John Shibuda: Tundu Lissu ni Interahamwe

John Shibuda: Tundu Lissu ni Interahamwe

msisitizo ni muhimu mkuu, sisi walimu tunaamini mwalimu hata uwe mzuri vipi darasani kama haukazii maarifa baada ya kipindi wanafunzi wako wataambulia patupu. SHIBUDA yuko sahihi kabisa.

Lazima Umpongeze Interahamwe Mwenzio Shibuda Mpenda Posho
 
Shibuda!! Kikwete aliutangazia umma wa Tz kuwa ni mara mia Dr Slaa achaguliwe kuwa Rais kuliko Lissu achaguliwe kuingia bungeni. Hivi ni jinsi Kikwete anavyomuogopa Mh Lissu. Ccm yote, Shibuda inclusive wanamuogopa na kumgwaya Lissu, kwa hiyo hazishangazi kauli kama hizi
 
Prof.
Kabudi alishawaambia si kila mwanasheria anaelewa mambo ya katiba,
akasisitiza katiba ina wataalamu wake. Tena akaelezea masikitiko yake
kwa wanasheria machiriku kama Lissu, ambao hawajui kitu lakini wanaongoza
kwa kubwatabwata.

Ukiwa CCM kama wewe kweli
kumjadili Tundu Lissu ni headache sababu anasema yale ambayo nyie
hamtaki yasemwe.Sasa nyie CCM ole wenu mtupe katiba mdebwedo?
 
Anaogopwa kwa sababu ni mchochezi sana.

Shibuda!! Kikwete
aliutangazia umma wa Tz kuwa ni mara mia Dr Slaa achaguliwe kuwa Rais
kuliko Lissu achaguliwe kuingia bungeni. Hivi ni jinsi Kikwete
anavyomuogopa Mh Lissu. Ccm yote, Shibuda inclusive wanamuogopa na
kumgwaya Lissu, kwa hiyo hazishangazi kauli kama hizi
 
Ni mwenda wazimu pekee anaeweza kumwamini Shibuda, sijui kwanini mtu wa umri kama wake bado ni NDUMI LA KUWILI.
 
Kabla ya uchaguzi wa viongozi wakuu ndani ya CHADEMA tutaendelea kusikia mengi hasa ikichukuliwa kuwa tarehe ya Uchaguzi imebadilishwa mara tatu.

Haya ndiyo matokeo ya baadhi ya viongozi ndani ya chama kujijenga katika misingi ya kilaghai.

Kila uchaguzi wa ndani ukikaribia, lazima kuna baadhi ya viongozi watapata misukosuko ndani ya CHADEMA na hata kufukuzwa uongozi na uanachama.

Tutaona na kusikia mengi!

Hivi huyu Mpuuzi mnaposema kaachia ngazi mna maana enyi kizazi cha laana akina MwanaDiwani?
Kwanini asifanye kama kile alichofanya Mpendazoea kutoka CCM.
Kule ndio kuachia ngazi,Shibuda njaa ndo zinamsumbua,eti 2015 sitagombea kupitia CHADEMA...mwenzake kambilia mahakaman abakizwe ma nyie Ma Nyumbu mnakuja kutaka kupotosha hapa...
 
Last edited by a moderator:
Shibuda mbona anarudia yale yale??
kama ana hoaja za maana aziweke hapa sio story zile zile za kila siku.
Mchawi akiwa anakata roho huropoka hovyo yale yote yaliyomjaa.

Halafu anadai eti kaachia ngazi Mpaka 2015,njaa ndo zinamsumbua huyu mzee.
Afanye kama alichofanya Mpendazoea tumsifu
 
Halafu anadai eti kaachia ngazi Mpaka 2015,njaa ndo zinamsumbua huyu mzee.
Afanye kama alichofanya Mpendazoea tumsifu

Hapa Ndio CHADEMA TUJIFUNZE TABIA YA KUCHUKUA WANACHAMA WA MIHEMKO KAMA HAWA KINA SHIBUDA.
 
bila chadema angekuwa mbunge???ccm si walikuwa washamtosa huyu domo kaya...kwani chadema alifuata helikopta?????
shibuta anaipendan ccm kwa roho moja huku upinzani alikuja tu kwa kuwa ccm ilimtosa na kumjali milioner kisena....bye bye shibuda rudi where you belongs to.
huku hakuna rushwa au kubebana
 
bila chadema angekuwa mbunge???ccm si walikuwa washamtosa huyu domo kaya...kwani chadema alifuata helikopta?????
shibuta anaipendan ccm kwa roho moja huku upinzani alikuja tu kwa kuwa ccm ilimtosa na kumjali milioner kisena....bye bye shibuda rudi where you belongs to.
huku hakuna rushwa au kubebana

2015 hagombei tena?
 
