Jose Chameleon bilionea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jose Chameleon bilionea

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Dec 8, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ndiyo, kwa asiyeamini, hebu angalau baadhi ya mambo yanayothibitisha utajiri wa nyota huyo.
  Anamiliki jumba la kifahari katika vilima vya Sekuku jijini Kampala, pia ana nyumba huko Arizona, Marekani, achilia ile ya Kigali, Rwanda aliyoinunua hivi karibuni kwa mamilioni ya shilingi.

  Ukiachilia mbali gari la kisasa aina ya Cadillac Escalade lililomgharimu zaidi ya Sh milioni 100, Chameleone ambaye ni baba wa watoto watu, pia anamiliki Mercedes Benz, BMW na aina nyingine za magari.
  Kwa ujumla, anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Sh bilioni 1.5 kwa fedha za Tanzania. Na anasema bado anazisaka, kwani bila ya kuwa na tamaa ya kusaka mafanikio zaidi, ndoto huenda zisitimie.

  Anayasema hayo akisisitiza kuwa, baada ya nyumba, magari na akaunti nono benki, sasa ana ndoto za kumiliki helikopta yake, baada ya kuwa amekuwa akikodi mara kadhaa ama kwenda katika matamasha au kama alivyofanya wakati anamuoa mkewe Daniela Atim.
   
 2. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 180
  wanamuziki pamoja na wanafilamu wa BONGO wanaibiwa sana na jamii ya akina Ruge, wasipozinduka wataendelea kuwashangaa wenzao ktk mataifa mengine. wanasaa shitukeni jamani
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Du huyu jamaa ni tajiri pia ana jumba lipo karibia na ufukwe wa ziwa victoria kwa upande wa uganda,pia ana apartments kibao huko uganda,hilo cardillac ni zaidi ya million 250 za kitanzania,Ukija kina Bobby winne na Bebe Cool wanamiliki hadi meli na Hummer hizi wanazotembelea kina 50 cent(kwenye video ya Wanksta,acha hizi za kina musofe za kichina/south),Kwa upande wa kwetu washika dau wananeemeka sana ila wanamziki wana hali duni(nanukuu kwa inspector haroun),yani diamond na kuuza kote huko album kupiga show za kufa mtu lakini anatembelea opa haaa,Prof jay Raum haaaaaa
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Hapana wanamuziki wa hapa bongo wengi akili mukichwa hakuna utawakuta muda wote wako kwenye vigorosali wakilamba kinywaji,pia wanalewa sifa akipata vijisenti tu kidogo inakuwa taabu,nafikiri wangekuwa makini kama Lady JD wangekuwa mbali ,ukiwaangalia vijana wetu wako juu kimuziki kuliko wakenya na waganda ,tatizo wengi hawashauriki na wana elimu duni,na hawataki kujifunza,kwa TZ ni lady JD,huenda akiendelea AY namuona yuko makini
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe kilaza unafahamu maana ya Billionea? maana kwa akili zako ndogo sasa mtu anaemiliki show room ya magari sijui utamuitaje!!
   
 6. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 996
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Angefungua biashara ndo ningemuona wa maana..co kuwa na magari tuu???
   
 7. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Umeshaambiwa ana apartments, au hukuelewa
   
 8. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ahahaha kiiengereza kigumu si unajua kilikuja na meli, hakuelewa
   
 9. King2

  King2 JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Atakuwa anauza unga! Hawezi kuwa na pesa yote kwa muziki tu.
   
 10. W

  Warrior Ruff Member

  #10
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  What Vinegaz fighting for
   
 11. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Uko serious??, ni majumba ya kifahari au vibanda?? Mbona thamani ya mali zote ni ndogo?, Mi nilitegemea Jumba la kifahari moja tu litazidi hiyo fedha uliyotaja kama utajiri wake wote!!
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Dec 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  iwe shule kwa wasanii wa bongo wanaodhani pesa ipo redioni!!!

  they need to learn musicians walio nje ya virus ndio wanaotengeneza pesa
   
 13. THK DJAYZZ

  THK DJAYZZ JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  teh teh teh
   
 14. Lonestriker

  Lonestriker JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 641
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  uliza watu waliotembelea Uganda na kupata nafasi ya kuona show za Kiganda.Matamasha makubwa ya uwanjani ni kawaida.Uwanja wa Nakivubo umegeuka kuwa uwanja wa matamasha ya muziki.
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Huyu uwezo wake wa kufikiri umefikia tamati. ubongo wake umeaminishwa kwamba kila mwenye mafanikio ni drug dealer.
  Msome maneno yake mwenyewe Chameleone ni haya:

  Anakumbuka akiwa na Bebe Cool na Redsun alipata fursa ya kutumbuiza katika shindano la kumsaka Mrembo wa Kenya.

