Jongoo ana nini mpaka wanawake mumuogope?

Jongoo ana nini mpaka wanawake mumuogope?

Hahahahaa aseeee mbona kama ni mm umenisemea...mm anaconda nta dili nae lakini sio millipede walah naweza nikaweweseka cku nzima na ucku nkaota......

Cjui kwann.....aagh.
 
Mimi na wanaume wangu wa nguvu(la kijeshi)

Nikiona chambo/wale wadudu wanaotumikaga kuweka kwenye ndoano na kuvulia samaki .

Hao wadudu nawaogopa sana

Kuna siku nilikuwa naoga bafuni nikaona chambo mrefu kweli bafuni

Aiseeee!!wana Jf nilichomoka uchi mabafuni mbio mpaka ndani nikiwa na sabuni usoni.

Yaani sijui huwaga nawafikiriaje tu jinsi walivyo tena akiwa anatembea vile wanavyojinyonga nyonga.

Yaani nikiwaona tu mwili wangu unasisimuka vile na ngozi kuwa kama nina baridi .
 
Jongoo ni mdudu mdogo sana ambaye anaogopwa na jopo kubwa kabisa la wanawake,
Hii inafika mbali zaidi mpaka unakuta wanawake wanatoka nduki huku wakisasambua nguo zao, wengine hujikuta wanaruka Kung-Fu Panda bila kutegemea huku wakituachia TV ya bureee eti kisa wamekaona kajijongoo kanapita karibu yao!

Kitu kilichonifanya mpaka nishangae unakuta wengi ukiwauliza wanadai eti huwa wanamuogopa jongoo sana tena kuliko nyoka,
Umeona balaa hilo? Yani eti nyoka mwenye sumu kwao ni bwege tu, lakini akiona jongoo atapiga yowe utadhani U.S.A ameona mabomu ya Korea Kaskazini.!

Sasa wanawake inabidi mje mtuambie kipi kinachofanya mpaka mumuogope kiasi hiko?
 
hapana simaanishi hivyo, jongoo analeta hisia kama unapandiwa na chavichavi au wale wadudu wa kwenye Mwembe.
niliwahi tishiwa jongoo nikazimia kwa woga ,maana alonitishia alimbeba akawa anataka kunigusisha, yani unakua hutaki akuguse huyo mdudu kwahivo ukimwona tu unakua na hisia kama vile kakupandia mwilini hicho ndio kinafanya tuogope sana.
Hisia tu maana hata vingine vyenye mwendo wa jongoo vinawaingilia mwilini na mnafurahia.
 
Hivi jongoo hutumika kufanyia nin? Na wanafaida gan?kunasiku niliona MTU akisafirisha hayo makitu kwenye boksi bahati mbaya hakufika mbali alikamatwa na polisi huku akilala mika kuna MTU amemchomea akasikika mtua akisema hao jongoo wana faida sikuelewa wanafaida gan
Ila jongoo wanatisha jamani has a ukutane na Yale makubwa yanarangi nyeusi lazima mwili usisimke na sarakas zisizo na matarajio

Hao unaosema wewe anaitwa Jongoo Bahari, huwa wanapatikana baharini hasa maeneo ya mtwara na Zanzibar, Kiingereza anaitwa orthurians, kwa Tanzania bara ni Marufuku kuwavua hawa wanavuliwa kwa magendo na huwa wanasafirishwa kwenda China na Japan, wako tofauti na hawa wanaoogopwa na Wanawake
 
Mimi na wanaume wangu wa nguvu(la kijeshi)

Nikiona chambo/wale wadudu wanaotumikaga kuweka kwenye ndoano na kuvulia samaki .

Hao wadudu nawaogopa sana

Kuna siku nilikuwa naoga bafuni nikaona chambo mrefu kweli bafuni

Aiseeee!!wana Jf nilichomoka uchi mabafuni mbio mpaka ndani nikiwa na sabuni usoni.

Yaani sijui huwaga nawafikiriaje tu jinsi walivyo tena akiwa anatembea vile wanavyojinyonga nyonga.

Yaani nikiwaona tu mwili wangu unasisimuka vile na ngozi kuwa kama nina baridi .
Kumbe wanaume tupo tofauti
 
Nadhani hili suala linachangiwa na mabadiliko ya mazingira. Kwa mfano nilikokulia mimi kumshika kinyonga, konokono, jongoo, panzi maduduwasha ni mambo ya kawaida kabsa wakati mwingine kuna watu humshika hadi nyoka. Ila najaribu kupata picha kwa MTU aliekulia DSM ambae anajua kupanda daladala na Schule, biashara n.k.
Shambani hapajui,
Kufuga hajui ni sawa kuwa na uoga wa namna hio
well said mkuu
 
Jongoo ana sumu inayoitwa cyanide ni hatari kama ukiila(ingest)... Anatumia kemikali hio kujilinda na wanaomla (predators kama ndege na baadhi ya wanyama)
Jongoo wengi wana rangi za onyo (aposematic colouration) mara nyingi ni nyeusi na rangi zingine mng'ao kama nyekundu na njano(hapo kwenye picha tunaona ni nyeusi na miguu mekundu) .... Rangi hizo huonya adui wa jongoo kama ndege na wengineo (ni kama kusema nione na kaa mbali na mimi, mi sifai kuliwa nina sumu kali)... Jongoo wengi wakiguswa hujifanya umbo la mviringo (kujilinda) au kujitupa(kwa kuzunguka kwa kasi kama nyoka) hapo uiga nyoka (mimicry) yote ni kujilinda na anayeweza kua adui... Kuna mnyama mmoja anapenda sana kula jongoo... Tunamuita fungo (civet),huyu mwili wake unaweza kuchakata sumu ya jongoo isimdhuru.
NB:kama sio mtaalam wadudu epuka kugusa wadudu wenye rangi za mng'ao...hasa mchanganyiko wa nyeusi, nyeupe, nyekundu au njano Wengi wao wanasumu(chemicals za majimaji) inayoweza kutoa malengelenge au kuunguza ngozi. Japo kuna wadudu wanatumia hizo rangi kudanganya wana sumu (mimicry)
bata nae anawala sana hawa wadudu
 
huwa wanatisha hivi hasa wawe wale wanene. kuna siku nilipita chini ya muembe akanidondokea mmoja begani uuuwi siwez kusahau, mpaka kesho sipiti wala kusimama chini ya muembe
Hukuvua nguo wewe kweli?
 
Mimi na wanaume wangu wa nguvu(la kijeshi)

Nikiona chambo/wale wadudu wanaotumikaga kuweka kwenye ndoano na kuvulia samaki .

Hao wadudu nawaogopa sana

Kuna siku nilikuwa naoga bafuni nikaona chambo mrefu kweli bafuni

Aiseeee!!wana Jf nilichomoka uchi mabafuni mbio mpaka ndani nikiwa na sabuni usoni.

Yaani sijui huwaga nawafikiriaje tu jinsi walivyo tena akiwa anatembea vile wanavyojinyonga nyonga.

Yaani nikiwaona tu mwili wangu unasisimuka vile na ngozi kuwa kama nina baridi .
Hao tulikuwa tunaenda kwenye kinyesi cha ng'ombe kuwachukua for fishing. Unafukua samadi, unatoa mmoja mmoja kwa mikono, unatupia kwenye kikopo cha mafuta Rays, moja kwa moja mtoni kupiga kazi.
 
Back
Top Bottom