Kutokana na uzi huu nashawishika kuconnect the dots na kuona aya:

Tundu lissu ni msukule= ni mgonjwa= ni kichaa= ni interahamwe=ccM

Kwa kuwa prof. lipumba alitumbia interahamwe =ccM , then Lissu > interahamwe= ccM
 
SIKU moja baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi, mkoani Simiyu, Bw. John Shibuda kutangaza kuachia ngazi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mbunge huyo ameibuka tena na kusema aliahidiwa kupewa helikopta mbili na uongozi wa chama hicho aweze kuzitumia katika kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010 lakini hakupewa.

Alisema uongozi wa chama hicho ukiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Wilbrod Slaa, ulimwahidi kumpa helikopta hizo kwenye kampeni zake na kumpigia debe Katibu huyo aliyekuwa akiwania nafasi ya urais.

Bw. Shibuda aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Malampaka, wilayani Maswa na kuongeza kuwa, alijitolea kutumia pesa zake katika uchaguzi huo na kuahidiwa kurudishiwa lakini mpaka sasa bado kurudishwa.

"Katika kampeni za mwaka 2010, mbali ya kuahidiwa helikopta, pia nilikuwa chanzo kikubwa cha Dkt. Slaa kupata kura nyingi kwa mara ya kwanza na kuongoza kwenye Wilaya ya Maswa akimzidi mgombea mwenzake kutoka CCM, Rais Jakaya Kikwete.

"Helikopta nilizoahidiwa, hata wakati wa kampeni sikupewa, nilipouliza niliambiwa nitapewa...mimi ndiye chanzo kikubwa cha Rais Kikwete kupata kura ndogo katika jimbo langu, nilitumia gharama zangu kumfanyia kampeni Dkt. Slaa," alisema.

Wakati huo huo, Bw. Shibuda alisema msimamo wake ni Serikali mbili na kusisitiza hawezi kuwaunga mkono wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao msimamo wao ni Serikali tatu ambazo zitawaongezea mzigo wananchi wangu ambao ni wakulima na wafugaji.

Bw. Shibuda alisema wananchi wake hawataki kuongezewa mzigo wa Serikali; bali wanataka kutatuliwa kero walizonazo hasa zinazohusu kilimo cha pamba, migogoro ya wakulima na wafugaji.

"Siko tayari kuunga mkono muundo wa Serikali tatu kwa sababu wakulima wa pamba wana matatizo makubwa katika bei ya zao hili na pembejeo, pia katika wilaya yangu kuna migogoro mikubwa ya wakulima na wafugaji inayopaswa kutatuliwa kwa serikali hii tuliyonayo," alisema Bw. Shibuda.

Katika mkutano huo, Bw. Shibuda alikwenda mbali zaidi akimfananisha Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni Mwanasheria wa chama hicho, Bw. Tundu Lissu na kundi la Interahamwe lililochochea ubaguzi wa kikabila uliosababisha mauaji ya kimbari nchini Rwanda akidai mbunge huyo amekuwa mchochezi wa vita ndani na nje ya chama.

"Tundu Lissu ni Interahamwe kwani amekuwa mtu- mchochezi mwenye tabia ya kuwatukana wenzake, hana tofauti na kundi hili kama wenzake walivyosababisha mauaji nchini Rwanda," alisema.

Credit: Majira
 
Hata akina Zitto na Kafulila walitofautiana na cdm lakini lipofikia wakati wa maslahi mapana ya kitaifa 'wamechanganya na zao' kama JK alivyowaasa wajumbe wa BMK na historia tayari inawaweka kwenye mkondo sahihi.
Sasa huyu mheshimiwa anatumia falsafa gani kufanya anayoyafanya!?
 
Hata akina Zitto na Kafulila walitofautiana na cdm lakini lipofikia wakati wa maslahi mapana ya kitaifa 'wamechanganya na zao' kama JK alivyowaasa wajumbe wa BMK na historia tayari inawaweka kwenye mkondo sahihi.
Sasa huyu mheshimiwa anatumia falsafa gani kufanya anayoyafanya!?

anatumia falsafa ya abunuwasi, kukata tawi la mti huku amelikalia!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom