Jongoo ana nini mpaka wanawake mumuogope?

Jongoo ana nini mpaka wanawake mumuogope?

Jongoo ni mdudu mdogo sana ambaye anaogopwa na jopo kubwa kabisa la wanawake,

Hii inafika mbali zaidi mpaka unakuta wanawake wanatoka nduki huku wakisasambua nguo zao, wengine hujikuta wanaruka Kung-Fu Panda bila kutegemea huku wakituachia TV ya bureee eti kisa wamekaona kajijongoo kanapita karibu yao!

-

Kitu kilichonifanya mpaka nishangae unakuta wengi ukiwauliza wanadai eti huwa wanamuogopa jongoo sana tena kuliko nyoka,
Umeona balaa hilo? Yani eti nyoka mwenye sumu kwao ni bwege tu, lakini akiona jongoo atapiga yowe utadhani U.S.A ameona mabomu ya Korea Kaskazini.!

Sasa wanawake inabidi mje mtuambie kipi kinachofanya mpaka mumuogope kiasi hiko?
Tatizo la jongoo hapandi mtungi ndio maana wanamuogopa laiti angekuwa anapanda mtungi ungeona km ..,
 
Yaani sijui kwanini akikugusa unaweza hata zimia, nina rafiki yangu ukimuekea jongoo mbele yake chochote utachomuambia anakubali...sijui kwann tunaogopa kiasi hiki
Naomba kumujua huyo rafiki yako ili niweze kumuomba chochote kile kitu nitakachokihitaji nikimuwekea jongoo...tehtehteh!!
 
mm jongoo sio sana

wale mende wakubwa yeuuuwii naeza nikapoteza ata fahamu
 
Miguu mingi, hana macho, ukimgusa tu anajikunja simpendi ila simuogopi.
 
Screen Shot 2017-04-21 at 1.29.08 PM.png

Nadhani wanaoogopa majongoo siyo wanawake peke yako... hata baadhi ya wanaume pia wanagopa majongoo...
  • Majongoo hupendelea sana kujitokeza nyakati za mvua.
  • Hawana sumu ya kusema, itamdhulu binadamu lakini wana tezi ambazo zinauwezo wa kutengeneza maji maji, ambayo husababisha allergy kwa watu wengi. Hayo maji maji yanauwezo wa kunguza ngozi yako au kusababisha muwasho mkali sana na kuharibu ngozi. Wengine wanasema usimguse jongoo atakujambia.
  • Ukiachilia mbali maji maji wanayotoa pia wanangata, na maumivu yake ni makali kwa sababu yanaambatanishwa na sumu, lakini siyo sumu ya kukuua.
  • Kuna baadhi ya majongoo, kwenye kujihami hurusha au humwaga maji maji yenye harufu kali, mbali na yote itakuachia vitu kama malengelenge kwenye ngozi yako.
  • Wengi pia labda watakuwa wanaogopa ile miguu yake... majongoo wana miguu 40-400 mpaka 750

cc: mahondaw
 
vile anavyojinyonga nyonga aisee ila mm ni muoga ata kwa mende
 
Hehehe jaman mtuache tuu hao wadudu sjui wana nini yani uuuwiiiii wanatishaaa
 
Jongoo ni mdudu mdogo sana ambaye anaogopwa na jopo kubwa kabisa la wanawake,

Hii inafika mbali zaidi mpaka unakuta wanawake wanatoka nduki huku wakisasambua nguo zao, wengine hujikuta wanaruka Kung-Fu Panda bila kutegemea huku wakituachia TV ya bureee eti kisa wamekaona kajijongoo kanapita karibu yao!

-

Kitu kilichonifanya mpaka nishangae unakuta wengi ukiwauliza wanadai eti huwa wanamuogopa jongoo sana tena kuliko nyoka,
Umeona balaa hilo? Yani eti nyoka mwenye sumu kwao ni bwege tu, lakini akiona jongoo atapiga yowe utadhani U.S.A ameona mabomu ya Korea Kaskazini.!

Sasa wanawake inabidi mje mtuambie kipi kinachofanya mpaka mumuogope kiasi hiko?
Umesahau mende na vinyonga,
Yaani kuna ambao wanaowagopa mende kuliko hata jehanam!
 
Back
Top Bottom