msisitizo ni muhimu mkuu, sisi walimu tunaamini mwalimu hata uwe mzuri vipi darasani kama haukazii maarifa baada ya kipindi wanafunzi wako wataambulia patupu. SHIBUDA yuko sahihi kabisa.
shibuda ana tamaa kuliko hata fisi. ukionza anaanza kujikosha kwa ccm anataka apate huruma ya ccm ili apate ubunge kupitia ccm hana jipya. anasema eti anaunga mkono serikali 2 sio tatu.huyu alishaona taa nyekundu kwenye kila chama cha upinzani hawezi kupata nafasi ya kujipatia ubunge ndio maana unaona anaanza kujisogeza ccm apate huruma kwa kuunga mkono serikali 2. mbona hakuyasema haya tangia mwanzo? baada ya kuona upepo unamwendea vibaya ameamua kuweka tumbo mbele
Alafu unakuta mtu ana watoto na familia ambao wanawajibika kushape-up jamii ya miaka 300 ijayo kama binadamu wengine lakini kwake hata miaka mitatu ni mingi kusimamia mawazo yake. Kweli hata kama ni matumbo yetu lakini nafsi zetu zitusute!anatumia falsafa ya abunuwasi, kukata tawi la mti huku amelikalia!!!!!
SIKU moja baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi, mkoani Simiyu, Bw. John Shibuda kutangaza kuachia ngazi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mbunge huyo ameibuka tena na kusema aliahidiwa kupewa helikopta mbili na uongozi wa chama hicho aweze kuzitumia katika kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010 lakini hakupewa.
Alisema uongozi wa chama hicho ukiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Wilbrod Slaa, ulimwahidi kumpa helikopta hizo kwenye kampeni zake na kumpigia debe Katibu huyo aliyekuwa akiwania nafasi ya urais.
Bw. Shibuda aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Malampaka, wilayani Maswa na kuongeza kuwa, alijitolea kutumia pesa zake katika uchaguzi huo na kuahidiwa kurudishiwa lakini mpaka sasa bado kurudishwa.
"Katika kampeni za mwaka 2010, mbali ya kuahidiwa helikopta, pia nilikuwa chanzo kikubwa cha Dkt. Slaa kupata kura nyingi kwa mara ya kwanza na kuongoza kwenye Wilaya ya Maswa akimzidi mgombea mwenzake kutoka CCM, Rais Jakaya Kikwete.
"Helikopta nilizoahidiwa, hata wakati wa kampeni sikupewa, nilipouliza niliambiwa nitapewa...mimi ndiye chanzo kikubwa cha Rais Kikwete kupata kura ndogo katika jimbo langu, nilitumia gharama zangu kumfanyia kampeni Dkt. Slaa," alisema.
Wakati huo huo, Bw. Shibuda alisema msimamo wake ni Serikali mbili na kusisitiza hawezi kuwaunga mkono wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao msimamo wao ni Serikali tatu ambazo zitawaongezea mzigo wananchi wangu ambao ni wakulima na wafugaji.
Bw. Shibuda alisema wananchi wake hawataki kuongezewa mzigo wa Serikali; bali wanataka kutatuliwa kero walizonazo hasa zinazohusu kilimo cha pamba, migogoro ya wakulima na wafugaji.
"Siko tayari kuunga mkono muundo wa Serikali tatu kwa sababu wakulima wa pamba wana matatizo makubwa katika bei ya zao hili na pembejeo, pia katika wilaya yangu kuna migogoro mikubwa ya wakulima na wafugaji inayopaswa kutatuliwa kwa serikali hii tuliyonayo," alisema Bw. Shibuda.
Katika mkutano huo, Bw. Shibuda alikwenda mbali zaidi akimfananisha Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Mwanasheria wa chama hicho, Bw. Tundu Lissu na kundi la Interahamwe lililochochea ubaguzi wa kikabila uliosababisha mauaji ya kimbari nchini Rwanda akidai mbunge huyo amekuwa mchochezi wa vita ndani na nje ya chama.
"Tundu Lissu ni Interahamwe kwani amekuwa mtu wa mchochezi mwenye tabia ya kuwatukana wenzake, hana tofauti na kundi hili kama wenzake walivyosababisha mauaji nchini Rwanda," alisema.
Chanzo: Habari leo
Magale John Shibuda; that is a little too late; you can shout yourself hoarse; haitasaidia kitu, wewe ni malaya wa kisiasa. nenda utakako. Good riddance & God speed
Sasa bunge la katiba waliobaki sijui 400, CCM wabunge wapo sijui 300 hivi ukijumlisha wakina Kingunge,Paul Kimiti,Shamsa mwangunga hao wote sio wabunge ninyongeza ya ccm ili 2/3 itimie ukiweka tena akina arfi,shibuda,leticia nyerere wameshafika 400.Kwanini Katiba isiwe ya CCM yaani mimi nasubiri sababu wajumbe wakamati wamebaki nyingine wapo 30 wkt ilitakiwa 50 halafu 2/3 wanaipata.Hapo ndipo NDIYOOO zinapokuwa kaulimbiu kwa kila Jambo.Nasema tena katiba hii ni ya CCM ole wenu mtupe matango pori?Ndugu, CCM haitoi katiba katika stage zote nne za mchakato wa Katiba.
Katiba inatolewa na wananchi wenye haki kisheria kupiga kura ya maoni baada ya katiba mpya kutungwa na bunge la Maalum.
Na sio kila professa ni mtaalamu wengine walikariri wakawa wanapiga A tuu.Usininukuu vibaya hapa ila point yangu ukiwa CCM wewe hata tukisema Wachina waruhusiwe kuingia bunge la katiba utasema NDIYOOOOO.Mimi nasubiri najua CCM kutupatia katiba wataweza sana sababu hata katiba ya sasa ilitungwa na wachache.Kwa hiyo sitoshangaa hata kura ya maoni mashati ya kijani ya katawala sababu tushazoea NDIYOOOOOO.Prof.
Kabudi alishawaambia si kila mwanasheria anaelewa mambo ya katiba,
akasisitiza katiba ina wataalamu wake. Tena akaelezea masikitiko yake
kwa wanasheria machiriku kama Lissu, ambao hawajui kitu lakini wanaongoza
kwa kubwatabwata.
Yeah ,hujakosea ni kweli ni tatizo kwa serikali ya magamba.watu wa ajabu sana CHADEMA, hivi kwa nini hawataki kukubali kuwa MBOWE na SLAA ndiyo tatizo?