Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,186
- 10,922
Baada ya muda mrefu wa ukimya jana Jumanne serikali ya Jordan imeongeza idadi ya askari na vifaa vya kivita mpakani na Israel tayari kwa mapigano iwapo Israel itaendelea kuhatarisha usalama wao na kuvunja mkataba baina yao.
Hayo yamebainishwa na waziri mkuu wa Jordan,Bisher Khasawneh akielezea mwenendo usio kuwa mzuri wa Israel kwa wapalestina wanaoishi ukingo wa mashariki kuvuka mto Jordan
Katika maelezo hayo ya utayari wa kivita waziri mkuu huyo amesema kumekuwa na shinikizo kwa baadhi ya wabunge wa Israel wakisema suluhisho la wapalestina walio maeneo hayo ni kuingia Jordan.
Kivitendo walowezi wa kiyahudi wamekuwa wakiongeza mashambulizi kwa wapalestina kwa kuwatoa kwenye majumba yoo na mashamba kwa nguvu ili waondoke na kuingia Jordan.
Waziri mkuu huyo amesema vitendo hivyo ni aina ya ukiukwaji wa mkataba baina yao wa mwaka 1994.
Akaongeza kwa kusema aina yoyote ya kuwahamisha kwa nguvu na matendo yanayopelekea hilo ni ukiukwaji wa mkataba huo.
Hali hiyo itapelekea na wao kuuona mkataba huo kama ni kipande cha karatasi kilichojaa mavumbi basi.
Vitendo hivyo vya Israel mbali ya kukiukwa kwa mkataba amesema vile vile vinahatarisha usalama wa Jordan jambo ambalo hawataweza kulivumilia.
Watu upande wa Jordan wametoa ushahidi wa kuoona idadi kubwa ya magari ya kivita na vifaru vikielekea kwenye bonde la Jordan mpakani na Israel.