John Pombe Magufuli faces cash crisis

John Pombe Magufuli faces cash crisis

Magufuli kidogo azimie alivyoambiwa hazina BOT kuna laki mbili na nusu imebaki teh teh teh
 
Guys...hii issue ya financial crisis ni uzushi mtupu. Juzi hapa zaidi ya billioni 15 na ushee imepelekwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Na kana kwamba hiyo haitoshi, trillion 1.7 imekusanywa na TRA kwa mwezi wa huu wa kumi tu.

trillion 1.7 ukilipa mishahara ya wafanya kazi inabaki shing ngapi?
Gharama za mafuta kwa magari yote ya serikali inabaji shing ngapi?

Hataree sanaa
 
namba tutaisoma wote, haijalishi wewe ni ccm au chadema


Nawazingua hao wanaodhani Ukawa ndio wanaoisoma namba.

Kumbe wao ndio wanaoisoma namba zaidi kuliko sisi.
 
Guys...hii issue ya financial crisis ni uzushi mtupu. Juzi hapa zaidi ya billioni 15 na ushee imepelekwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Na kana kwamba hiyo haitoshi, trillion 1.7 imekusanywa na TRA kwa mwezi wa huu wa kumi tu.

Hivi hao The Citizen si ndio walikuwa wanaonyesha mikutano ya Lowasa hadi kenya? Hivi wanatutafuta nini?
 
Acha tule nyasi wote mmeipenda wenyewe ccm ni ileile wacha tuisome namba wote,mimi sikuichagua ccm.
Tuisome namba namna hii: 2015 = 2+0+1+5 = 8 = MAGUFULI (Tarakimu nane) ndo maana ya Mtaisoma namba. Naona hamkuelewa maana ya fumbo kwani mwaka huu ulikuwa mwaka wake wa ushindi. Kila anachokiguza kinakuwa kama atakavyo. Mko mpaka hapo?
So muungeni mkono ili nawe ubarikiwe kupitia baraka zake (JISHIKIZE AKUSHINDIE)
TUTASHINDAAA KWA JINA LA YESU
 
Kwa ushauri wauze ma v8 landcruiser na Nissan patrol zote zilizopo ofisi za serikali na mashirika ya umma wanunue rav 4,wadhibiti posho,wapunguze mishahara ya watumishi tra
 
Kweli tupu.

Uchaguzi huu ulikuwa uchaguzi wa "pesa"......napata harufu hela zilichotwa hazina maana hii ni tabia ya serikali nyingi za kiafrika kutumia rasilimali za nchi hovyo huku lengo kuu kusalia madarakani.
 
wakati mwingine inakubidi pia uangalie habari imeandikwa na gazeti gani.
 
Na issue ya TRA kutotoa taarifa kwa kuwa CCM imeswindle hela nayo imekaaje.Mambo mengine yanachefua sana.Magufuli nampenda,lakini mizengwe mingi iliyokuwepo kwenye uchaguzi na kabla ya kusimikwa kwake kuwa raisi nayo inanifanya nijiulize maswali mengi kuhusu yeye na kumuwekea kiza kinene.Kama alijua uovu wote CCM waliofanya ili yeye aweze kuwa rais, why did he keep quiet.Doesn't this show that he indorsed swindling by CCM where ever it was done including ESCROW,mifuko ya jamii,CWT,hazina,TRA nk.?Je,anayofanya sasa ni usanii?Maana kila mtu siku hizi ni msanii.Haya mambo ni magumu sana.Ngoja tusubiri tuone ataishia wapi.
Guys...hii issue ya financial crisis ni uzushi mtupu. Juzi hapa zaidi ya billioni 15 na ushee imepelekwa bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Na kana kwamba hiyo haitoshi, trillion 1.7 imekusanywa na TRA kwa mwezi wa huu wa kumi tu.
 

wewe ni sawa na mbuni anayeficha kichwa chake ndani ya udongo while kiwiliwili chote kinaonekana.
kapu jeupe pee.
Mwambie Tanroads hawajatangaza kazi mwaka huu mpaka sasa wakati zilitakiwa ziwe zimetangazwa miez 4 iliyo pita japo bunge lilipitisha bajeti yao.... tafakari...
 
CCM ni ileile.

Ukawa tutaisoma namba.

UKAWA hawezi kusioma namba maana hawana tofauti na raia wengine wa kawaida. Kwa sasa CCM hasa wale vigogo na wafanyabiashara wakubwa waliokuwa wanatumia jina la CCM kukwepa kodi ndo wanaisoma namba kwa sasa. JPM hana uswahiba hata kidogo aiseee. Kamuulize Lukuvi atakumegemea kilichompata na sijuwi kama hata unaibu waziri atapewa kipindi hiki.
 
magufuli ndio kwanza ana wiki moja.... mambo yatakaa sawa tu..!!!

