Jonas Savimbi of UNITA

1475158734817.jpg


Ndivyo ilivyokuwa kwa Jonas Savimbi ambaye kitendo chake cha kugomea kurudiwa kwa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo na kuamua kuingia msituni kulipelekea kuuawa kwake. Savimbi alifanya kosa moja kubwa alilazimisha vikosi vyake kuingia msituni kupambana na serikali akiwa bado hajajipanga vyema, ni bora angekubali kurudia uchaguzi dhidi ya Rais Dos Santos huku akijipanga.Bahati mbaya hakulikumbuka hilo, aliwaza jambo moja tu kuingia msituni kuandaa kikosi chake tayari kuuondoa utawala wa Dos Santos.

Aliingia msituni kipindi ambacho tayari kikosi chake kilikuwa kimeingiliwa na vibaraka ‘spy’ kutoka ndani ya kabila lake, vibaraka hawa waliandaliwa kwa ustadi mkubwa na ndiyo walihusika kutoa siri zote za nini kilikuwa kinaendelea kwenye kikosi cha Savimbi.

TAARIFA YA KUUAWA KWAKE
Februari 22, 2002 vyombo vingi vya habari duniani kote vilitawaliwa na habari kubwa ya kuuawa kwa komando wa vita, mbabe wa wababe, mfalme wa pori na mwanaume aliyeisumbua serikali ya Angola kwa zaidi ya miaka 27 akiongoza vita vya msituni dhidi ya vikosi vya serikali.

HISTORIA YAKE
Jonas Malheiro Savimbi, alikuwa mtoto wa pekee kwa baba yake Lote, aliyekuwa mfanyakazi wa reli ya Benguela na mhubiri wa kanisa la Protestanti lililokuwa likifadhiliwa na Wamarekani. Pamoja na baba yake kuwa muumini wa dini kamwe Jonas hakuwa muumini, tangu utoto wake alikuwa mtukutu.

Wazazi wake wote wawili walikuwa wanatoka kabila la Bieno ambalo baadaye ndiyo likawa msingi wa nguvu kubwa ya Jonas Savimbi kijeshi, kwani aliunda jeshi imara kwa kuwachukua ndugu zake na watu wa kabila lake hali iliyopelekea kuwa na jeshi imara na lenye umoja na mshikamano.

Waliwasiliana kwa kutumia lugha yao na ilikuwa ngumu kwa mtu asiye kabila la Bieno kuingia. Alifanya hivyo lengo likiwa kuwakwepa vibaraka ‘spy’ wa serikali. Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi alibahatika kwenda kusoma elimu ya sekondari nchini Ureno na akiwa huko alikutana na mwanaharakati Augustino Neto ambaye baadaye alikuja kuwa rais wa kwanza wa Angola.

HARAKATI ZAKE
Mwaka 1966 baada ya kurejea kutoka nchini China ambako alienda kupata mafunzo ya kijeshi alirudi na kuunda UNITA na kuanza kupambana na serikali ya kikoloni sambamba na vyama vingine ambavyo vyote vilikuwa vikipigana kumtoa mreno.

Hapa ndipo jina la Jonas Savimbi likaanza kusikika kote duniani kutokana na mbinu kubwa za kijeshi alizonazo huku akisapotiwa na wananchi kutoka kabila lake la Bieno. Akitoa maelekezo ya kijeshi kwa wasaidizi wake (hawako pichani)
Huku akipata sapoti kubwa kutoka China na baadaye Marekani, aliongoza vita vikali kwa muda wa miaka zaidi ya 20 huku akiwa ni tishio kubwa kwa Serikali ya Luanda. Kuna muda aliwahi karibia kuipindua serikali ya Rais Dos Santos.

