Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 573
- 2,555
Akizungumza na wandishi wa habari makao makuu ya Chama cha CHADEMA muda huu, Katibu Mkuu wa Cha CHADEMA John Mnyika amesema bado wanaendelea kupiga hesabu ya hasara zilizotajwa na CAG, ambapo hadi sasa wamepata jumla ya Tsh. Trilioni 2.
Kuhusu DPP Biswalo Mganga, CHADEMA inashauri kiundwe chombo tofauti cha Kijaji ili kufanya uchunguzi na hatimaye kumchukulia hatua kwa kuwa tume ya Haki Jinai haina uwezo wa kumchukulia hatua yoyote.
Pia, amesema Rais hajatoa muda maalum wa Makatibu wakuu kujibu hoja za CAG, CHADEMA ina wasiwasi kuwa hoja hizo zinaweza kuchukua muda mrefu pasipo kupata majibu, hali ambayo hutokea kila mwaka. CHADEMA imeshauri Rais atumie vyombo vyake vya kimamlaka kuhakikisha hoja za CAG zinapata majibu kwa wakati.
Katika hatua nyingine, Mnyika ametoa wito kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwajibika kwa kuwa yeye ndie msimamizi mkuu wa kazi za serikali, pia ni mtu anayewajibika na kufuatilia utekelezaji wa ripoti za CAG ambazo hazijafanyiwa kazi tangu ashike Wadhifa huo.