Joshua Nassari apitishwa kura za maoni ya mkutano mkuu wa CHADEMA - Arumeru

Hongera kamanda Nassary, Hongera makamanda waliomtia kajoto, sasa unganisheni nguvu yenu iwe moja, kwa maslahi ya chama chenu na wananchi wa Arumeru. Kazi iliyobaki ni moja tu, kuhakikisha Nassary anashinda beyond 90%

Mkuu huenda ushindi ukavuka asilimia 90%. Tunataka ushindi wake uandikwe kwenye vitabu vya historia
 
Hiyo visibility study na harambee ya Lema, kipi kilianza?
Hata mimi bado najiuliza yai na kuku kipi kilianza lakini mbona unakwepa swali langu bado tuko camp moja ya Sioi au mwenzetu wamekupandishia dau.
 
nassari amezaliwa tar 8/01/1985 .anaelimu ya chuo kikuu UDSM ya sera,mipango na utawala aligraduate 2009.
 
wapiga kura walikua wachache sana...

Ngoja nikusaidie gamba.

Kura za CCM Arumeru Mashariki

Jina Kura

1. Siyoi Sumari 361

2. William Sarakikya 259

3. Elirehema Kaaya 205

4. Elishiria Kaaya 176

5. Anthony Musani 22

6. Rishiankira 11

Jumla 1034


Ukichukua 1034 (CCM) - 888 (CHADEMA) = 146.
Usisahau kura za CCM zilipigwa kwa rushwa na rafu za kila aina ndo maana wanatuzuga kwa kurudia kupigiwa kura magamba wawili (2).
Pia usisahau wapigakura wa CCM walipelekwa na kulipwa ili kupiga kura wakati wa CHADEMA walienda wenyewe tena bila malipo yoyote kupiga kura.
Mpaka hapo tusubiri hadi hiyo April matokeo yatakapotangazwa ndo utajua vizuri watu hawa wa CHADEMA ni wachache au la.
 
Mkuu Chachana,

Ilitegemewa Nassari atashinda hasa ukitilia maanani uchaguzi uliopita alipigana kiume dhidi ya Marehemu Summari.Sijui kama fedha za harambee zilitumika dhidi ya wapinzani wake ndani ya chama ?.

Sikuwahi dhania kuwa Ngongo ni mgonjwa wa akili!
 
Joshua Nassari mbunge kijana atakayeingia bungeni kwa kupata ushindi wa kimbunga
 
Sawa haina neno huyu Joshua Nassari ni mzuri kwenu na ndiyo maana alijua atakuwa yeye na kuanza kukusanya pesa za kampeni mapema sasa subirini muone sisi wananchi wa Arumeru tutamchagua nani huwa sisi hatupendi mbwembwe na kelele tu ambazo hazina vitendo tunachagua mtu ambaye tunaona anao uwezo wa kutuletea maendeleo hatuchaguhi mtu kufuata udini,ukanda,ukabila, undugu,maandamano wala hatuvutiwi na helikopta tunataka sera zinazoeleweka na namna zitakavyotekelezwa hatutaki majungu wala mipasho vinginevyo tunamchinjia baharini!
 
Sawa haina neno huyu Joshua Nassari ni mzuri kwenu na ndiyo maana alijua atakuwa yeye na kuanza kukusanya pesa za kampeni mapema sasa subirini muone sisi wananchi wa Arumeru tutamchagua nani huwa sisi hatupendi mbwembwe na kelele tu ambazo hazina vitendo tunachagua mtu ambaye tunaona anao uwezo wa kutuletea maendeleo hatuchaguhi mtu kufuata udini,ukanda,ukabila, undugu,maandamano wala hatuvutiwi na helikopta tunataka sera zinazoeleweka na namna zitakavyotekelezwa hatutaki majungu wala mipasho vinginevyo tunamchinjia baharini!

????????????????????
 
tunashukuru hakuna alionesha dalili za kutumika na Magamba, hope wangemchinjia baharini..taratibu mpinga posho mwingine ndani ya mjengo

wenzie wamjulishe kabisa kuwa mshahara wa mbunge take home ni laki saba...isijekuwa ameacha kazi yake nzuri baadaye aje kujuta kama wale waliomfuata Makinda wakitaka kujiuzulu!
 
Jambo jema ni kuwa ktk mkutano wa watu zaid ya 800 anapata kura za idadi kama hyo.hii ni imani kubwa waliyonayo kwa bwana nassary,hivyo pia ni ishara ya aendako yaani uchaguzi wa jimbo.hivyo sasa ni wakati sahihi kwake kuendelea kujipanga zaid kisera,hoja na mikakati ya kuijenga arumeru lakini pia kupapambana vilivyo na mahasimu wake.hongera kamanda nassary na hongera wanacdm kwa uchaguzi usioibua majungu na malalamiko.viva cdm!
 
Back
Top Bottom