Akiwa na uwezo wa kuzungumza lugha saba kiufasaha zikiwemo tatu za ndani ya bara la Afrika na nne nje ya bara aliweza kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali kuwaomba msaada wa zana za kivita na alifanikiwa kuwa na jeshi imara. Aliwahi kunusurika kuuawa mara kadhaa likiwemo jaribio la Februari 1990 ambapo aliponea chupuchupu na kukimbilia nchini Marekani na kufanikiwa kuonana na Rais Bush ambaye alimuahidi kumuongezea zana zaidi za kijeshi na baada ya kupona alirejea nchini Angola kuendeleza mapambano.

Baada ya kunusurika kuuawa zaidi ya mara 20 na vikosi vya serikali ya Angola huku taarifa za kuuawa kwake zikiripotiwa zaidi ya mara 15 hatimaye 22 Februari 2002 Jonas Savimbi aliuawa. Maauaji yake yalitokea kwenye mapigano baina ya vikosi vyake dhidi ya serikali kwenye mto uliopo jimbo la Moxico eneo ambalo alizaliwa. Mapigano hayo ya kushtukiza yalipangwa baada ya vibaraka kutoa siri za mahali alipo Savimbi na baadhi ya wasaidizi wake muhimu, haikuwa kazi rahisi kumuua.

Kwenye shambulio hilo kali kuwahi kufanywa na vikosi vya serikali dhidi ya kikosi cha Savimbi walifanikiwa kumpiga risasi 15 mwilini mwake, alipigwa kichwani, kifuani na sehemu za miguuni na aliweza kumudu na kuendeleza mapambano kwa zaidi ya saa nne kabla ya kuishiwa damu na kuanguka chini na kufariki. Tukio la kuuawa kwake bado limeacha maswali mengi mpaka leo inakuwaje na aliwezaje kuhimili kuendeleza mapambano hata baada ya kupigwa risasi 15 mwilini mwake?

Alizikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao ya Luena na kuhudhuriwa na wapiganaji mbalimbali wa UNITA. Mauaji yake yalimaanisha mwisho wa mapigano ya msituni nchini Angola, Chuma kilikuwa kimeangushwa, wasaidizi wake hawakuwa na mbinu na uwezo kama Savimbi. Baada ya kifo chake serikali kuu ilitangaza ya kwamba hatimaye wameangusha mbuyu wa chuma uliowasumbua miaka mingi.

Wapo wanaoamini mpaka kesho kwamba Jonas Savimbi hakuwa binadamu wa kawaida, walimuona ni binadamu wa pekee mwenye uwezo mkubwa kuliko binadamu wa kawaida. Wenye imani potofu walimfananisha na jini au mzimu unaotembea popote na wakati wowote bila kujali hatari iliyo mbele yake. Hadi mauti yake yanamkuta ameacha watoto na wake wengi ambao idadi yake haijawekwa wazi kulingana na sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa akiishi msituni.

Na Kwa usaidizi wa Leonard Msigwa/GPL
 

Attachments

  • 1475159044533.jpg
    1475159044533.jpg
    66.9 KB · Views: 35
Tujikumbushe leo ktk historia .

