Naanza kudoubt uwezo wa huyu kijana umbile la mtu haligawi nchi bali maneno ya mtu.Mimi naona bora anyamaze mambo ya poe kwanza.Mbowe mwambie afyate mdomo huyu kijana.
Ngoja niweke wazi kabisa; sina tatizo na kauli ya 'kujitenga'. Ni kauli ya kisiasa na imeshawahi kutolewa mara nyingi na watu wa Kigoma, watu wa Mtwara/Lindi, na hata watu wa Pemba.Binafsi hilo halinisumbui sana. Na mtu yeyote anajua aliitoa kauli hiyo kwa maana ya kuweka point ya utani ndio maana alisema "kama Sudan". Haina maana nzito ya kihivyo kwani na wengine wameshatoa kauli kama hizo.
Lakini huwezi kutoa kauli yenye kumtishia Rais na ukabakia hivihivi. Mtagundua kwamba kauli zenye kutishia maisha au usalama wa kiongozi yeyote wa umma huwa hatuzivumilii hapa kwa sababu moja kubwa - siyo watu wote wana akili zilizotulia na huwezi kujua nani akisikia anasukumwa vipi.
Nassari ni kiongozi maarufu sana sasa hivi na ameshinda kwa kishindo kikubwa sana. Kule Arusha ana mvuto mkubwa sana na ni mvuto wa watu kukesha na kumlinda hadi dakika ya mwisho. Chuki dhidi ya CCM ni chuki ya kweli (real hate) na siyo watu wote wanaweza kudumu kwenye chuki hiyo na wakiacha kwenye mambo ya kisiasa tu. Sasa, mbunge maarufu, tena kijana anaposimama na kusema anaweza kumpiga mkwara rais asikanyage Arusha siyo jambo dogo kwa sababu siyo wasikilizaji wake wote wanamuona 'mdogo hivyo'. Nassari ana ushawishi na anamvuto.
Labda watu wengi hawajui historia. Martin Luther King hakuwa na cheo chochote cha kisiasa zaidi ya kuwa mhamasishi mwanaharakati. Lakini mauaji yake yalisababisha miji ya Wamarekani kuingia katika machafuko makali sana. Ni kwa sababu watu walijua ameuawa na mikono ya watu wenye nguvu. Hata Nassari pamoja na "udogo" wake wote hakuna mtu Arusha atapenda anatendewa vibaya au kuonewa na wapo watu wanaoweza kufanya lolote kwa ajili ya utii wao. Nadhani watu wengi wameshasahu kuwa mauaji ya Arusha ya 2011 kwa kiasi kikubwa yalisababishwa na polisi kutumia nguvu dhidi ya watu ambao waliona wanaonewa.
Sasa mbunge anaposimama na kutoa kauli ambayo vyombo vya usalama vinaiona ni ya vitisho dhidi ya Rais ni kutokuwa makini kudhania tu ni jambo dogo. Alichotakiwa kusema Nassari ni hiyo kauli yake ya kwanza tu kuwa hakumaanisha ubaya wowote na kama mtu yeyote amekwazwa anaomba radhi. Lakini siyo kusema kuwa ati yeye ni mtu mdogo na asingeweza kugawa nchi; well hilil ni zaidi ya kugawa nchi. Hivi akisema kuwa Rais asikanyage na Kikwete akaamua kukanyaga na mwehu mmoja akaamua kufanya kitu kibaya kwa msafara wa rais watu watamlaumu mwehu kwa vile ni mwehu siyo? Lakini, yule mwehu ukimuuliza atasema "rais wetu" alitoa amri Kikwete asikanyage Arusha na akakanyaga!
Hii ni sababu moja ambayo inanifanya miye nisiwe shabiki sana ya hoja ya 'uongozi bora ni ujana' kwani tayari tumeshaona mengi yasiyo ya lazima ambayo vijana wameyafanya na kuthibitisha ukosefu mkubwa wa hekima na utulivu unaotokana na busara. Siyo lazima useme kila kinachoingia kichwani hata kama unaamini ni sahiihi. Kuna vingine unaweza kuvisema ila kwa namna tofauti. Hili huwezi kufundishwa shuleni au chuoni!
Ni matumaini yangu Polisi hawatoliendeleza hili na Nassari atakuwa amegundua (sidhani kwa sababu arrogance ya madaraka nayo nimbaya sana!) makosa yake. Sitaki ajisikie ameonewa bali ajue genuinely hakupaswa kutoa kauli hiyo na ni unfortunate. Kwa mfano Lema angekuwa makini na kauli zake wala asingevuliwa Ubunge! HEKIMA, HEKIMA, HEKIMA!!
ile kauli ya dogo janja isiporekebishwa mapema itaicost sana cdm,dogo janja ningemuona km mweledi sana angeomba radhi,n it was spoken unintentionally.
sikutegemea kama Nasari ambaye tulimwamini hivi ayafanye haya..ni aibu kwake na wanachadema wenye akili timamu
Wewe sio mdogo tena, Umeshapakwa mafuta kuwa mwakilishi wa wameru mashariki wote, Chochote utakachofanya kwa sasa ni msimamo wa jimbo lako chini ya mwavuli wa CHADEMA, kwa hiyo nakuomba umwombe MUNGU akuongezee hekima zaidi, kama mfalme Suleman, Kwa kuwa ameshakupa nguvu kama DAUDI, sasa hivi kwa mkono wa MUNGU unao uwezo wa kumuua GOLIATHI, Kwa hiyo jitahidi usimdhuru SAULI kwa kuwa ni Mpakwa mafuta wa Mungu hata kama anakusudia kumwacha.
tatizo la msingi kwenye hii habari ni kuwa nje ya "context" kwa makusudi. Nassari amesema maneno mengi lakini watu wana"donoa" maneno machache ili kuharibu maana halisi ya alichosema. Kwa mfano hapa unashupalia yeye kusema ni mdogo tu, lakini pia amesema ilikua kauli ya kuhamasisha mikoa mingine. Pia udogo aliosemea siyo umri, ni cheo chake cha ubunge katika chama chake cdm. Tukitaka kutendea maneno haki, tuyachambue kwa ujumla wake, (katika context) tuache "udonoaji"
Kwahiyo unataka kusemaje........Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
mambo madogo tu hayo nyie..........dogo anajifunza kidogo kidogo.......unaweza kuwa carried away na jazba wakati mwingine.Hapo kwenye RED mkuu panawakilisha ujumbe wa maana sana...ni ukweli usiopingika kuwa wana'chadema wasio na akili timamu tu ndo wanaoweza ku'support ujinga huu.