Jolie Detta: Mwanamuziki wa Kwanza wa kike kuimba bendi ya TP Okk Jazz

Wakuu nawasalimu hasa Wale wapenzi wa Rhumba wenzangu

Msanii Jolie Detta aliandika historia ya kuwa mwanamke wa Kwanza kurekodi wimbo katika band ya muziki maarufu tp okk jazz iliyokuwa chini ya Franco Makiadi iliyoanzishwa miaka ya 1950's

Kabla ya kuja okk jazz mwanadada huyu alikuwa akiimba bend ndogondogo zisizo na majina na hatimaye mwaka 1986 marehemu Franco alimsajili rasmi tp okk jazz ambapo kutokana na kipaji chake Cha uimbaji alitunga wimbo maarufu uitwao " Massu" uliovuma sana Kipindi hicho,pia Jolie detta aliimba wimbo mwingine "Layile" ktk bendi hiyo kabla ya kuhama na kujiunga na bandi nyingine ya Bozi Boziana.

Jolie Detta ambaye ni chotara,akizaliwa na babá mgiriki na mama m kongomani alitamba na nyimbo maarufu Kama Massu,darse likotino,naboya kosambua, Layile,chérie okamus n.k.

Baada ya kifo Cha mumewe kwa jina Ndeko(ambaye inasemekana alifariki kwa Ukimwi), Jolie alihamia nchini Angola.Kwasasa Jolie ameokoka na anaimba nyimbo za injili huko jijini Zurich Uswisi ambapo baada ya kuokoka amebadili jina kwasasa anaitwa Évangéliste mirriame na huduma yake ya kanisa inajulikana Kama "welcome karibu".

Miaka kadhaa iliyopita wakati akihojiwa,alijutia Sana miziki ya kidunia aliyoimba pamoja na Mambo yote ya anasa aliyofanya huku akisisitiza ameokoka na hapendi kutambulika kwa jina hilo la jolie akisisitiza jina la Évangéliste mirriame.

NB
Admins naomba Uzi huu usiunganishwe pamoja na kwamba kuna uzi huku Kipindi Cha nyuma kuhusu msanii huyu kuzungumzia nyimbo zake,lakini uzi huu ni special kwa ajili yake kwasasa (latest) hivyo naomba usiunganishwe.

Cc
Masiya
Lucas Mobutu
View attachment 2011749View attachment 2011750

luambo makiadi asante sana kwa post hii, mimi pia niliwahi mtafuta Jolie Detta mitandaoni na taarifa niliyopata ni kuwa alifariki, nimefurahi kujua kuwa ni mzima. Kwa kweli sauti yake ni ya dhahabu haswa katika wimbo Massu. Asante sana.
 
Alivyo kwa sasa
FB_IMG_1637393911063.jpg
 
Back
Top Bottom