuatilia siasa za Ole Medeye utakuta ni mtu anayependa ukubwa,madaraka na kupata fursa za kiuchumi kupitia madaraka.Baada ya kujiunga CHADEMA alipewa fursa ya kugombea nafasi ya spika wa Bunge la JMT akashindwa kwakuwa wabunge wa CCM ni wengi.Ukinda mbele zaidi alihitaji kuwemo katika nafasi za ujumbe wa Kamati Kuu ya CDM alipoona hakupata nafasi akatimkia chama cha Mzee Mapesa (Cheyo).Akajitolea nyumba yake kwajili ya ofisi a chama na kuanza kujenga mizizi katika mkoa wake wa Arusha.Mzee Cheyo alipogoma kumwachia nafasi ya mwenyekiti akarejea CCM na sasa anataka ubunge na pengine uwaziri.

Ole Medeye ni mtu wa kupenda madaraka,kwasasa anaona fursa ipo CCM.Ni mtakie kila la heri katika safari yake.
 
Back
Top Bottom