Jose mla vichwa anawezaje kula nyama za ajabu!?

Jose mla vichwa anawezaje kula nyama za ajabu!?

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
22,862
Reaction score
27,676
Huyu jamaa anawezaje kula makitu kama kenge,je midude ya aina hii huwa aina sumu?,au kuna namna ya upishi wake!.....
 
Tuna uwezo wa kufanya tunachotaka hapa duniani Mkuu
Ukiwa busy ku enjoy maisha haya mambo ya Jose hutayaona
1000171424.jpg
 
Venom= sumu inayokuua mnyama anapokung'ata
Poison=sumu inayokuua unapokula/kunywa kitu chenye hiyo sumu.

Hao nyoka, sijui mijusi na kenge wana venom ila sio poisonous, ndio maana wanaliwa tu (nduhu shida).
 
Mtu anakula nguruwe sembuse kenge , mbona watu wanakula sana hata hapo pwani ..Watu wanakula mamba nenda Handeni huko mpaka kenge
 
Mkuu ukiwa bado unaishi jaribu kutoka nje ya Tanzania na kwenda nchi zingine, mabara mengine
Kuna jamii za watu wanakula
Scorpion 🦂
Spider 🕷️
Exotic animals huko Asia na kawaida sana kwao
Tembelea YouTube ya mtu anaitwa “Best ever review show” utastaajibu aina ya mimea na wanyama wanaoliwa

Tanzania bado tuko limited sana kwenye aina za nyama
Ngombe
Mbuzi
Kondoo
Kuku
Nguruwe
Samaki

Hapo ilibidi tuongezs
Farasi
Mamba
Punda
Bata mzinga 🦃
Sungura 🐇
 
Huyu jamaa anawezaje kula makitu kama kenge,je midude ya aina hii huwa aina sumu?,au kuna namna ya upishi wake!.....
Tulikamatwa tunachunga ng'ombe karibu na hifadhi ya taifa miaka hiyo na Hawa jamaa wa gemu,
Jamaa Yangu alikuwa amekamata Hawa kanga wa porini, tulikuwa watu yule mkubwa wetu akasema tukimbie, mwenzetu mmoja akabaki, wale jamaa walipofika wakamuuliza Dogo unauza bei Gani huyo kanga, kasema 5,000
Akashuka mmoja kutoka kwenye gari, kamkamata yule mwenzetu, kapewa kipigo siyo Cha nchi hii, halafu akaambiwa amtafune yule kanga akiwa mzima mzima na manyoya, alimtafuna yule kanga kama robo hivi na kipigo juu,
Wale wale watu wa maliasili wengine wakawa wanasema muache huyo bado Dogo haelewi kitu, Ila mmoja akawa amekomaa kwamba Dogo lazima amle yule kanga mzima mzima.
Kutoka pale Dogo alikaa ndani siku 3 hajatoka nje, kama kwako kungekuwa na Hela basi angeenda kulazwa hospital.
Samahani nimetoka nje ya mada ila nimeona Uzi unazungumizia kuhusu kula vitu
 
Miaka fulani nlikuwaga rafiki
Mmoja mfaransa alikuwa tz kwenye NGO moja inajihusisha na mambo ya kilimo,huyo jamaa mke wake alikuwa mu ivory coast
Mke wake alikuwa anakula kenge sana tu,na alinambia kwao kenge msosi wa kawaida tu

Ova
 
Miaka fulani nlikuwaga rafiki
Mmoja mfaransa alikuwa tz kwenye NGO moja inajihusisha na mambo ya kilimo,huyo jamaa mke wake alikuwa mu ivory coast
Mke wake alikuwa anakula kenge sana tu,na alinambia kwao kenge msosi wa kawaida tu

Ova
 
Back
Top Bottom