Joto Dar

Magingil Magingila

New Member
Jan 3, 2016
4
1
Ndugu wana jf vipi hii hali ya joto la hapa jiji Dar es salaam! Imekuwa ikiongezeka siku hadi siku. Tatizo ni kukosekana kwa mvua? Au ndo mabadiliko ya tabia ya nchi kiujumla katika dunia? Mwenye weredi katika hili tujuzane
 
Joto limekuwa kali sana hata wenye mifugo wanalalamika mifugo inakufa kwa heat stress...Ni sheeda.
 
Mwaka huu utakuwa mwaka wenye joto zaidi kuliko mwaka mwingine wowote tangu dunia kuumbwa. Kiasi cha mvua pia kitakuwa juu ya kiwango hivyo kutakuwa na mafuriko kuliko yale yaliyotokea mwaka 1997/1998. Tutakuwa na majanga mengine kama vimbunga(tazama kinachotokea us na southern sea) . Hi ni kwa mujibu wa NASA.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
wa Dsm punguzeni dhambi! Poda ninyi! Umalaya ninyi! Dhulma ninyi! Wake za watu, waume za watu, ninyi! Ubadhirifu wa Mali ya Umma! Ulevi! Ujuaji! Utapeli! Umarioo! Wizi wa Kura!
 
Mabadiliko ya tabia nchi ni kitu cha kawaida joto sana baridi sana nk. Yote haya yanatokea na dunia inazidi kuumbika maziwa makubwa yanakauka na misitu inakauka kwa upande mwingine baada ya hili joto zitakuja mvua nyingi na mabwawa mapya yatajitokeza mito mipya itatokea yoote haya ni kuthibitisha kuwa uumbaji unaendelea hata baada ya wewe kufa.
 
Back
Top Bottom