Jongoo ana nini mpaka wanawake mumuogope?

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Jongoo ni mdudu mdogo sana ambaye anaogopwa na jopo kubwa kabisa la wanawake,
Hii inafika mbali zaidi mpaka unakuta wanawake wanatoka nduki huku wakisasambua nguo zao, wengine hujikuta wanaruka Kung-Fu Panda bila kutegemea huku wakituachia TV ya bureee eti kisa wamekaona kajijongoo kanapita karibu yao!

Kitu kilichonifanya mpaka nishangae unakuta wengi ukiwauliza wanadai eti huwa wanamuogopa jongoo sana tena kuliko nyoka,
Umeona balaa hilo? Yani eti nyoka mwenye sumu kwao ni bwege tu, lakini akiona jongoo atapiga yowe utadhani U.S.A ameona mabomu ya Korea Kaskazini.!

Sasa wanawake inabidi mje mtuambie kipi kinachofanya mpaka mumuogope kiasi hiko?
 
Yaani umenikumbusha mbali....kuna mama mmoja anaogopa jongoo siwezi hata kuelezea........
Yeye hata ukitamka tu jongoo anapiga kelele mpaka majirani wanajaa
 
Simpendiiiiii..mtu akinitishia ilo dudu sisemezan nae maana huwa naweweseka had usiku. Yaan likijikunjaa mara litembee mwili wangu unasisimka woga. Naandika huku nimekunja midomo umemtajia ninnn
 
Sijawahi kumuogopa jongoo kwakweli.
Ila kitu nyoka na ile mijusi wakati fulani unaezaikuta ndani (kwa baadhi ya nyumba zetu flan)
Doohntaenda lala kwa jirani
 
Back
Top Bottom