Kande
Senior Member
- Mar 15, 2016
- 116
- 106
John Shibuda, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini amesema adui mkubwa wa ustawi wa Demokrasia Tanzania ni njaa ya wanasiasa ambayo inawafanya kusumbukia matumbo yao na kuacha pembeni maslai ya taifa.
Amesema hayo leo katika mdahalo uliondaliwa na Twaweza kujadili Mstakabali wa Demokrasia ukiangazia wapi watanzania tumekosea katika kuendesha siasa za amani ana uzalendo.
"Ugonjwa mkubwa wa watanzania nia njaa, wanasiasa wanasumbukia matumbo yao na kuacha maslai ya taifa", amesema Shibuda na kuwataka watanzania waache unafiki na wapiganie demokrasia ya kweli kwa kuwapinga wanasiasa waongo.
Naye John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini amesema Demokrasia tunayoitaka ni demokrasia ya wananchi kuwa na uwezo na kuwa huru kufanya siasa na kuchagua chama wanachokitaka. Maoni yao yaheshimiwe lakini kuwaambia mmekosea kumchagua mgombea wa chama fulani sio dhana njema.