Jongoo ana nini mpaka wanawake mumuogope?

Hivi jongoo hutumika kufanyia nin? Na wanafaida gan?kunasiku niliona MTU akisafirisha hayo makitu kwenye boksi bahati mbaya hakufika mbali alikamatwa na polisi huku akilala mika kuna MTU amemchomea akasikika mtua akisema hao jongoo wana faida sikuelewa wanafaida gan
Ila jongoo wanatisha jamani has a ukutane na Yale makubwa yanarangi nyeusi lazima mwili usisimke na sarakas zisizo na matarajio
 
Nadhani hili suala linachangiwa na mabadiliko ya mazingira. Kwa mfano nilikokulia mimi kumshika kinyonga, konokono, jongoo, panzi maduduwasha ni mambo ya kawaida kabsa wakati mwingine kuna watu humshika hadi nyoka. Ila najaribu kupata picha kwa MTU aliekulia DSM ambae anajua kupanda daladala na Schule, biashara n.k.
Shambani hapajui,
Kufuga hajui ni sawa kuwa na uoga wa namna hio
 
huwa wanatisha hivi hasa wawe wale wanene. kuna siku nilipita chini ya muembe akanidondokea mmoja begani uuuwi siwez kusahau, mpaka kesho sipiti wala kusimama chini ya muembe
Hahahah inaelekea hata ukitaka kula embe ukimkumbuka jongoo basi unaliacha
 
Jongoo ana chemical anayo itoa inaitwa hydrogen cynide.... Utafit wang utaanzia kam hii chemical ipo kweny manii. Hapa c kuna watu wanasem jongoo =dushe. Ndiomana nimejarib ingia ndan kidogo
Hiyo kemikali anaitoa anapohisi hatari au anaitoa muda wowote tu?
 
Ama kweli wewe ni Jungle master, Ahsante sana mkuu kwa elimu ya bure kabisa,
na usisite kuja kutuelezea mengi zaidi ili tuwafahamu vizuri.
Sasa swali la kujiuliza inamaana hawa wanawake wamepewa sense kubwa kabisa ya kuhisi hatari ndomana huwa wanawaogopa pasipo kutambua wanawaogopa kwasababu gani? Cc miss chagga Valentina mahondaw ukhuty Shunie
 
Kuna duduwasha flani hivi tulipokuwa watoto tulikuwa tunaambiwa eti linaingia kunyonya ubongo kupitia puani, yaani mpaka na uzee huu sitaki kabisa kuliona lile ingawa najua siyo kweli.
mwenye tabia hiyo tuliambiwaga ni Kenge, sijui kweli
 
kabisa Mungu katupendelea
 
na kunakipindi kipo chanel ya wanyama dstv wanasema nyani hutumia jongooo kama dawa ya kujizuia na wadudu wanao wadhuru.. na niliona nyani anamkamata jongoo anana muuma na meno halafu anajirushia damu ya jongooo yule muelezeaji akasema ile ni kinga dhidi ya wadudu
 
Juzi nilihama nyumba kisa nilikuta gamba la nyoka ndani....nyoka ni hatari jmn kuliko hata jongoo [emoji21]
Bora nyoka umuone na umuue, kuliko kumuona alafu apotelee chumbani heheheh
 
kabisa Mungu katupendelea
Jongoo ana umbo lenye vipingili (segments) kila segment ina pea mbili za miguu (Jongoo anaweza kuwa na miguu mia mpaka 700 lakini haiwezi fika 1000 kama jina la Kiingereza linavosuggest "millipedes" (kutoka latin milli=1000 pedes=legs) wanapendelea unyevunyevu, mara nyingi huonekana nyakati za mvua au maeneo yanaotunza unyevunyevu kwa muda mrefu... Wanakufa haraka kama ardhi inakua kavu... Kuna baadhi ya Jongoo hukwepa hali ya ukavu kwa kujifukia kwenye udongo wenye unyevunyevu au chini ya magamba ya miti na mawe... Jongoo wanakula majani, mbao au mimea ilioza kwenye ardhi.... Ni muhimu sana kwa kuchakata maozo ya mimea lakini pia wanaweza kuwa waaribifu kwa kula mizizi ya karanga na hata pamba kama wakizidi... Jongoo hutaga mayai kwa kuyafukia kwenye ardhi (yenye unyevunyevu)
 
asante mkuu kwa somo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…