Jokes Mix

Jokes Mix

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
3,811
Reaction score
1,607
1. Mzee mmoja aliingia kwa daktari na kuanza kulalamika.
"Daktari, mimi nina matatizo. Cha kwanza, ninakwenda vizuri bila shida. Cha pili, ninaanza kujisikia kuchoka. Cha tatu, ninakuwa ninatetemeka mwili mzima. Cha nne, kizunguzungu, hata nikifika cha tano ninaweza hata kuzimia".
Daktari akamshanga yule mzee na kumwuliza, "Hivi mzee una umri gani?
"Miaka 87"
"Sasa kwa umri huo unataka Mungu akupe nini tena? Mimi nina miaka 50 lakini kumaliza cha pili shida"
"Mimi nataka niwezw kupanda vidaraja vyote vitano hadi kufikia mlango wa nyumba bila kuchoka."

2. Bosi mmoja anarejea kwake, muda wote yuko kimya, mawazo tele. Mkewe anamwuliza:
"Mbona hivyo mume wangu, una tatizo gani?"
"Nina tatizo kubwa sijui nilitatue vipi?"
Mwanamke anamsogelea na kumpa moyo:
"Usijali mume wangu wala usiseme tatizo lako, kwani daima tatizo lako ni letu sote. Enhe, umefikwa na nini tena?"
"Asante sana mke wangu, nilijua hutoniangusha. Ni hivi, sekretari wangu ni mja mzito na anatarajia kuzaa "mtoto wetu".
 
Hahahaaaa kweli hata mimi kwa babu nilijua ni yale mambo yetu
 
Ya kwanza ni super! Ya pili ni deja vu
 
ka hata mimi ni hivyo hivyo, nilifikiri ni mambo yetu!!
 
du! Mi nilifikiri kwamba babu anagonga vyombo namna hiyo kumbe...........
 
Back
Top Bottom