  Anakiri hapo ndipo milango ya neema ilipoanza kufunguka. Anasema Dorotea, baada ya kuzoeana alimshawishi ahamie nyumbani kwake badala ya kuendelea kulala studio, ushawishi ambao ulimchukua zaidi ya wiki moja kumkubalia.

  "Nilipohamia tulikuwa marafiki, lakini mengine yaliibuka tukiwa katika nyumba moja. Mara nyingi kila akitoka, alinikuta nimetulia naandika nyimbo, huku akihoji ni lini nitarekodi. Nilikosa jibu kwa kuwa siku wa na fedha.

  "Siku moja akiwa safarini huko Afrika Magharibi aliniachia bahasha yenye dola za Kimarekani 1,000 (karibu Sh milioni 1.8 za Tanzania kwa sasa), akaniambia niingie studio.

  "Huo ukawa mwanzo wa kibao Mama Mia na sikuamini kama fedha ile ingebadilisha maisha yangu na kunifikisha hapa nilipo. Mengine yanabaki kuwa historia," anasema.

  Pamoja na utajiri aliovuna kupitia muziki, nyota huyo anasema historia ya kushuhudiwa `Live' na watu zaidi ya bilioni 9 akitumbuiza wakati wa Kombe la Dunia kwake ni kitu cha kipekee.

  "Mtoto wa Afrika tena Afrika Mashariki kupewa heshima ile haikuwa kitu kidogo. Najiona mwenye bahati na ni mastaa wachache wanaweza kuingia katika kundi la bahati hata wangeishi kwa miaka 1000."

  Anasema kutokana na baraka alizopata maishani, ameamua kuanzisha taasisi ya Chameleone ili aweze kuwasaidia wasiojiweza.

  "Nikiwa mdogo sikuwa na maisha mazuri, sikutoka katika familia bora, kwa hiyo ninajiona mwenye wajibu wa kuwasaidia wengine wakianzia katika misingi mizuri ya kielimu. "Nimeshanunua eneo kwa ajili ya kujenga kituo.

  Nataka jamii siku moja inikumbuke kwamba niliwika na kuitangaza nchi yangu, lakini pia sikuwa mchoyo, bali niliyatumia vyema matunda ya muziki.

  Kwa kufanya hivi, naamini ipo siku nitawashawishi wengi kufanya mambo makubwa kwa ajili ya jamii wanayotoka."

  Huyo ndiye Joseph Mayanja ambaye pamoja na misukosuko ya maisha tangu akiwa shule hadi sasa akiwa staa, bado nyota yake inang'ara.

  Je, atazidi kupata mafanikio? Bila shaka ni jambo la kusubiri na kuona, hasa ikizingatiwa kuwa, mwenyewe amejijengea falsafa ya kutolewa sifa, bali kazi kwa kwenda mbele.

  Pamoja na yote, Chameleone anapaswa mfano wa kuigwa kwa wasanii wengi wa Kitanzania ambao huvuma kwa muda mfupi, lakini wakishazikamata fedha hupotelea kwenye ulimwengu wa anasa na baadaye kujikuta wakiwa `choka mbaya', tena wakiwa hawana akiba benki wala hawajawekeza.
   
 16. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,557
  Trophy Points: 280
  uganda hakuna monopoly ya industry ya muziki.leo hapa Bongo hata Diamond aliye juu sasa akigombana na Ruge tu kwisha!! Ruge ndio refa wa industry! Ndio maana tunapigana muziki uwe huru kutegemea vipaji tu!
   
 17. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,557
  Trophy Points: 280
  Ruge akikupania anapiga fitna redio zote na maafisa masoko wote,wasambazaji wote! Msanii kwisha! Msanii mafanikio yake yapo mikononi mwa wengine! Jiulize inakuwa Afande sele ameanza kutamba tena?
   
 18. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,158
  Likes Received: 5,589
  Trophy Points: 280
  We una nini usishabikiewe wenzio mpwa wengine ukiambiwa chanzo cha utajiri utajifungia kanisani mwezi mzima ooooooo
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,158
  Likes Received: 5,589
  Trophy Points: 280
  mpwa nakwambia kuna wengine hata mada awabebi
  huko dubai mpwa kuna wazee waanava kanzu na ushungi katikati hao mpwa wakiamua wanakupa ndege ya emirate moja ama billions unakuwa na kazi ya kuwafanyia kazi usiniulize ipi
  irene uwoya atatusaidia kwa hili
   
 20. Kitomai

  Kitomai JF-Expert Member

  #20
  Dec 8, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,032
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Miimi nadhani tatizo la wasanii wetu wa hapa bongo hawana malengo makubwa mfano kuwa na malengo ya kuwa mwanamziki mwenye hadhi ya kimataifa. Haitoshi tu pia kuwa na lengo hilo bali mikakati ya namna utakavyolifanikisha lengo hilo. hili suala la kumtupia mtu fulani lawama kwa sababu umekwama naona halina tija kwa kiasi kikubwa.
   
Loading...