Jolie Detta: Mwanamuziki wa Kwanza wa kike kuimba bendi ya TP Okk Jazz

luambo makiadi

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
10,295
8,258
Wakuu nawasalimu hasa Wale wapenzi wa Rhumba wenzangu

Msanii Jolie Detta aliandika historia ya kuwa mwanamke wa Kwanza kurekodi wimbo katika band ya muziki maarufu tp okk jazz iliyokuwa chini ya Franco Makiadi iliyoanzishwa miaka ya 1950's

Kabla ya kuja okk jazz mwanadada huyu alikuwa akiimba bend ndogondogo zisizo na majina na hatimaye mwaka 1986 marehemu Franco alimsajili rasmi tp okk jazz ambapo kutokana na kipaji chake Cha uimbaji alitunga wimbo maarufu uitwao " Massu" uliovuma sana Kipindi hicho,pia Jolie detta aliimba wimbo mwingine "Layile" ktk bendi hiyo kabla ya kuhama na kujiunga na bandi nyingine ya Bozi Boziana.

Jolie Detta ambaye ni chotara,akizaliwa na babá mgiriki na mama m kongomani alitamba na nyimbo maarufu Kama Massu,darse likotino,naboya kosambua, Layile,chérie okamus n.k.

Baada ya kifo Cha mumewe kwa jina Ndeko(ambaye inasemekana alifariki kwa Ukimwi), Jolie alihamia nchini Angola.Kwasasa Jolie ameokoka na anaimba nyimbo za injili huko jijini Zurich Uswisi ambapo baada ya kuokoka amebadili jina kwasasa anaitwa Évangéliste mirriame na huduma yake ya kanisa inajulikana Kama "welcome karibu".

Miaka kadhaa iliyopita wakati akihojiwa,alijutia Sana miziki ya kidunia aliyoimba pamoja na Mambo yote ya anasa aliyofanya huku akisisitiza ameokoka na hapendi kutambulika kwa jina hilo la jolie akisisitiza jina la Évangéliste mirriame.

NB
Admins naomba Uzi huu usiunganishwe pamoja na kwamba kuna uzi huku Kipindi Cha nyuma kuhusu msanii huyu kuzungumzia nyimbo zake,lakini uzi huu ni special kwa ajili yake kwasasa (latest) hivyo naomba usiunganishwe.

Cc
Masiya
Lucas Mobutu
download-1.jpg
download.jpg
 
Kuna wimbo niliupenda sana, nimejaribu kutafuta youtube nimeshindwa. Makumbuka kibwagizo kidogo:
Mugo simama turudi nyumbani kwetu nyumbani bwana

Unihurumie sababu yake ilipita zamani tutunze batoto betu babaaa!
Naomba mwenye kujua jina na muimbaji wa huo wimbo tafadhali
 
Kuna wimbo niliupenda sana, nimejaribu kutafuta youtube nimeshindwa. Makumbuka kibwagizo kidogo:
Mugo simama turudi nyumbani kwetu nyumbani bwana,
Unihurumie sababu yake ilipita zamani tutunze batoto betu babaaa!
Naomba mwenye kujua jina na muimbaji wa huo wimbo tafadhali
Nadhani mwimbaji wa wimbo huo ni LEAD ISSA
 
Kuna wimbo niliupenda sana, nimejaribu kutafuta youtube nimeshindwa. Makumbuka kibwagizo kidogo:
Mugo simama turudi nyumbani kwetu nyumbani bwana,
Unihurumie sababu yake ilipita zamani tutunze batoto betu babaaa!
Naomba mwenye kujua jina na muimbaji wa huo wimbo tafadhali
Wa Rhumba?
 
Back
Top Bottom