#hapakaziTu

 
sasa kama hayo yanayozungumzwa na "the citizen " ni kweli maana ndio walewale kina NIPASHE ... basi imagine angekuwa rais ni lowassa angekuwa na madeni ya kulipa fadhila ...... kama sasa hivi vitalu vya gesi angekuwa ashagawa kwa washkaji zake....

yaani mungu ni mwema hili fisadi halikuwa Rais......


 
sasa kama hayo yanayozungumzwa na "the citizen " ni kweli maana ndio walewale kina NIPASHE ... basi imagine angekuwa rais ni lowassa angekuwa na madeni ya kulipa fadhila ...... kama sasa hivi vitalu vya gesi angekuwa ashagawa kwa washkaji zake....

yaani mungu ni mwema hili fisadi halikuwa Rais......



Yaani MUNGU ni mwema katuepusha sana na hilo fisadi la UKAWA, Tungeibiwa mpaka basi
 
Habari za Asubuhi GT's,


Nimeona magazeti ya Leo yakipambwa na taarifa za Mkurugenzi mkuu kushughulikia wakwepa kodi.


Naomba pia kuipongeza TRA kwa makusanyo mazuri. Baada ya pongezi hizo naomba kuendelea.


Awali ya yote kama nilivyosema hapo juu nimefurahi na taarifa Yake ya makusanyo na kuwa wako kwenye asilimia zaidi ya 90 ya malengo waliyojiwekea.


Kupitia taarifa hiyo naomba kuchangia yafuatayo ili tuendelee kuboresha zaidi ukusanywaji wa kodi ktk nchi yetu.


Ukusanywaji sahihi wa kodi utaondoa bajeti tegemezi na tutaweza kutoa huduma za jamii kwa wakati hasa tutakapobana matumizi yasiyo ya lazima.


1. JE MALENGO WALIYOJIWEKEA (Targets) YAKO SAHIHI??
Nauliza hivi baada ya ripoti kuwa na excellence performance wakati yeye mwenyewe anasema sasa amepewa rungu atashughulika wakwepa kodi hasa wakubwa.


Ina maana hii ripoti Yake hao wakwepa kodi wakubwa makadirio yao hayakuwekwa kwenye targets?


2. Je hao wakwepa kodi wakubwa (defaulters) ni kina nani? Mbona taarifa Yake haikuwataja???


3. Je hadi sasa kodi ambayo imekwepwa kwa maana kuwa iko due na haikukusanywa ni Tshs ngapi???


4. Je ana mikakati gani ya kukusanya hayo madeni ya hao defaulters? Nilitegemea kwenye ripoti Yake angetoa ultimatum kuwa baada ya mwezi wawe wote wamelipa hayo madeni vinginevyo sheria ichukue mkondo wake.


5. Atoe level ya compliance regional wise.


6. Tunataka kuona realistic targets katika ukusanyaji wa kodi. Sio kuweka low targets halafu watu wanajisifia tumevuka malengo wakati malalamiko ya watu kukwepa kodi ni kila mkoa.


7. Wakati wa kuweka malengo watenganishe kodi inayotokana na mishahara (PAYE) na hiyo ya wafanya biashara ili tuone magnitude ya ukusanyaji katika kila eneo.


8. Taarifa za walipa kodi na defaulters zisiwe siri Kama kuna nia ya kweli ya kuboresha mfumo wetu wa kodi.


Naomba wadau wengine muongezee hoja ili kusaidia suala zima la ukusanyaji kodi ktk nchi yetu.


Mwisho ni ushauri kwako wewe usiyelipa kodi ujue huduma mbovu ktk jamii na Vifo vinavyotokana na kukosekana fedha vinakuhusu.


Hizo damu ziko mikononi mwako. Kwenda kwako misikitini au Kanisani ni bure bora ulale nyumbani.


Pia mfanyakazi yoyote wa TRA anayeshiriki ktk uovu huo. Basi mikono Yake imejaa damu za watu waliokufa sababu ya kukosa huduma mbalimbali za jamii ambapo pesa hizo wewe unahusika kuzipoteza.


Kila mtu asafishe MIKONO Yake tuendelee na kazi kwa kasi ya UWAJIBIKAJI; UFUATILIAJI; na UADILIFU.


Karibuni kwa michango zaidi. Tanzania ni yetu sote na sisi ndio tunaoamua mustakabali wa nchi yetu.


Queen Esther

Hii post inabidi ipandishwe juu aisee.

Well done!
 
Back
Top Bottom