Wambague wasimbague, haijalishi atabaki kuwa ni Waziri Mkuu mstaafu na kati ya wazee wenye busara zao, waliobaki, wapigania haki na sheria kwa nchi hii. Mzee wa watu yuko mioyoni mwa Watanzania wengi, tunamuombea maisha marefu, aje aione Tanzania inayotakiwa kuwa.
Walishamfanyia visa vyote, kupigwa kibao na yule mwenye domo kama nyama ya nyongeza. Mtoto wake Kipi (ex shemeji) kufanyiwa mizengwe. Haijamkatisha tamaa kutetea Wananchi, angeweza akae ale mafao yake kwa raha zake, ila Mzee wa watu siyo mbinafsi, kajitoa kwaajili ya nchi hii. So hilo la kualikwa ni dogo sana anaheshima kubwa kwa wengi.