Risasi 15 zilizoingia katika maeneo tofauti ya mwili wa Jonas Malheiro Savimbi ziliukatiza uhai wake, baada ya miaka 27 ya mapambano ya msituni dhidi ya Serikali ya Angola.
Katika mapambano hayo ya mwisho, Savimbi ambaye alipambana hadi pumzi yake ya mwisho, pale roho ilipouacha mwili, aliingia katika historia ya taifa hilo na ya dunia, kutokana na namna alivyoshiriki katika vita baridi, akichukuliwa kama ngome muhimu kwa nchi za dunia ya tatu, hasa za Afrika.
Risasi hizo zilimaliza mapambano ya Savimbi aliyezaliwa Agosti 3, 1934 huko Munhango akiwa mtoto wa Lotte, mfanyakazi, Mkuu wa Stesheni wa Shirika la Reli la Angola na mhubiri katika Kanisa la Kiprotestanti la Angola lililoanzishwa na wamisionari wa Marekani.
Jonas Savimbi alikuwa ni kiongozi wa vita vya msituni Angola. Savimbi alifariki Februari 22, 2002.
Alisoma katika shule za Kiprotestanti na Kikatoliki, lakini akiwa na miaka 24 alipata udhamini wa kwenda kusoma Ureno ambapo alimalizia masomo yake ya sekondari na somo la lazima la siasa huku akishindwa kuanza kwa wakati masomo ya udaktari wa binadamu aliyotakiwa kuyachukua.
Mwaka 1966 alianzisha vuguvugu la Unita kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno.
Katika nyakati zake za awali, kabla ya kuanzisha Unita, alijiunga na chama cha wapigania uhuru wa MPLA mwaka 1964, muda mfupi baadaye alijiunga na chama cha FNLA.
Mwaka huohuo alipata fursa ya kufanya ziara maalumu China na aliahidiwa kupatiwa nafasi zaidi kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi na misaada ya zana za kijeshi.
Hatua hiyo ilitokana na mgongano wa kimasilahi, baada ya FNLA na MPLA kuanza kupingana kuhusu nani anastahili kupewa nchi iwapo watapata uhuru, hivyo muda mfupi baadaye wakoloni hao walitoa taarifa kueleza kwamba Savimbi anapigana kwa ajili ya masilahi yao.
Hatua hiyo ilisababisha kuungwa mkono na Marekani iliyokuwa na masilahi tofauti na MPLA iliyoungwa mkono na Wasovieti tangu mwaka 1974 na kilijipambanua kufuata mrengo wa Marxist-Leninst kuanzia mwaka 1977, wakati Savimbi alijipambanua kufuata sera za Mao na kuungwa mkono na China.
Vita baina ya MPLA na Unita hata hivyo ilikuwa na sababu nyingi za ndani na kwa hiyo kuanza kutumiwa kama chanzo cha mvutano wakati wa vita baridi baina ya Marekani na USSR.
Baada ya kupata Uhuru mwaka 1975, mwaka 1985, kwa msaada wa Serikali ya Marekani chini ya Ronald Reagan, taasisi ya Jack Abramoff kwa kushirikiana na wabunge wa Conservative iliandaa kongamano kubwa la kimataifa la demokrasia katika mji wa Jamba, huko katika Jimbo la Cuando, kusini mwa Angola ilipokuwa ngome ya Savimbi na huo ukawa mwanzo mpya kwa Savimbi.
Kupitia Taasisi ya Heritage Foundation ya Marekani ambayo kiongozi wake, Michael Johns na wenzake walianza safari za kila mara katika ngome ya Savimbi, Marekani ilijikita kumpatia msaada wa kujijenga kisiasa na kijeshi dhidi ya Serikali ya Angola iliyokuwa chini ya MPLA.
Marekani ilianzisha mkakati maalumu kwa ajili ya kumpatia Savimbi silaha za kisasa na mafunzo kwa wapiganaji wa msituni ili kumpa nguvu katika vita yake dhidi ya Serikali ya Angola ambayo ilikuwa ikiunga mkono sera za Kikomunisti chini ya USSR mjini Moscow.
Baada ya kunusurika katika mashambulizi karibu 15 ya kujaribu kumuua, akiwa ameripotiwa kuuawa katika mashambulizi hayo, hatimaye aliuawa Februari 22, 2002 kwenye mapambano na majeshi ya Serikali.
 
