PreGE2025 John Mrema avuliwa uanachama wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,439
Reaction score
6,692
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia Tawi lake la Bonyokwa mkoani Dar es Salaam, kimemvua rasmi uanachama, John Mrema, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu, dharau kwa mamlaka halali za chama, na kukaidi misingi na maadili ya chama.

Kwa mujibu wa barua rasmi iliyoandikwa na kusainiwa Aprili 30, 2025 na Katibu wa Tawi, Solomini Kagaruki, ambayo Jambo TV tumepata kuiona, na ambayo ilitolewa na tawi hilo, Kamati Tendaji ya tawi hilo ilikutana Aprili 29, 2025 na kupitia tuhuma dhidi ya Mrema, kisha kufikia uamuzi wa pamoja wa kumvua uanachama wake kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006, toleo la 2019, ibara ya 5.4.3.

Miongoni mwa tuhuma zilizomkabili Mrema, aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, ni pamoja na dharau dhidi ya mamlaka za chama ambapo imeelezwa kuwa alisambaza barua ya wito ya kufika mbele ya kamati ya nidhamu kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuitikia kwa utaratibu wa chama, jambo lililotafsiriwa kuwa ni dharau kwa mamlaka husika.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tuhuma nyingine ni kukaidi maadili na misingi ya chama, ikielezwa kuwa akiwa bado katika mchakato wa kujieleza, alifanya mkutano na waandishi wa habari Aprili 22, 2025 na kutoa tuhuma hadharani dhidi ya chama chake, akibeza misimamo na programu za CHADEMA kinyume cha utaratibu wa ndani wa chama.

Barua hiyo imeeleza kuwa, kutokana na mienendo hiyo, Mrema amepoteza sifa za kuendelea kuwa mwanachama wa CHADEMA kuanzia tarehe 30 Aprili, 2025. Hata hivyo, amepewa haki ya kukata rufaa kwa ngazi ya juu endapo hataridhika na uamuzi huo.






Source: Jambo TV
 
Ana kadi yake ya kijani kule, watamrejeshea aendelee na maisha
 
Bora
 
Huku nje wanasisitiza uhuru wa kutoa maoni wakati ndani ya chama ni madikteta mtu akitoa maoni mbadala anafukuzwa chama, tukiwapa nchi tutaweza kuwakosoa kweli nyie madikteta uchwara?

Huwezi kumpa mtu nchi Bali una mpa ridhaa ya kuongoza. Halafu tofautisha mawazo mbadala na kwenda kinyume na maamuzi ya Mkutano Mkuu.
 
Kama anadhani ana nguvu akae nje ya CDM aone udogo wake
 
mze wa kulilia ruzuku Akaungane na akina hanje na mwakagenda huko sisiemu chama chenye ruzuku kubwa tuone akifaidi ruzuku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…