Alimwaga damu za waafrika wenzake kwa upumbavu wa kutumia na marekani baada ya adhima ya marekani kutimia wakasavimbi kwa risasi
 
Pengine alichokuwa anapigania kilikuwa na tija lakini pia aliua wananchi wasiokuwa na hatia indiscriminately. Mpaka leo Angola ni mojawapo ya nchi hatari sana kutokana na uwepo wa mabomu mengi ya kutegwa ardhini ambayo hayajaripuka.
d2abcdeef4260c8fc518e530008306bc.jpg
Mandela, Annan na akina Gaddafi walijaribu sana kusuluhisha mgogoro huu mpaka akapewa u-vice president lakini yeye alitaka kuwa rais kwa gharama yo yote ile. Ha got what he deserved na alitumiwa sana na Wamarekani na kama kawaida yao alipomaliza thamani yake wakamtupa kama mbwa!
532a48b0ddd36f15bfd9ee0eea9fd014.jpg
 
Anae ishi kwa upanga, atakufa kwa upanga.
Savimbi alikua kikaragosi cha Marekani(enzi za vita baridi) Kuu piga vita utawala wa kikomunist wa Angola, uliokuwa uki ungwa mkono na soviet union na Cuba baada kusambatika soviet union, Angola ikakubali mfumo wa vyama vingi na ikarudisha urafiki na marekani, ndio hapo Savimbi akawa adui wa maslahi ya Marekani. Marekani kwa kutumia shirika lake la kijasusi CIA ikaisaidia Angola kumwua Savimbi
3452857bee7f90aa1989061258489e8b.jpg
48a5fde226e2d3d62e1cfc32f6e0a2f9.gif
33518328e44755f55deee88c5dd00204.jpg
 
Pengine alichokuwa anapigania kilikuwa na tija lakini pia aliua wananchi wasiokuwa na hatia indiscriminately. Mpaka leo Angola ni mojawapo ya nchi hatari sana kutokana na uwepo wa mabomu mengi ya kutegwa ardhini ambayo hayajaripuka.
d2abcdeef4260c8fc518e530008306bc.jpg
Mandela, Annan na akina Gaddafi walijaribu sana kusuluhisha mgogoro huu mpaka akapewa u-vice president lakini yeye alitaka kuwa rais kwa gharama yo yote ile. Ha got what he deserved na alitumiwa sana na Wamarekani na kama kawaida yao alipomaliza thamani yake wakamtupa kama mbwa!
532a48b0ddd36f15bfd9ee0eea9fd014.jpg
kumbeee

kavuna alichopanda ,Ndomana mimi nasema haya makundi mengi duniani yapo kimslahi sana
 
SAVIMBI ngome yake kubwa ambaye alikuwa ame jizatiti na wapiganaji wake wenye silaha za kisasa toka marekani, ilikuwa HUVAMBO. Kwa miaka mingi jeshi la angola lilishindwa kupangua ngome hiyo lakini baada ya Makubaliano ya amani na kufanyika uchaguzi, ilibidi UNITA ya savimbi ivunje jeshi lake na UNITA ikawa chama cha kisiasa. Uchaguzi ulio fanyika Savimbi na chama chake cha UNITA walishindwa na savimbi akapewa umakamu rais, hapo yeye na wapinaji wake wachache hawakurithika wakarudi tena msituni, bila msada wa marekani ambaye mwanzo alikua akiwafadhili, ndio hapo mwisho wangome ya HUVAMBO na maisha ya Jonas Malhero Savimbi.
59a39b1ccac8d0f23bbde006d16366a9.jpg
7be66f4280651ef3d231538810df43a3.jpg
fe3743ee5d72f5b51f1896ee4c6bb4ac.jpg
595b8f141d898c961c2d50014b1f51a0.jpg
 
kumbeee

kavuna alichopanda ,Ndomana mimi nasema haya makundi mengi duniani yapo kimslahi sana
Wakati wa vita baridi yeye na Mobutu walikuwa vikaragosi wa Wamarekani ku-destabilize nchi zilizokuwa zinafuata siasa za kikomunisti ikiwemo Angola,Msumbiji na eneo zima la Afrika ya Kati na Kusini. Misaada yake ya kijeshi na pesa ilikuwa inapitia kwa makaburu Afrika Kusini. Shirikisho la Russia liliposambaratika na Angola ikaruhusu vyama vingi vya kisiasa; na kuanza kuuza mafuta yake Marekani basi umuhimu wake ukaisha na kama kawaida yao Wamarekani wakamtupa (kama walivyofanya kwa Saddam, Osama, Mobutu na wahanga wengine wa kihistoria).
dc8dc8c5df3eee286d18ef455b333d26.jpg
Wengi walishangaa sana alipoukataa u-vice president na kuamua kurudi msituni kuendelea kupigana wakati jeshi lake akiwa ameshalivunja. Wakati ule Marekani inahitaji sana mafuta ya Angola basi akawa ame-miskalikyuleti na ku-ovaestimeti umuhimu wake. Nasikia wanaume wa CIA walim-tag na GPS tracking device wakatuma makomando wao wakaja wakaongozana na wenzao wa Angola wakamfanyizia. Na huo ukawa ndo mwisho wake. Aliua wananchi wa Angola wengi sana na mpaka leo kuna mabomu madogo madogo ya ardhini yanayokadriwa kufikia hata milioni 5 yanasubiri kuripuka na yanaendelea kuua.
2ec4c097bf2c1e7ce04be84cf827c9aa.jpg
Tumwache aozee katika shimo la takataka la historia!
abe32cee8e8a834de85a738ec6574d70.gif
Hapa maiti yake inaangaliwa na wanakijiji. Nasikia alizikwa huko huko msituni na baadaye kaburi lake lilifukuliwa na mpaka sasa hajulikani alizikwa wapi. Ni yale yale yaliyofanyika kwa mwili wa Osama!
 
Wakati wa vita baridi yeye na Mobutu walikuwa vikaragosi wa Wamarekani ku-destabilize nchi zilizokuwa zinafuata siasa za kikomunisti ikiwemo Angola,Msumbiji na eneo zima la Afrika ya Kati na Kusini. Misaada yake ya kijeshi na pesa ilikuwa inapitia kwa makaburu Afrika Kusini. Shirikisho la Russia liliposambaratika na Angola ikaruhusu vyama vingi vya kisiasa; na kuanza kuuza mafuta yake Marekani basi umuhimu wake ukaisha na kama kawaida yao Wamarekani wakamtupa (kama walivyofanya kwa Saddam, Osama, Mobutu na wahanga wengine wa kihistoria).
dc8dc8c5df3eee286d18ef455b333d26.jpg
Wengi walishangaa sana alipoukataa u-vice president na kuamua kurudi msituni kuendelea kupigana wakati jeshi lake akiwa ameshalivunja. Wakati ule Marekani inahitaji sana mafuta ya Angola basi akawa ame-miskalikyuleti na ku-ovaestimeti umuhimu wake. Nasikia wanaume wa CIA walim-tag na GPS tracking device wakatuma makomando wao wakaja wakaongozana na wenzao wa Angola wakamfanyizia. Na huo ukawa ndo mwisho wake. Aliua wananchi wa Angola wengi sana na mpaka leo kuna mabomu madogo madogo ya ardhini yanayokadriwa kufikia hata milioni 5 yanasubiri kuripuka na yanaendelea kuua.
2ec4c097bf2c1e7ce04be84cf827c9aa.jpg
Tumwache aozee katika shimo la takataka la historia!
abe32cee8e8a834de85a738ec6574d70.gif
Hapa maiti yake inaangaliwa na wanakijiji. Nasikia alizikwa huko huko msituni na baadaye kaburi lake lilifukuliwa na mpaka sasa hajulikani alizikwa wapi. Ni yale yale yaliyofanyika kwa mwili wa Osama!
Dah shukran kwa kutujuza ,ila hawa watu nimeanza kuamka huwa siwaungagi mkono ,makundi yote yanayoanzishwa ,maana nyuma yao najua kuna mmarekaniii
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom